CHADEMA wapinga Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa kupiga marufuku Vikundi vya Ulinzi vya Vyama vya Siasa, ikiwemo Red Brigade.

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
May 30, 2017
2,869
3,188
Kufuatia kusomwa jana bungeni kwa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa, ambao pamoja na mambo mengine, unapiga marufuku vikundi vya ulinzi vya Vyama vya Siasa, vikiwemo: Red Brigade, Green Guard na vingine.

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema, pamoja na mambo mengine alipinga juu ya Muswada huo kupiga marufuku vikundi vya ulinzi na kudai kuwa, ulinzi ni jukumu la kila mtu kwa mujibu wa Katiba.

Hapa ndipo penye shida, kuna watu wanadai kila siku kuwa, wanapigania Utawala wa Sheria but still wanaonyesha kuwa, shida yao siyo kuheshimu sheria za Nchi bali wawe na uhuru wa kufanya wayatakayo kinyume na Katiba. Wanatamani Tanzania iwe a rogue State.

Hao wanaojidai kupigania Utawala wa Sheria, wamesahau namna Wajerumani walivyokuwa wakimpitezea Adolf Alois Hitler na Kikundi cha Sturmabteilung (SA) na pia kingine cha schutzstaffel (SS). Hivi vikundi licha ya kutoa show matata mitaani iliyowafurahisha Wajerumani waliokuwa very desperate katika miaka ya Inter-Wars Period (1918 - 1933) lakini ndivyo vilivyokuwa vikitumiwa na Manazi kuwafuatilia mbali Wapinzani wao wa kisiasa na makundi yaliyoonekana inferior katika jamii ya Wajerumani hasa Slavs na Jews. Hofu ya uasi na mapinduzi, ndiyo yaliyochangia sana Rais na shujaa wa kivita, Jenerali Paul Hindenburg kumteua Hitler kuwa Chancellor mwaka 1933.

Hayo hayo ya Ujerumani ndiyo hayo hayo yaliyokuwa yamemuweka madarakani Benito Mussolini nchini Italia muongo mmoja kabla. So, Historia ni mwalimu tena hakuna mwalimu mzuri wa ubovu wa vikundi hivi kama Ujerumani, hivyo natarajia CDU/CSU, pamoja na SPD waishauri CHADEMA juu ya madhara ya vikundi hivyo. Faida zake ni ndogo sana kulinganisha na madhara ya vikundi hivyo.

IMG_0165.JPG
 
Baadaye wazungu wakiwakaba koo watasema tena mabeberu wanatumia watu wasio wazalendo kuchonganisha nchi. Yetu macho na nasema wapitishe tu ila tusijeshikana uchawi. Tena waziri mwenyewe ni Jeniii!!! Ha ha haa.
 
Wapinzani wamekosa uongozi ndio maana wamebaki wanatapatapa.

Kuna mambo mengi tulitarajia azungumze Mbowe ,Lipumba ,Cheyo,Mrema, na wengine lakini hawaonekani wala hawasikiki.
Wao ni wababe tu wakisikia nafasi zao zimeguswa. Masuala mengine mapana kwa nchi hawayasemei wanawaachia akina Sugu na Lema.
 
Ccm wana vyombo vya dola lakini upinzani hawana lazima waendelee kuwa vikundi vya ulinzi

Hizo sheria wanatunga zitakuja kuwamaliza ccm wenyewe maana soon kinaenda kuwa chama cha upinzani

Mida huamua yote
 
Itakuwa sheria ya kijinga mno tangu kuanza mfumo wa vyama vingi vya siasa! Sheria inalenga watu badala ya maudhui! Hivi msajili atakuwa na uwezo wa kuidhibiti CCM?!!

Hivi CCM imejihakikishia utawala wa milele?!
 
Wapinzani wamekosa uongozi ndio maana wamebaki wanatapatapa.

Kuna mambo mengi tulitarajia azungumze Mbowe ,Lipumba ,Cheyo,Mrema, na wengine lakini hawaonekani wala hawasikiki.
Wao ni wababe tu wakisikia nafasi zao zimeguswa. Masuala mengine mapana kwa nchi hawayasemei wanawaachia akina Sugu na Lema.
WATASIKIKA WAPI WAKATI MMEWAZUIA KUONGEA? WAKIONGEA MNAWAKAMATA NA KUWAFUNGULIA KESI NA KUHARIBU MALI/UWEKEZAJI WAO, PIA MNAWAAMBIA KUWA WANATUMIWA NA WATU WASIOITAKIA MEMA NCHI? BARA WANYAMAZE TU MFANYE MNAVYOTAKA
 
Mkuu wakati mwingine kujibizana na watu kama hawa ni kujishushia heshima
Me ngoja niendelee kutafakari mabeberu ni kina nani na wanaotupa mikopo, misaada na ruzuku huku tukikenua meno yote nje na kuwazodoa wengine ni kina nani hao mabeberu. Kana ni mbuzi au viumbe wa kufikirika tu.
 
Kufuatia kusomwa jana bungeni kwa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa, ambao pamoja na mambo mengine, unapiga marufuku vikundi vya ulinzi vya Vyama vya Siasa, vikiwemo: Red Brigade, Green Guard na vingine.

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema, pamoja na mambo mengine alipinga juu ya Muswada huo kupiga marufuku vikundi vya ulinzi na kudai kuwa, ulinzi ni jukumu la kila mtu kwa mujibu wa Katiba.

Hapa ndipo penye shida, kuna watu wanadai kila siku kuwa, wanapigania Utawala wa Sheria but still wanaonyesha kuwa, shida yao siyo kuheshimu sheria za Nchi bali wawe na uhuru wa kufanya wayatakayo kinyume na Katiba. Wanatamani Tanzania iwe a rogue State.

Hao wanaojidai kupigania Utawala wa Sheria, wamesahau namna Wajerumani walivyokuwa wakimpitezea Adolf Alois Hitler na Kikundi cha Sturmabteilung (SA) na pia kingine cha schutzstaffel (SS). Hivi vikundi licha ya kutoa show matata mitaani iliyowafurahisha Wajerumani waliokuwa very desperate katika miaka ya Inter-Wars Period (1918 - 1933) lakini ndivyo vilivyokuwa vikitumiwa na Manazi kuwafuatilia mbali Wapinzani wao wa kisiasa na makundi yaliyoonekana inferior katika jamii ya Wajerumani hasa Slavs na Jews. Hofu ya uasi na mapinduzi, ndiyo yaliyochangia sana Rais na shujaa wa kivita, Jenerali Paul Hindenburg kumteua Hitler kuwa Chancellor mwaka 1933.

Hayo hayo ya Ujerumani ndiyo hayo hayo yaliyokuwa yamemuweka madarakani Benito Mussolini nchini Italia muongo mmoja kabla. So, Historia ni mwalimu tena hakuna mwalimu mzuri wa ubovu wa vikundi hivi kama Ujerumani, hivyo natarajia CDU/CSU, pamoja na SPD waishauri CHADEMA juu ya madhara ya vikundi hivyo. Faida zake ni ndogo sana kulinganisha na madhara ya vikundi hivyo.

View attachment 937218
Hiyo Red guard iko wapi zaidi ya kuwepo kwenye ofisini zao ili kulinda mali zao walizookoteza. Green guard ipo mitaani ikisaidian na dola hata kwenye mikutano ya viongozi wa kitaifa wao wanajipa jukumu la kuwalinda.
Hata hivyo kiwango chako cha kufikiri ni kidogo mno kwani umeacha mambo muhimu na kushabikia kitu kidogo! Acha utoto weka vitu muhimu ilivyovisema kama la msajiri kumfukuza uanachama mwanachama!
 
Kuhusu vikundi vya ulinzi, nadhani kuna sheria inyodhibiti makampuni binafsi ya ulinzi; sheria hiyo hiyo ndiyo pia itumike katika kudhibiti sungungu na na vikundi vyote vya ulinzi visivyokuwa vya kiserikali.
 
Back
Top Bottom