CHADEMA
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 488
- 2,468
Ikumbukwe kwamba waliotia nia ni wengi lakini ni wachache waliojitangaza hadharani , Sasa leo tega sikio ili usikie ni akina nani wengine Wazito sana waliotia nia ya kuomba Urais wa Tanzania kupitia Chadema .
Mungu ibariki Chadema
=======
----UPDATE----
Ndugu wanahabari
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinapenda kuutarifu Umma wa Watanzania kupitia mkutano huu kuwa jumla ya wanachama 11 wamejitokeza kutia nia ya kuwania uteuzi wa kupeperusha bendera, kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba, mwaka huu, ambao utahusisha pia nafasi za udiwani, uwakilishi na ubunge.
Wanachama hao ambao idadi yao na majina yao yanatangazwa rasmi kwa umma kupitia taarifa hii kwa vyombo vya habari, wamejitokeza, kila mmoja kwa wakati wake, ndani ya muda uliowekwa, kutangaza nia hiyo kwa kutekeleza Kifungu cha (1) cha Mwongozo wa Chama wa Kutangaza Kusudio la Kuwania Nafasi za Uongozi Kwenye Vyombo vya Uwakilishi Serikalini, kipengele cha (g), ambacho kinatamka;
"Kwa nafasi ya Uongozi wa Kitaifa ndani ya Chama na Urais taarifa za walio na kusudio la kugombea nafasi hizo zitawasilishwa kwa Katibu Mkuu na kujadiliwa na Kamati Kuu na kutolewa uamuzi kwa hatua zinazofuata."
Mtakumbuka kuwa mnamo, Juni 3, mwaka huu, Chadema kupitia tamko lililotolewa na Katibu Mkuu wa Chama, Mhe. John Mnyika, kilifungua rasmi mlango kwa mwanachama yeyote anayetaka kutia nia ya nafasi ya urais, kuandika barua ya kusudio lake Ofisi ya Katibu Mkuu wa Chama.
Hadi mlango huo wa kutia nia unafungwa rasmi Juni 15, mwaka huu, saa 10.00 jioni, ikiwa ni jumla ya siku 12 baada ya kufunguliwa, wanachama waliotekeleza kanuni hiyo ni hawa wafuatao;
Charles, Mwita Isaya
Lissu, Tundu A.M
Dkt. Majinge, Mayrose Kavura
Manyama, Leonard Toja
Mbowe, Freeman Aikaeli
Mch. Msigwa, Peter Simon
Adv. Mwanalyela, Gasper Nicodemus
Nalo, Opiyo G.O.M
Adv. Neo, Simba Richmund
Nyalandu, Lazaro Samuel
Shaban, Msafiri
Ndugu wanahabari
Ofisi ya Katibu Mkuu pia ilipokea barua iliyokuwa imeandikwa na vijana wa makundi mbalimbali ya waendesha bodaboda, kwa niaba ya mwanachama mmoja ambaye wao waliona anafaa kutia nia ya kuwania urais, lakini kwa kuwa barua hiyo haijakidhi matakwa ya kifungu hicho cha 1(g) cha mwongozo uliotajwa hapo juu, haijazingatiwa na hivyo hata jina la mwanachama huyo halijawekwa katika orodha ya watia nia wala hajatajwa hapa katika taarifa hii.
Hivyo basi, kufungwa rasmi kwa mlango huo wa kutia nia, kunaruhusu kuendelea kwa hatua zingine kwa mujibu wa taratibu za Chadema, kwa kuzingatia Katiba, Kanuni na Miongozo mbalimbali. Kwa mujibu wa mwongozo ulionukuliwa hapo juu, kwa sasa majina ya watia nia wote yatawasilishwa kwenye kikao cha Kamati Kuu ya Chama, ambayo nayo itatekeleza wajibu wake kwa hatua mbalimbali katika mchakato huu kwa kuzingatia ibara ya 7.7.16 ya Katiba ya Chadema.
Ni vyema pia tukawakumbusha wanahabari na wananchi wote wanaofuatilia mchakato huu kuwa, hatua hii ya kutia nia ilihusisha kuandika barua kwa Katibu Mkuu na si kuchukua na kurudisha fomu. Hatua nyingine zinazofuata zitatangazwa baadae.
Imetolewa leo, Jumatano, Juni 17, 2020 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Chadema