Mungi
JF Gold Member
- Sep 23, 2010
- 16,975
- 9,566
Wana Jf,
Kama mtakumbuka waziri mkuu juzi alitoa kauli ya serikali kuwa itagharamikia mazishi ya waliofariki katika milipuko ya mabomu na risasi Arusha.
Taarifa iliyothibitishwa ni kwamba Ndugu wa Marehemu wote wawili wamekataa serikali kujihusisha na mazishi ya ndugu zao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti ndugu hao wamesikitishwa na kitendo cha kushawishiwa kuwakataa CHADEMA, wamesema wao wapo na CHADEMA kwa kuwa wao pia ni wafiwa katika tukio ambalo lilitokea kwenye mkutano wao.
Leo hii miili ya marehemu wote zimesafirishwa kwenda makwao Tanga na Tabora, ambapo Mbunge Rose Kamili ndiye aliyeshughulikia taratibu zote ikiwa pamoja na kulipia gharama za usafiri, chakula na malazi kwa wote waliosafirisha miili ya ndugu zetu waliotangulia mbele ya haki.
Coster zote zimeondoka mapema leo kuelekea kwenye maziko.