CHADEMA wanamkana Tundu Lissu kisayansi kama walivyomtenda Dkt. Slaa, Lissu hana nafasi tena CHADEMA!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,609
141,429
Kwanza hakuna mtu anayeweza kumvua uanachama wa CHADEMA Mdee kwa sababu ana mizizi ndani ya chama kama alivyo Freeman Mbowe, Lucy Owenya na Grace Kihwelu.

Pili, Mnyika anajaribu kufahamu kinachoendelea lakini hakijui na siku ya Ijumaa ndio atakijua na huenda akajiuzulu.

Mzee Lowassa aliondoka CHADEMA lakini mzimu wake bado unaitafuna na hasa ule uwekezaji wake katika saikolojia ya wanachama wa CHADEMA.

Kiufupi, harakati za Tundu Lissu na amri zake haziendani na utamaduni wa CHADEMA na mabwanyenye wa Ufipa st hawazifurahii kwahiyo lazima waachane naye kisayansi.

Halima Mdee na wenzake wataruhusiwa na kamati kuu kuendelea na Ubunge na ambaye hatafurahishwa ataruhusiwa ama kujiuzulu nafasi za uongozi au kujivua uanachama.

Mungu wabariki wabunge wa CHADEMA.

Maendeleo hayana vyama!
 
Uko sahihi, Kama umemsikiliza vizuri Mnyika alikuwa anaongea na sauti ya kutetemeka hasa akiongelea vitu sensitive maana yake yawezekana yupo against Mbowe.

Kwa elimu ya Mdee na level yake chamani lazima awe na backup fulani kuongoza wamama 19 kuapa. Kihistoria Mnyika hana ubavu wa kumfanya lolote Mdee ndani ya CHADEMA nahisi kuna bomu kubwa linaenda kulipuka ijumaa kuigawa CHADEMA vipande vipande. Muda utaongea.
 
Uko sahihi, Kama umemsikiliza vizuri Mnyika alikuwa anaongea na sauti ya kutetemeka hasa akiongelea vitu sensitive maana yake yawezekana yupo against Mbowe. Kwa elimu ya Mdee na level yake chamani lazima awe na backup fulani kuongoza wamama 19 kuapa. Kihistoria Mnyika hana ubavu wa kumfanya lolote Mdee ndani ya Chadema nahisi kuba bomu kubwa linaenda kulipuka ijumaa kuigawa Chadema vipande vipande. Muda utaongea.
Leo Mdee amekua mheshimiwa, siku chache nyuma mlimtukana matusi yote.
 
Uamuzi wa hekima ni kuwaruhusu akina Halima Mdee kuendelea na Ubunge! Mnyika amejaribu sana kuwa defensive dhidi ya Mbowe ila tu anajaribu kum- tantalize Tundu Lissu.

Hata hivyo Tundu Lissu siyo mwanasiasa makini bali ni mwanaharakati mropokaji tu! Huwezi kuwa unatoa matamko yako binafsi then unataka yawe ndo msimamo wa CHADEMA.

Gharama ya kuwapoteza Tundu Lissu na Mnyika (ajiuzulu) ni ndogo kuliko kuwavua Wanawake hao 19 uanachama na hatimaye kuwataka wapoteze Ubunge wao ambao wamepata kwa mujibu wa sheria za JMT na si hisani.

CHADEMA mkijifanya ujuaji na ulimbukeni wa kuendeshwa na mihemuko ya social media warriors kama akina Kigogo 2014 tambueni imekula kwenu!

Vumbi la mgogoro wenu utatulia 2025 imefika na hamtapata hata Madiwani 10 Nchi nzima achilia Ubunge mtakaousikilizia Redioni tu.

Time is the best Judge let's wait and see!
FK
 
Leo nime prove kuwa wewe nawe ni wa hovyo kama wenzako! What kind of analysis is that? Kuna watu nimewapiga block kuepuka kupoteza muda kusoma rubbish! You are the next!
 
Back
Top Bottom