CHADEMA washauriwa kuhakiki ushahidi wa kura za Urais kwa Ernst & Young | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA washauriwa kuhakiki ushahidi wa kura za Urais kwa Ernst & Young

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Nov 3, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,643
  Trophy Points: 280
  Kuondoa hisia za "mwamba ngoma huvutia kwao" Chadema ninawashauri waajiri Ernst & Young au PRICE-WATERHOUSE COOPERS ambayo ni kampuni yenye sifa za kimataifa katika kufuatilia wizi wa aina zote za kalamu kwa utaalamu ujulikanao kama............."forensic auditing" ili kujua ni nani kweli kati ya Dr. Slaa na Jk alishinda Uraisi........

  Taarifa ya kampuni ya ukaguzi wa mahesabu yenye hadhi ya kimataifa kama hiyo ya PRICE-WATERHOUSE COOPERS au Deolette Touche zenye hadhi hiyo zaweza kutoa uchambuzi ambao utakubalika kimataifa na hivyo kumuumbua JK mchana kweupe kuwa kumbe ni mwizi wa kura.........

  Tukumbuke ni kampuni ya Ernst & Young ambao waligundua wizi wa EPA na hivyo tusidharau kwenye nyanja hizo kazi hii yaweza kuwachukua takribani wiki mbili hivi na taarifa yao kukabidhiwa kwa waangaliz wa kimataifa, ofisi za mabalozi wote hapa nchini na kwa JK mwenyewe ili tukae chini kama taifa na kupata ufumbuzi wa kudumu haswa wa hii NEC uchwara kabisa........
   
 2. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  hawaitajiki kwa sasa kwa kuwa chadema ina copy ya matokeo ya kila kituo ni suala la kuyajumlisha kwa calculater tofauti na ile ya tume ambayo inaonekana kuchoka kama si mbovu
   
 3. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #3
  Nov 3, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Ni kweli kabisa. Hata mie nakubaliana na hoja yako. Kwa nini tupoteze zaidi pesa yetu tunayohitaji kwa ajili ya maendeleo ya watu wetu?
   
 4. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2010
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kwa kujuwa nani kashinda hai-itaji uwe na kampuni ya kigeni, calculator ya buku inatoa majibu papo hapo. Jambo la msingi ni CHADEMA watujumlishie matokeo toka kwenye copy za mawakala watwambie tulishinda jimbo gani na kwa asilimia ngapi na za urais tulipata asilimia ngapi za ukweli. Hizi za tume ya uchaguzi ya CCM hatuzikubali. :A S 112::A S 103::A S angry:
   
 5. sensa

  sensa JF-Expert Member

  #5
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  We Ruta una matatizo kweli, ina maana sisi hatuji kujumlisha? Au wewe ndio hujui? Naomba urudi shule hesabu darasa la kwanza na la pili hutakiwi kuwa unachat hapa wakati mambo madogo kama hayo hujui.

  Ujinga Tanzania ni wa kiwango cha juu sana, duh nasikitika kweli.
   
 6. j

  joka Member

  #6
  Nov 4, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanakwetu naona mnapoteza muda wenu kufikiria mambo ambayo katika ulimwengu huu halipo. Huwezi kulazimisha watu wakuchague kwa nguvu. Mgombea wenu Dr slaa kashindwa kweli wala hajaibiwa.

  Nakubaliana na aliyesema kwamba chukueni vikokotozi vyenu kokotoa then utapata jibu mwenyewe. Tatizo ni kwamba mliamini na kujipa ushindi wakati uwanja nyie ni wageni na wajuzi wa porojo tu. Kwa sasa uchaguzi umeisha tulijenge taifa letu. Waamini hao wabunge wenu waloingia mjengoni basi waendeleze libeneke. Chao
   
 7. G

  GAMA LUGENDO Senior Member

  #7
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 131
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yes that is a very good idea.but sidhani kwa nchi yetu kam hiyo itapewa nafasi ya kufanyika auditing kama hiyo.cha muhimu hapa ni kwamba dr slaa aendelee kutoa incontrovertible evidence namna uchakachuaji ilivyofanyika ili dunia na wapenda demokrasia wajionee wenyewe.

  Historia ya mabadiliko ya kijamii inatuonyesha kuwa hakuna na wala hapatakuwa na mtu au chombo cha kuzuia mabadiliko yanayoletwa na jamii, bali kinachoweza kufanyika ni kuyumbisha au kuchelewesha mabadiliko hayo.

  CCM inaelekea ukingoni kwa vile kwa sasa haikidhi matakwa ya wananchi walio wengi, na kwa hivyo basi haina zaidi ya miaka 10 kuanzia sasa ni lazima itakufa tu na kubaki kuwa historia.time will tell, let's wait and we shall see.
   
 8. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #8
  Nov 4, 2010
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  .... iko mashine inayofanya spectral analysis ya hata wino uliotumika kuchapa pamoja na consistency ya karatasi. Ni rahisi sana kutofautisha DIFFERENT inks na kwa hiyo mchapaji pia. Haka kamashine kapo pale IB makao makuu ya Polisi pia...kama bado kazima.
  In short ni jambo rahisi sana.
   
 9. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #9
  Nov 4, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Sijakuelewa kabisa kwenye ushauri huu unachihitaji hasa. Yaani ni kama vile mtu anaumwa ugonjwa wa kimeta unamletea daktari wa mifugo kumtibu.
   
 10. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #10
  Nov 4, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  hata mimi nawashauri kuhakiki ushindi maana uchakachuaji wa hali ya juu umefanyika kwa kweli
   
 11. LeopoldByongje

  LeopoldByongje JF-Expert Member

  #11
  Nov 4, 2010
  Joined: Apr 28, 2008
  Messages: 373
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hii ni mbinu nyingine ya kuchelewesha kudai haki. Nakala za matokeo kutoka kwa wasimamizi kama zipo zitumike. Nadhani Dr. Slaa anachodai si wizi wa kura bali utoaji wa takwimu zinazotofautiana na zile ambazo zimetoka kwa wasimamizi wa kura majimboni.

  Hii haitaki mtu awe profesa au msomi kuliona. Kama Jimbo A msimamizi ametoa takwimu za kura kuwa 20 tume inatakiwa itangaze hizo na si 5 au 100. Kwa hili huitaji hao wataalam wa kimataifa kugundua udanganyifu wa makusudi ambao tume imejiijngiza kuufanya.
   
 12. L

  Lalashe Member

  #12
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hili swala la wizi wa kura ni nyeti na ni la ndani zaidi kuliko nje. Kumbuka waasisi wa makampuni hayo ni mabeberu unajuaje kama mabeberu wananufaika na kuwepo kwa Jk madarakani?

  Naamini wananufaika na ndo haswa JK anawatengenezea maisha bora hivyo basi Ernst and Young au Price Coopers hawana lolote la kuwasaidia watanzania. Find local solution using local means. :nono: mimi siwaamini inaweza ikawa njia ya kumtakasa mwizi.

  Kura zimeibiwa ushaidi upo mtu ashughulikiwe bila kujali ni mrembo au la
   
 13. C

  CLAY KITUMBOY Senior Member

  #13
  Nov 4, 2010
  Joined: Sep 8, 2009
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Slaa ni mjanja sana anajua jinsi ya kucheza na akili za watu, hajaibwa kura wala nini yeye ni bingwa wa kupagawisha watu.
   
 14. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #14
  Nov 4, 2010
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mhaambiwa kuwa dunia haitambui wala haijishughulishi Na chaguzi zenu Hadi Mkatane mapanga

  Mkianza kumwaga Damu Mtawaona Aljazeer, CNN BBC N.k.

  -Source: Propaganda CCM
   
Loading...