CHADEMA washinda kwa Sumaye, Nagu

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797


Sunday, 02 October 2011 20:50



bendera ya chadema.jpg
Bendera ya Chama cha Maendeleo (Chadema)

Waandishi Wetu Mwananchi

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeshinda kiti cha udiwani katika Kata ya Endasak, ambako ni nyumbani kwa Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mary Nagu ambaye pia ndiye Mbunge wa Jimbo la Hanang ilipo kata hiyo.

Ushindi huo wa Chadema sasa unakifanya chama hicho, kuwa na idadi sawa ya madiwani na CCM katika Halmashauri ya Hanang kwa kufikisha madiwani 12. Pia kila chama kina mbunge mmoja, Nagu na Rose Kamili ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema).

Kwa mujibu wa matokeo kutoka vituo 13 vya kura, mgombea wa Chadema, Hashim Muna alipata kura 1,244 wakati mgombea wa CCM, Lazaro Shauri alipata kura 1,183. Kura 62 ziliharibika.

Awali, Muna alikuwa Diwani wa CCM wa Kata hiyo, lakini alijiuzuru na kujiunga na Chadema baada ya jina lake kuenguliwa na chama hicho tawala alipokuwa akigombea nafasi ya uenyekiti wa Halmashauri ya Hanang.

Baada ya matokeo hayo, kuwekwa kwenye mbao za matangazo, wafuasi wa Chadema wakiongozwa na Mkurugenzi wake wa Uchaguzi, Jimbo la Hanang, Mustapha Akoonay ambaye pia ni Mbunge wa Mbulu waliibuka na shangwe.

Msimamizi wa Uchaguzi Kata ya Endasaki, Herman Jerojika alitangaza matokeo hayo saa 1:43 usiku baada ya kuyapokea katika vituo 13 kuwa mgombea wa Chadema ameshinda kwa tofauti ya kura 62 na wapiga kura walikuwa 2,489.

Katika uchaguzi mwingine wa udiwani, mgombea wa CCM Kata ya Engutoto, wilayani Monduli, Gideon Kimongishu ameibuka mshindi kwa kura 1,020 dhidi ya mgombea wa Chadema, Gilbert Mganga aliyepata kura 207. Waliojiandikisha walikuwa 3,569.

Uchaguzi huo ulifanyika baada ya aliyekuwa Diwani wa Kata hiyo Magdaline Shoo kufariki dunia Aprili, mwaka huu.

Huko Serengeti, Mara, Ryoba Marwa wa Chadema ameshinda udiwani wa Kata ya Stendi Kuu kwa kupata kura 650 wakati Tugoro Mboto wa CCM amepata kura 270 na Joseph Rhobi CUF 35. Msimamizi wa uchaguzi, Bhoke Ruhinda alisema kura zilizopigwa ni 964 , kura halali 955.

Manispa ya Shinyanga: Mshindi wa udiwani Kata ya Masekelo ni Zacharia Mfuko wa Chadema ambaye amembwaga mwenzake wa CCM, Rashida Mahenga. Akitangaza matokeo hayo, Mtendaji wa Kata ya Masekelo, Steven Masabo, alisema Mfuko alipata kura 1,080 dhidi ya 603 za mgombea wa CCM.

Habari hii imeandikwa na Mussa Juma, Hanang, Suzy Butondo, Shinyanga, Anthony Mayunga, Serengeti na Peter Saramba, Monduli.

 
oh yeah... lazima waangalie daftari la usajili; CCM wanalitumia kuongeza wapiga kura
 
nilipost huu ushindi tangu wakati wa kampeni na wachache hapa jf hawakuniamini
 
Ff cdm huwa hatufungi ndoa na wezi hata siku moja! Kilichofanyika kigoma ilikuwa ni kugawana vipindi vya kutawala,tofauti na cuf na magamba maana wao wanatawala pamoja na hii ndiyo ndoa,hivi kwanini uelewa wako ni mdogo sana? Hujui hata kutofautisha mambo?pole sana .
 
Hongera Chadema![/QUOTE ]

Lakini tusisahau kwamba kati ya kata 22, CCM imezoa kata 17 na Chadema 5 !!!! Vilevile tusisahau kwamba, wakati wakazi wa Igunga vijijini hawana elimu wala hawakusoma ndo maana wameichagua CCM; kata za Iringa Mjini nao wameichagua CCM!!
 
Pongezi kwa wananchi wote mnaotambua nini maana ya ukombozi. Big up chadema!
 
Back
Top Bottom