CHADEMA wanataka mikutano ya hadhara wakati wanatangazia dunia nzima kuwa Tanzania kuna CORONA. Hivi wazungu watawaelewa hawa watu?

yakowazi

JF-Expert Member
Feb 9, 2012
1,740
2,000
CHADEMA Wanataka mikutano ya hadhara wakati wanatangazia dunia nzima kuwa Tanzania kuna CORONA!! Hivi wazungu watawaelewa hawa watu?

Lisu amekuwa akihojiwa na vyombo kibao vya kimataifa akisema Tanzania kuna Corona kweli kweli nyingi ya kutosha ila serikali inaficha taarifa!!! Ulaya sababu ya Corona mikutano ya hadhara ni marufuku

Hata leo hii mazishi ya Prince Phillip wa Uingereza yatakayofanyika kuanzia saa sita na nusu yatahudhuriwa na ndugu wa karibu wa familia ya Kifalme 30 tu

Sasa hata watanzania hivi CHADEMA tuwaelewaje? Mbowe mwenyewe kasema Corona Tanzania iko kibao serikali ilete chanjo yeye keshachanja!!! Halafu hapo hapo wanataka mikutano ya hadhara wanata kuua watu kwa Corona au?

20210417_102939.jpg
 
stakehigh

JF-Expert Member
Aug 9, 2019
5,441

pongezi zote kwa waliowaita hawa mabinti nyumbu, lowassa ni fisadi
 
Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
44,417
2,000
Huu sio muda wa mikutano,ni muda wa kazi

Siasa ni sayansi sio makelele,ukianza kelele unamshitua adui,wake up ....

Kwenye siasa ndio sayansi inatumika, ila kwenye kutibu covid ni kupiga nyungu na kujifukiza, uza ubongo huo dogo.
 
Shehullohi

JF-Expert Member
Jul 21, 2020
2,545
2,000
Utaratibu wa mikutano ya hadhara ya kisiasa kila uchao hauna tija. Utaratibu ule mzuri wa kuendelea na mikutano ya ndani udumishwe na utungiwe sheria na bunge.

Mikutano ya hadhara ya ihusishe tu viongozi wa serikali na wazungumzie utendaji wao wa kuwaletea wananchi maendeleo na kusikiliza kero.

Mikutano ya kisiasa isubiri mwaka wa uchaguzi na kwa kipindi maalumu cha kampeni. Na kwenye chaguzi za marudio.

Tusikubali kurudisha ule mradi wa kutapale wananchi na kuwachangisha fedha za hedikopta na gharama za mikutaono isiyokuwa na tija.

Viongozi wetu mchunge kauli zenu maana hazikawii kukuwindeni. Ukiwaambia wapinzani hakuna hii mikutano kwa sasa kwa nia njema tu. Watakuambia unatumia miguvu na mibavu kutuzuia kufanya mikutano pia sheria haipo kusimamia hili.
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
24,626
2,000
..na ccm hawataki mikutano ya hadhara wakati wanaitangazia dunia kwamba Tz hakuna corona. je, wazungu watawaelewa hawa watu?
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
30,438
2,000
Similarly, serikali ya CCM inakataza mikutano ya hadhara wakati inaitangazia dunia kuwa Tanzania hakuna CORONA. Hivi wazungu watawaelewa hawa watu?
CCM inasimamia inachokiamini inasemaCorona hakuna na inaonyesha kwa vitendo

Chadema mnaosema Corona ipo halafu hamsimamii maneno yenu hapo ndipo tatizo lilipo
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
30,438
2,000
Wanacho'press' ni freedom of assembly - hii haki ikiheshimiwa then wanaofanya mikutano watachukua tahadhari.
Wrong timing !!! Wana press kwenye nchi wanayotangaza imejaa Corona? Nani atawaelewa? Huku unasema Tanzania imejaa corona huku unataka mikusanyiko akili zimo hapo?
 
Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
44,417
2,000
CCM inasimamia inachokiamini inasemaCorona hakuna na inaonyesha kwa vitendo

Chadema mnaosema Corona ipo halafu hamsimamii maneno yenu hapo ndipo tatizo lilipo

Wakati wa JK ccm ilisema umeme wa maji tatizo ni mabadiliko ya tabia nchi. Wakati wa Magufuli wanasema umeme wa maji ndio mpango mzima maana ni wa bei rahisi! Hebu fafanua hilo fumbo la imani tujue msimamo wa ccm ulipo.
 
Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
25,337
2,000
Bavicha hawataki kabisa kujishughulisha na kazi nzito nzito zinazohitaji matumizi ya akili nyingi na nguvu,

Wanapenda zile kazi laini laini tu kama kupanda majukwaani na kudanganya watu.

Ndio maana wanapiga sana vita vitambulisho vya wamachinga kwani watu wakiwa na shughuli za kufanya watakosa wateja wa kuwapigia porojo.
 
Pac the Don

JF-Expert Member
Feb 17, 2021
1,581
2,000
CHADEMA Wanataka mikutano ya hadhara wakati wanatangazia dunia nzima kuwa Tanzania kuna CORONA!! Hivi wazungu watawaelewa hawa watu?

Lissu amekuwa akihojiwa na vyombo kibao vya kimataifa akisema Tanzania kuna Corona kweli kweli nyingi ya kutosha ila serikali inaficha taarifa!!! Ulaya sababu ya Corona mikutano ya hadhara ni marufuku

Hata leo hii mazishi ya Prince Phillip wa Uingereza yatakayofanyika kuanzia saa sita na nusu yatahudhuriwa na ndugu wa karibu wa familia ya Kifalme 30 tu

Sasa hata watanzania hivi CHADEMA tuwaelewaje? Mbowe mwenyewe kasema Corona Tanzania iko kibao serikali ilete chanjo yeye keshachanja!!! Halafu hapo hapo wanataka mikutano ya hadhara wanata kuua watu kwa Corona au?
Hapa nadhan lengo sio kuanza mikutano ya kisiasa, lengo ni kuondolewa kwa zuio la mikutano ya kisiasa then wataamua wenyew lin na kwa utaratib upi wafanye mikutano. BTW hakuna official report kuhusu uwepo wa Corona nchini na uchukuaji tahadhari. Tusubir wahusika watoe taarifa rasmi. So tutakuja kuwasema chadema pindi watakapofanya mikutano wakati kuna taarifa rasmi ya Corona na tahadhari zake.
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
30,438
2,000
Hapa nadhan lengo sio kuanza mikutano ya kisiasa, lengo ni kuondolewa kwa zuio la mikutano ya kisiasa then wataamua wenyew lin na kwa utaratib upi wafanye mikutano. BTW hakuna official report kuhusu uwepo wa Corona nchini na uchukuaji tahadhari. Tusubir wahusika watoe taarifa rasmi. So tutakuja kuwasema chadema pindi watakapofanya mikutano wakati kuna taarifa rasmi ya Corona na tahadhari zake.
Chadema wanatangaza hadi nje ya nchi sana kuwa Tanzania kuna Corona tele hizo taarifa huwa wanazitoa wapi wakati taarifa rasmi hazipo?
 
Pac the Don

JF-Expert Member
Feb 17, 2021
1,581
2,000
Chadema wanatangaza hadi nje ya nchi sana kuwa Tanzania kuna Corona tele hizo taarifa huwa wanazitoa wapi wakati taarifa rasmi hazipo?
Very interesting... Ungeweka ushahid jins wanavyotangaza huko nje ingekua vzr maan nimeshindwa kukujibu cz cna ushahid wala taarifa juu ya hilo la kusambaza habar nje ya nchi
 
Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,133
2,000
Wrong timing !!! Wana press kwenye nchi wanayotangaza imejaa Corona? Nani atawaelewa? Huku unasema Tanzania imejaa corona huku unataka mikusanyiko akili zimo hapo?
Lakini corana haindoi haki ya mtu (ingawa inaweza kui'limit' in some circumstances). Lakini Tanzania hakuna lockdown, hivyo sioni kama ni wrong timing kwa wao ku'press' freedom of assembly ambayo ni haki yao ya Kikatiba.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom