CHADEMA wapinga muswada wa mchakato wa katiba mpya

safi sana, mambo ya kupelekwa pelekwa yamepitwa na wakati, watoe tamko mapema tumechoka, hii nchi c ya salima kikwete wala prince wala ****** mwenyewe,

Hapo utasikia gadafi kafufuka na ametishia kulipua mijadala yote ya katiba mpya, si mnajua intelejensia yetu?
 
ccm wanatafuta pa kutokea'katiba mpya lazima iwatoe madarakani'wapishe watanzania waendeshe nchi yao wenyewe
 
Dr. Slaa atupe feedback za mikakati ya kupinga mchakato onevu wa katiba mpya mara kwa mara ili tuelewe kinachoendelea, itasaidia kuimarisha msimamo.
 
Hivi hawa watu wanaugua ugonjwa wa akili au wana mapepo?. Ni mara ngapi wananchi wamesema wanataka kupunguza madaraka ya rais? Kwa nini hawasikii? Draft ya kwanza imekataliwa kwa makosa haya haya ya sasa, wanataka wananchi wafanye nini? waingie barabarani?

Muda wa kufunika kombe mwanaharamu apite haupo, miaka 50 tuna uzoefu wa kutosha. Warekebishe huo mswada au wasubiri Tahriri Square.

See U at Tahrir square!
 
Katibu mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa amesema Chadema haitambui mswada wa mchakato wa katiba mpya kwani umechakachuliwa na bado umempa madaraka makubwa Rais kuingilia mchakato huo.Dr Slaa ameonya kama serikali haitasalimu amri na kubadilisha basi Chadema itawaongoza watanzania kuupinga kwa njia zote itakazoona zinafaa. SOURCE-ITV SAA 2 HABARI

Jamani iyo rasimu yenyewe ipo wapi?
Wenye uwezo waiweke hapa tuangalie mapungufu.
 
Kombani at work! Kwa nini hawataki kuwasikiliza wananchi wanachotaka? Hii tabia ya kulazimisha mambo mwishoe itatugharimu kama taifa.
 
Inakuwaje wajumbe /Tanganyika 50% na Zanzibar 50% si wenzetu wanakatiba yao jamani ebu waitendee haki Nchi hii kwa kufanya mambo yanayostahiki kwenye swala hilo ,naunga mkono hoja mswaada huu tunaukaataa urekebishwe kukidhi haja ya wananchi
 
Zile enzi za uchaguzi wa kiongozi umpendaye na kivuli pembeni zimepitwa na wakati na siasa za kihuni sasa watanzania tupo macho na kweli tupo macho..Peoples Power....
 
Nami naunga mkono hoja.

............Tukumbushane lakini, hivi tumeshaandaa mswada mbadala ambao ndiyo utaongoza hoja kule mjengoni na baadae kwa wananchi (itakaposhindikana mjengoni)?

.......Je, tuna rasimu ya Katiba tuitakayo kwa ajili ya uamsho wa umma?

Umeuliza swali zuri mkuu hili la kwanza.

Mimi nilishawahi kutoa maoni hapa kwamba Katiba ni kitu nyeti kuliko hata kumpta Rais na wabunge wa nchi hii. Ni lazima tukubali kutumia Rasilimali zetu kwa ajili ya jambo hili bila kuogopa gharama kama sasa inavyoonekana serikali inataka kujificha kwenye kichaka cha gharama.

Mapendekezo yangu ni kutumia mfumo wa kuwapigia kura wajumbe wote wa baraza la katiba. Wajitokeze watu wapige kampeni tuwahoji kwa muda mrefu tu hata miezi mitano wakipita sehemu mbalimbali nchini yakiwemo midaharo mikubwa kila mahala. kuwepo na makundi(wakristo,waisilamu,wahindu,wasio na din,wanasiasa,vijana,wazee,wanawake, etc) yaainishwe na kila kundi lipewe idadi ya wawakilishi. watu waombe uwakilishi katika haya makundi ili wananchi wawapigie kura wanaona wanafaa.

Baada ya kuwapata labda jumla yao ni 300 basi watapiga kura kuchagua wajumbe kati yao wa tume ya kukusanya maoni kwa niaba ya baraza zima. Maoni yataletwa mbele ya baraza na kuchambuliwa kupata yanayofaa kuunda katiba mpya. Baraza pia litateua na kumwajili consultant wa sheria wa kuandika draft ya katiba mpya itakayo pigiwa kura ya ndiyo au hapana kwenye referundum.

Tukifanya hivyo tutapata katiba ya wananchi na si ya Raisi aliyopo madarakani.
 
Hivi a loser Dr. Slaa kwa nini kila kitu uwa anapinga tu yeye kwake uwa hakuna zuri..

Uzee unamuijia vibaya
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom