CHADEMA wanavyompaisha Zitto

Makonyeza

Member
Feb 2, 2020
69
252
Chadema wanavyompaisha Zitto:

Achana na habari za Polepole na manyang'unyang'u na maroroso yake, mganga keshakufa mteja lazima atapetape, habari ya mjini kwa sasa ni kitendo cha mwanasiasa Zitto Kabwe kuwasilisha ombi la kuachiwa mwanasiasa mwenzake na mwalimu wake wa Siasa Freeman Eikaeli Mbowe.

Ombi hilo liliwasilishwa na Zitto mbele ya Mheshimiwa Rais WA Jamhuri ya muungano WA Tanzania alipokuwa akifungua mkutano wa kujadili hali ya Demokrasia nchi ulioandaliwa na baraza la vyama vya Siasa nchini.

Ni mambo ya ajabu saaana, Mbowe yupo Gerezani lakini Chadema wameonesha kutopendezewa na kitendo cha mwenyekiti wao kuombewa msamaha, sijaisikia tamko lao rasmi, lakini hali ya mambo inaonesha hivyo na baadhi ya viongozi wao na wanachama wamesikika wakisema wao kama Chadema hawajamtuma Zitto kufanya hivyo, na yeye Zitto amethibitisha hili kupitia ukurasa wake wa Twitter, Dunia ina mambo ya ajabu sana.

Takriban vyama vyote kumi na tisa vilishiriki katika mkutano huo usipokuwa Chadema chama pekee kinachoamini katika mbinu ya kususasusa licha ya kwamba haijawahi kuwapa faida yoyote.

Kwanza acha nitoe hongera zangu kwa Zitto, Zitto kwangu kwa sasa namuona ni mwanasiasa anayetumia mbinu za kisiasa za karne ijayo, yaani mbinu ambazo wanasiasa wengine wameshindwa na wala hawajawahi kufikirika kuzitumia.

Ndiyo, mm nasema wanasiasa wengine wakiwemo wote wa Chadema wameshindwa kutafsiri mambo madogo sana yanayohitaji akili ya kawaida tu.

Zitto anafahamu, na ndivyo ilivyo kwamba 'ukikutana na Jumbe Sema shida zako zote', ndugu zangu wa Chadema hilo hawalijui. Ukikutana na Mama Rais WA Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hapo si ndio mahala sahihi pa kusema kwa Sauti kubwa kwamba MBOWE SIO GAIDI!

Usiposema mbele ya Rais ukasikika wapi pengine unaweza kusema Dunia ikakuelewa na hata ikikuelewa itakusaidia nini wakati haina mamlaka yoyote kukusaidia.

AU wenzetu hawajui kwamba Rais anayo mamlaka ya kuiambia Sheria kamata na sheria ikatii au akaiambia acha na pia ikamtii.
Hii ni ushahidi kwamba kumbe nguvu za Rais kikatiba hatizijui, na Sasa mbona tunalilia katiba mpya ilhali hata hii ya Sasa hatujui!!!!
Ni narudia tena, Rais anayo mamlaka ya kuitumia fimbo ya Sheria atakavyo yeye na dhana hiyo ndo ile inaitwa Nguvu ya Dola, mamlaka hayo ya kuitumikisha sheria ndio Dola hiyo na ndio sababu kiongozi anapata usingizi nyumbani kwake.

Rais anao uwezo wa kumuacha huru aliyeikosea sheria, na ikibidi, hii nakunong'oneza tu, anawe pia kuitumia fimbo hiyo ya Sheria dhidi ya viroboto wasumbufu, lakini Kiroboto akijitambua akaona radhi KUSAMEHEANA KUPO!

Lakini zaidi niwajuze, waTanzania sisi ni waungwana, Siasa ni GAME kila mmoja ana namna yake kuzicheza, Sasa katikati ya game unaweza kuzidiwa kwa kupigwa kabali vizuri, ile kabali ya Roho, acha ufala, piga mkono chini jamaa alegeze mkono, ukijifanya ngangali utakufa unajiona, ahsante Zitto kumsaidia Mbowe kupiga mkono chini kumuokoa Mwalimu wako wa Siasa.

Ni kweli Zitto hakutumwa na Chadema, lakini dhamira yake binafsi imemtuma na kujikuta akiwajibika kwa faida ya mwalimu wake.
Ebu jiulize kesho akifutiwa mashtaka mwenyekiti wao watamshukuru Zitto au hawatatambua kufutwa kwa mashtaka hayo, watasusia na kukataa kufutwa kwa mashtaka hayo kwa kuwa wao hawakuomba na wala hawana haja ya kufutiwa mashtaka mwenyekiti wao, kwa kuwa wao wanachohitaji ni katiba mpya na Mbowe sio Gaidi!

Hongera tena Zitto umepajua pahala sahihi pa kusema maneno sahihi, Mungu atakulipa na kukupaisha zaidi kisiasa na kukuongezea umaarufu zaidi, wenye akili wamekuelewa.

Lakini kabla sijamaliza nisisahau jambo, kwa mbali naona kila viashiria kwamba sehemu kubwa sana ya wanachama na viongozi wa Chadema wala hawajui wanahitaji nini kwa wakati huu, wao lililopo mbele Yao wa naenda nalo kama lilivyo bila kutafakari. Wamekuwa wasahaulifu na kusahau kwamba kususa hakujawahi kuwa msaada kwao.

Hii inatishia hata mustakabari wa chama hicho kwa siku zijazo kwa kujishushia umaarufu.

_20211216_155212.JPG
 
ZITTO ANAVYOWAFUNDISHA CHADEMA KUFANYA SIASA

FB_IMG_1639629177137.jpg
 
Zitto hapaishwi na yeyote anajipaisha mwenyewe na hata kama anapaoshwa na chadema kitu gani kinawauma nyie ambao kila siku mnaombwa chadema ife
 
Zitto kacheza dili i na CCM lime backfire. Mbowe si wa kumpigia magoti mwanadamu hiyo siku haipo.

Angekuwa ni wa kupiga goti angempigia JPM kabla ya kuvunjwa bilicanas.
 
Mbowe amewekwa ndani kama sehemu ya utawala wa kiimla wa serikali ya ccm kutaka kuua upinzani wa kweli ktk Tanzania.

Ndipo wanafanya usanii na Zitto eti ionekane anamuombea Mbowe msamaha wakati Mbowe hana kosa.

Hivyo inaonekana ktk nchi hii rais akipenda anakuweka ndani na ikimpendezea anakuachilia. Hii nchi imechelewa sana kupata katiba mpya ndio maana mambo ya kipumbavu yamekuwa mengi.
 
Zitto kacheza dili i na CCM lime backfire. Mbowe si wa kumpigia magoti mwanadamu hiyo siku haipo.

Angekuwa ni wa kupiga goti angempigia JPM kabla ya kuvunjwa bilicanas.
Mbowe na kamati kuu nzima ya CHADEMA walikwenda mwanza kwenye sherehe za uhuru kumpigia magoti Jiwe
 
Back
Top Bottom