CHADEMA wanahitaji huruma ya kisiasa. Mbinyo waliopata unatosha

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Kwa ujumla wamepata fundisho kuwa taifa letu linahitaji amani ndio maana kila mtanzania anataka kila hitaji la kisiasa lipatikane kwa amani.

Hakuna haja ya kulumbana na kuvutana juu ya suala lolote ambalo ni hitaji la kisiasa. Hakuna haja ya kuleta jazba na vitisho juu ya hitaji la kisiasa ambalo lina nguvu ya umma. Maana hakuna anayeweza kuishinda nguvu ya umma.

Hivyo basi kwa binyo walilopata CHADEMA ni dhahiri kuwa wamejifunza mengi. Na sasa watakuwa na subira juu ya kudai hitaji lolote lile la kisiasa maana hakuna haja ya kuleta vurumai pasipo kuwa na nguvu ya umma.

My take; Nguvu ya umma ni muhimu sana katika kudai katiba mpya, tusidhanie ni suala la CHADEMA peke yao.
 
Sema kukomolewa kwao ili kuwanyamazisha kunatosha wasidai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
 
Kuna tofauti Kati ya kukomoa, kumjenga na kumkomaza mtu mtu kifikira, uvumilivu na mbinu pia.
 
CCM ndio kuna mbinyo wa kisawasawa. Shaka na Mama wameshasema 2025 ni yeye tena. Hakuna mjinga yoyote wa kuchukua fomu.
Na itaandaliwa fomu moja tu. Ole wake mtu alete fyokofyoko yatampata ya Membe.
 
Hivyo basi kwa binyo walilopata Chadema ni dhahiri kuwa wamejifunza mengi. Na sasa watakuwa na subira juu ya kudai hitaji lolote lile la kisiasa maana hakuna haja ya kuleta vurumai pasipo kuwa na nguvu ya umma.
Wewe kwa akili ulizonazo na unazi unaona walipata mbinyo; huoni ushindi mkubwa zidi ya hao unaowashabikia ambao wamefanya kila lililondani ya uwezo wao kuwapa "mbinyo" CHADEMA bila ya mafanikio yoyote!

Unapoona mambo yanakugeuka na kuanza kukimbilia majigambo ya ushindi ujue una tatizo.
 
Sema kukomolewa kwao ili kuwanyamazisha kunatosha wasidai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
Kila anayefikiri chadema inabinywa na in stahiki yake kubinywa, Hugo akili hazimtoshi.

Mtoto ukimpiga kila siku,mwisho was Siku usipompiga atajisikia vibaya na atatafuta kupigwa.
Huo unaoita mbinyo,huko tuendako wanaobinywa watakuwa na kiu ya kubinywa.
TUKIFIKIA HAPO NCHI HAITATAWALIKA
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom