CHADEMA wanapodai demokrasia na utawala wa kisheria toka kwa serikali wanakuwa wanafikiria nini?

PRODA LTD

JF-Expert Member
Oct 20, 2016
1,005
1,333
Habari Jamii Forum
Kimsingi nina mambo mengi ya kuwaambia, ila nitasema moja. UCHAGUZI WA KANDA YA NYASA. Nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa uchaguzi huu ambao uliibua msuguano kati ya wagombea wakuu Peter Msigwa, na Patrick Ole Sosopi. Msuguano huu ulipelekea kuwepo kwa maneno yasiyofaa kwa hadhi ya mtu kustahili anayejiita KIONGOZI. Zilikuwemo kejeli na dharau za wazi kabisa. Chama kama chama kikanyamazaaaaa kama vile kimesafiri. Kampeni zikaendelea.... Zikafika ukingoni.... Chama kukaibuka na jina mfukoni.... Wakitoa sababu kuwa ni kwa maslahi mapana ya chama...
Aliyeachwa (Msigwa) naye alishiriki kutoa lugha zisizofaa.... (Juzi nilizungumzia hili jambo la lugha)

Nikajiuliza,
1. Hivi, hawa wanachadema wanapodai demokrasia na utawala wa kisheria toka kwa serikali wanakuwa wanafikiria nini? Kwanza wana kipi cha kufananisha kwa matendo yao? Wao wanawaaminisha watu kwamba wakipewa nchi wataleta demokrasia, kwa kurejea mambo yapi? Nakumbuka nilisema wao ni kama mbegu kitaluni, na mbegu zisipoota kitaluni zitafikaje kwenye shamba kuu?
Uchaguzi uliopita CCM ilituhumiwa kucheza rafu kwa wagombea ikiwa ni pamoja na uwepo wa majina ya mfukoni, jambo ambalo kwa chadema limejitokeza.... Sasa juzi niliposema vyama vya upinzani vina VINASABA vya Ccm hamkuelewa nasema nini?
Nilieleza pia, lazima kuwe na jambo la tofauti kati ya mkosoaji na anayekosolewa, kwamba mkosoaji asiwe na kosa lile lile analolikosoa

2. Maslahi mapana ya chama ni yapi? Kama wagombea wote wana kashfa kwa nini abakizwe mmoja? Haki iko wapi? Ukweli, uwazi na sheria ni nini kwa wanachadema?
Hili jambo linaweka pabaya sura ya chadema kama chama chenye wafuasi wengi zaidi baada ya Ccm. Sasa huu ni uchaguzi mdogo unakata watu unaacha mtu mmoja unasema amepita bila kupingwa.... Yaani kama wale waliokuwa wanagombea naye ni "faru" ama?
Kama anayepitishwa na chama ni mropokaji na mwenye lugha chafu, hayo maslahi ya chama yanayozungumzwa ni kuwa na hazina ya matusi ama vipi? Sasa kwa nini watu wasiwaite vichaa? Ccm kuna wanaosifika kwa matusi, na wapo wanajulikana na wanapitishwa, kazi yao moja tu, kutukana.... Sasa chadema nao wanataka kuhifadhi jamii ya matusi?

3. Hivi Msigwa anaweza kusimama katika nafasi hiyo na kujiita mshindi? Yaani nafasi ya kugombea upewe kama viti maalum utajiona nawe uko juu? Hii tabia ya "kupeana" nafasi ilishapitwa na wakati. Hamkujifunza Ccm kilichowapata? Bado hamjifunzi katika teuzi zinazoendelea? Hamkuwananga?

Maoni yangu.
Kuna siku moja nilisema hapa.

"gharama ya kufanya uchaguzi ni ndogo kuliko gharama tutakayoingia kuitengeneza nchi iliyoharibiwa na mtu asiyejali"
Kwa wanachadema nasema hivi, " toeni boriti jichoni mwenu ndipo muweze kuona kibanzi katika macho ya wenzenu"
Kwamba, ikiwa mtanyamazia mambo ya ajabu yanayofanyika ndani ya chama, hakika chama hiki kitakuwa kibaya kuliko Ccm. Ccm ni mbooooovu kuliko, na wengi wameondoa matumaini huko, sasa ninyi mlioaminiwa mbona mnasaliti wanachama wenu?

Kwanza muondoe udikteta wa maamuzi waliyonayo viongozi wenu, kisha mje mlete sera zenu za kupambana na UKUTA.
Pili, msimamie sheria na demokrasia kama ambavyo mko tayari kuendesha operesheni kuidai
Tatu, chama hiki kimeshapoteza ile hadhi yake. Kuna haja ya wanachama kuumana na viongozi wao ili chama kirudi kwenye mstari. Pengine kimeona watu wanajiamini kikabweteka, kikawa kama tembo iliyotiwa maji na mgema baada ya kusifiwa. Wanachama tokeni katika ukimya, semeni waziwazi na msiogope viongozi. Kama unakipenda chama usife kibudu, kiambie, kikosoe, maana bila wewe mwanachama, hakuna chama
4. Ni wakati viongozi wa juu wa chama wajitathimini kama bado wanaweza kusimamia na kukiendesha hiki au la!
 
Tatizo chadema wanapigania demokrasia wasiyoijua wao ni wa kwanza kunyooshea kidole ccm na serikalilakini ndani ya chama chao wanashindwa kuitekeleza kwa vitendo, chimbukola ugomvi wa zitto na mbowe ni pale zito alipotaka kugombea uenyekiti, mchakato wao wakutafuta mgombea urais kilikuwa kioja cha mwaka kwa chama kikongwe kama chao
 
Sio kwamba lipo chadema tuu...hata spika wa sasa hivi tunakumbuka alishampiga Mtu kwa Rungu hadi jamaa akazimia kisa kura za maoni..

Hili jambo limekuwa ni Hulka yetu wa afrika wengi...tupo tayari kuharibu kuliko kujenga..

Tulipaswa tuwe na nia moja kama kweli tunataka tufanye kitu cha kujenga nchi/chama.

Lakini watu wanakuwa na agenda zao za siri..ndo sababu kunatokea ugomvi hivyo...

Siku tukiweza kujitambua ndani ya vyama vyetu na tukafanya demokrasia kweli tutaweza pia kuweka Utanzania mbele wala hutajua ccm ni yupi na chadema ni yupi!


Chadema viongozi wenu wanaenda sana jumuiya za kimataifa..

Huwa wanajifunza nini ?
 
Vitu vilivyoifanya ccm ikakimbiwa na wanachama wao wengi ni huu udikteta wa kuweka watu wao, vijana wengi walikubalika sana ila bahati mbaya hawakuwa watu wa watu fulani wanaoitwa wakuu wa chama, ndio ikawa mwisho wao na hapo hapo wananchi wakatafuta mbadala (chadema/cuf )bila hata kupigana na mtu, kama watu wanataka kuamini ''maslahi mapana ya chama''na kujuana yatawaweka huru wasubirie kwenye chaguzi. Watu wamebeba siri nzito, ukiwanyamazisha watatafuta nj8a ya kujinasua.
 
Back
Top Bottom