Chadema wanapaswa kujipanga kwa hili kabla ya 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema wanapaswa kujipanga kwa hili kabla ya 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbelwa Germano, Apr 29, 2012.

 1. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hali ya sasa ya kukubalika kwa kasi kwa CDM inatoa tafsiri nyingi kuhusu mustakabali wa baadaye. Wingi wa Wanachama ni ishara ya kujitokeza kwao kushiriki katika kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama. Lakini kikubwa zaidi cha kutazama ni kwa jinsi gani uteuzi wa wagombea nafasi za udiwani na ubunge zitafanyika. Ni ukweli usiopingika kama CDM wasipokuwa makini kutatokea makundi kama yaliyopo ndani ya CCM na kusababisha loopholes kwa CDM na kutoa mwanya kwa wapinzani(CCM).

  Kama nilivyotahadharisha awali kunahitajika umakini wa kuwaandaa viongozi wa kamati za utendaji wa wilaya ambazo ndio zinasimamia upatikanaji wa wagombea kwa nafasi nilizoeleza awali. Bila kuweka mazingira mazuri makombora ya ufisadi yataelekezwa CDM na kurudisha imani kwa CCM.Ni ukweli usiopingika kama vita ya kuwania uteuzi kwa nafasi hizi itakuwa motomoto kwa CDM.

  Nawakilisha
   
 2. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Itakuwa vema zaidi kama utapendekeza nini kifanyike ili chama kizidi kuimarika positively.
   
 3. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Uchaguzi wa viongozi wa chama 2013 ndio utakaotoa sura sahihi kuhusu mwelekeo wa chama. Pamoja tuijenge Chadema.
   
 4. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,105
  Likes Received: 553
  Trophy Points: 280
  mtoa rushwa yeyote hapati nafasi cdm ndo maana kuna watu waliondolewa bavicha mpaka sasa wana hasira na chama.
   
 5. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Ndio kuna kazi ya kujijenga kimuundo na kimkakati. Naamini wanaliona na pengine wamekwisha anza kulifanyia kazi.

  Nijuavyo mimi kuna makundi mawili ya wanachama:
  1) Wanachama wapya kabisa (hasa vijana) - linahitaji elimu ya uraia, maadili, uongozi, uzalendo nk
  2) Wanachama na makada wanaotoka ccm (hili haswa ndio kundi lenye kuhitaji macho ya ziada)

  Lazima mamluki wamo humo humo so hilo likitokea halitushtui bali tunataka CDM iwe na uwezo na mipango ya kushughulikia mambo hayo bila kupoteza focus au maono ktk kuongoza dola na kuleta maendeleo kwa Tz.
   
 6. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #6
  Apr 29, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mambo kama haya ndiyo ambayo ninatahadharisha...iwapo chuki hizi zitakithiri maeneo mengi ya Tanzania bila shaka chama kitaathirika. Mfano: Jimbo la Tarime tulishindwa kwa ajili ni chuki hizi..vita kati ya Heche,Waitara na mgombea wa CUF ambaye alikuwa CHADEMA, bila umakini CDM itajikuta ikipoteza majimbo inayoshikili hivi sasa. Vilevile Mkosamali alisinda awali baada ya kung'olewa CDM kutokana na uthaifu huu wa kuangalia majina badala ya watu makini.
   
 7. kevin nathan

  kevin nathan Member

  #7
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na uhakika kama kwa sasa ndani ya chadema hakuna makundi , yapo japo hayajawa na mizizi mingi saana mfano watu wamekuwa wakipingana waziwazi ndani ya CDM hasa wakati wa kuteua wabunge wa viti maalumu hii ingepaswa kuwasilishwa kama topic isemayo NINI KIFANYIKE ILI KUDHIBITI MAKUNDI YANAYO ONESHA DALILI KU EXIST NDANI YA CHADEMA MAANA NI VIZURI KUYADHIBITI HAYAJAOTA MIZIZI MIKUBWA.
   
 8. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #8
  Apr 29, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Mleta mada hongera kwa kuleta thread inayojenga chama na sio kubomoa so nina imani kuwa viongozi wa CDM waliopo humu watayachukua na kuyatendea kazi hasa pale yatakapohitajika kwa muda muafaka. But cha muhimu ni kuwa kitu ambacho kitaweza kuiokoa CDM kutona na makundi ni uwepo wa democracy ya kweli na yenye nidhamu.
   
 9. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #9
  Apr 29, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Naam!Umeeleweka...ukweli una hulka moja, haupendi kujificha, kwa muonekano wa nje makundi hayapo ila yapo makundi ya kufikirika ndani ya CDM,jambo la msingi ni kuweka mkakati imara kuhakikisha hayajitokezi.
   
 10. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #10
  Apr 29, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Naunga Mkono hoja!Pia kuna kundi la fedha chafu ambalo ndio litaleta migogoro ndani ya chama. Wapo viongozi ambao watakosa uzalendo na kununuliwa katika kupata nafasi hizi ndani ya majimbo.
   
Loading...