CHADEMA wanahukumiwa kabla ya kusikilizwa

sulphadoxine

sulphadoxine

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
2,264
Likes
12
Points
135
sulphadoxine

sulphadoxine

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2010
2,264 12 135
Haya wandugu naomba tujibu maswali yafuatayo:-

1.Katika purukushani za kumkamata muhalifu wa kike na ikatokea shanga,zikakatika,hijabu ikadondoka na saa ikapotea,kitendo hicho ni;
(a)shambulio la aibu
(b)utovu wa adabu wa mkamataji
(c)halali kwasababu bila hivyo vielelezo havitapatikana
(d)si halali kwasababu muhalifu mwanamke inabidi akamatwe na mwanamke na hayupo basi aachiwe'asepe'tu.

2.Polisi wa Tanzania ni wabovu kwa sababu;
(a)hawatumii akili bali hutii amri yoyote kutoka juu.
(b)wanapendelea chama tawala waziwazi.
(c)hawawapendi wapinzani.
(d)(d)majibu yote a,b,na c ni sahihi.

3.Kwa kuwahukumu chadema kuwa ni wahuni kabla ya kuwasikiliza Rajabu kiravu ni;
(a)mkurugenzi mzuri wa tume ya taifa ya uchaguzi.
(b)mkurugenzi mzuri wa tume ya taifa ya CCM.
(c)msimamizi mzuri wa maslahi ya chama tawala.
(d)majibu yote a,b,na c ni sahihi.

4.DC asiye jua ratiba za kampeni zinazo fanyika wilayani kwake ni;

(a)mvivu anaye pokea mshahara asio ufanyia kazi.
(b)mbumbumbu tu wa kazi ya ukuu wa wilaya.
(c)mbabaishaji tu ambaye ni kielelezo cha ubaya wa kuteua watu kwasababu tu ya ukereketwa wao.
(d)mtu safi anaye fanikishwa matakwa ya chama tawala.

5.Waandishi na wachambuzi wanaoilaumu chadema kwa kumkamata mtuhumiwa wa uhalifu;

(a)wanafanya kazi yao vizuri
(b)wanajipendekeza kwa ccm na watawala ili wapate safari na posho.
(c)hawajui walifanyaro kwasababu hawajasoma katiba ya nchi .
(d)mamluki wanao tumiwa na ccm kuvuruga upinzani.

6.Jukumu la kumkamata muhalifu ni la;
(a)polisi pekee.
(b)kila mwananchi.
(c)askari yoyote mwenye magwanda na silaha.
(d)vyama vya siasa.

7.Kama anaye paswa kumkamata muhalifu hataki yaani polisi wajibu wa mwananchi wa kawaida ni;

(a)kumwachia muhalifu aendelee kuvunja sheria.
(b)kumwachia muhalifu aende zake.
(c)kulalamika kwa polisi wale wale wasio taka kukamata.
(d)majibu yote a,b,na c ni sahihi.

8.Wanao sababisha amani kuvurugika katika kampeni za uchaguzi hapa tanzania ni;

(a)polisi wasio taka kutenda haki.
(b)wasimamizi wa uchaguzi na wakuu wa wilaya.
(c)viongozi wa ngazi za juu wano amuru polisi kufanya wanavyo taka na siyo polisi walivyo ona inafaaa.
(d)waroho wa madaraka wanaopendelea ccm kwa makusudi kwa matarajio ya kupandishwa vyeo.

Toa hoja sio vihoja.
 
Safari_ni_Safari

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2007
Messages
23,230
Likes
7,043
Points
280
Safari_ni_Safari

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2007
23,230 7,043 280
Tatizo hutasikilizwa......ila ni kweli
 
Mvaa Tai

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2009
Messages
6,173
Likes
2,212
Points
280
Mvaa Tai

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Joined Aug 11, 2009
6,173 2,212 280
Mkuu wa Polisi ameteuliwa na mwenyekiti wa CCM, mkuu wa wilaya mwenyewe ameteuliwa na mwenyekiti wa CCM, Mkuu wa wilaya alikuwa anafanya kazi aliyoagizwa na CCM. Je unategemea nini baada ya hapo hasa ukichukulia CCM ni chama chenye mbinu chafu katika kushinda chaguzi zake? Tujikumbushe miaka ile Omary Mahitah akiuonyesha umma visu vya CUF vilivyoingizwa kwa ajiri ya kuvunja amani na mpaka leo tunasubiri waliongiza hivyo visu wapelekwe mahakamani. Tatizo lao walizoea kuwahadaa wananchi kwamba Vyama vingi vitaleta ya Rwanda na Burundi na watu walikuwa wanaamini, wamesahau kabisa kwamba watu wanabadirika kifikra, Unaweza ukawadanganya watu wote kwa wakati mmoja lakini huwezi ukawadanganya watu wote kwa wakati wote, Sasa hivi wanaweza kumdanganya bibi yangu aliyepo Kasuru Kigoma lakini hawawezi kumdanganya na mjukuu wake kijana kama mimi, ninaamini vijana woote wameujua ukweli kuhusu CCM ila wana maslahi binafsi ambayo yanatofautiana kutoka mtu mmoja na mtu mwingine, kwa mfano mpaka sasa kuna vijana ambao ujanja wa kununua Tshirt na Kofia hawana wao inatosha sana kuwahonga Tshirt na Kofia, pia wapo wale ambao wanafanya biashara visivyo halali ili wawe salama wanalazimika kujifanya wao ni CCM damudamu mfano halisi ni maeneo mengi ya pembeni mwa barabara yenye vibustani vya kuuzia miti na maua, utakuta mtu yupo eneo lisilo ruhusiwa kibiashara ili kujihami anapeperusha bendera ya CCM au kufungua katawi ka wakereketwa wa CCM akiamini watu kama polisi na City hawatambuguzi kwa kujua ni mtu wao, Sijawahi kuichukia CCM kama hii miaka ya hivi karibuni
 
Mkuu saa ya ukombozi ni sasa.
 
Forum statistics

Threads 1,237,619
Members 475,675
Posts 29,294,978