CHADEMA wanaamini ikipatikana Katiba mpya CCM itaondolewa madarakani kidemokrasia kitu ambacho siyo kweli

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,885
141,816
Katiba ina mambo mengi na swala la Tume ya uchaguzi na taratibu zake ni sehemu kipande tu cha katiba.

Chadema wanapigania Katiba mpya kwa maslahi ya kimadaraka zaidi na siyo maendeleo ya jamii, ndio maana kilio chao kikuu kimekuwa ni Tume huru ya uchaguzi.

Niwakumbushe tu Chadema kuwa Katiba mpya siyo turufu ya kuitoa CCM madarakani bali vinahitajika vyama vya upinzani Imara visivyoendekeza njaa kuweza kuikabili CCM.

Ukiwa na vyama visivyo na njaa hata kwa katiba hii uchaguzi utakuwa huru kwa sababu wenye vyama vyao watalinda kura zao na hii tuliiona 2015 kule Iringa, Kawe, Mbeya, Arusha, Tunduma na Ubungo kwa Saed Kubenea.

Maendeleo hayana vyama!
 
Kwa bahati mbaya unaongea kinyume chake. Wanaccm wote wanaogopa katiba mpya maana wanajua wako madarakani kwa udhaifu wa katiba hii. Eti kulinda kura, ukiwa na katiba mpya ya wananchi, tume itakuwa huru, hakutakuwa na haja ya wananchi kwenda kulinda kura kama huko Iringa nk. Uchaguzi utakuwa kama inavyokuwa mitihani ya taifa ambapo wananchi hawaendi kulinda bali polisi tu.
 
Kwa bahati mbaya unaongea kinyume chake. Wanaccm wote wanaogopa katiba mpya maana wanajua wako madarakani kwa udhaifu wa katiba hii. Eti kulinda kura, ukiwa na katiba mpya ya wananchi, tume itakuwa huru, hakutakuwa na haja ya wananchi kwenda kulinda kura kama huko Iringa nk. Uchaguzi utakuwa kama inavyokuwa mitihani ya taifa ambapo wananchi hawaendi kulinda bali polisi tu.
Unasema sisiem wote hawaamin kuhusu katiba mpya ilhali haohao sisiem ndio walioasisi mchakato wa katiba mpya
 
Bila utawala nzuri unaowajibika, bila mwongozo wa kuuwajibisha ie katiba, sahau maendeleo. Watu watagombea usingizi si kuwatumikia wananchi, bali maslahi binafsi.
 
Katiba mpya kwa waTanzania itawaletea vitu vitatu muhimu
  1. Uhuru
  2. Haki
  3. Maendeleo ya watu
UHURU WA KWELI : Tangu mkoloni mweupe aondoke akaingia mkoloni mweusi CCM bado watanganyika na wazanzibari wanatafuta uhuru wao toka kwa wakoloni weusi. Uhuru wa kuchagua viongozi wao ngazi zote ktk utumishi wa umma na uwakilishi bungeni. Uhuru wa kuwawajibisha viongozi wazembe, wala rushwa, walioshindwa kulinda katiba n.k

HAKI : Haki katika nyanja nyingi hakuna mfano serikali ya mkoloni mweusi inasema inamiliki ardhi yote kupitia kwa rais kiasi wananchi wanaweza kubomolewa majumba, kuhamishwa bila fidia stahiki n.k n.k. Haki ya elimu bora kwa wote badala ya wengine kwenda shule za kata na kumaliza shule wakiwa raia daraja la pili kutokana na elimu isiyo ya viwango. Haki ya kupata matibabu sawa kwa wote bila kujali wewe ni kiongozi, mbunge n.k Haki ya kuwa na hospitali kubwa za kiwango cha Mlongozila, Muhimbili, Bugando ktk kila wilaya nchini.

Haki nyingine iliyopokwa ni Jeshi la Polisi halitumii PGO, ofisi ya DPP kupeleka mashtaka kwa shindikizo lisilo na haki au kufuata sheria, Mahakama na asasi zote ktk mfumo wa jinai haki (criminal justice system ) kuhakikisha watanzania wengi wasiwe wahanga wakuhangaika kupata haki.

MAENDELEO YA WATU: watanzania waweze kuanzisha biashara na shughuli zingine za kiuchumi kama ukulima, uvuvi na ufugaji bila vikwazo visivyo vya lazima kupata leseni, nyavu pia maboti ya kisasa, maeneo maalum ya ufugaji na huduma zake ili kuondokana na mapigano ya wakulima na wafugaji. Upatikanaji wa pasipoti kwa urahisi ili watanzania waweze kutoka na kuingia nchini ktk harakati za kutafuta maisha ughaibuni. Diaspora kutambulika kama kundi maalum na kupatiwa uraia pacha waweze kushiriki kuleta maendeleo kwao binafsi na kwa kushirikiana na watanzania wengine waliopo nyumbani. N.k
 
johnthebaptist, hwa nakuona kama mtu sensible kukubali ukweli kama Polepole alivyokuwa anakubali kuwa panapo uchaguzi wa huru n haki CCM ijiandae kukabidhi dola. Kweli unadhani kama kuna uchaguzi wa huru na haki (at least tume huru tu yenye composition ya vyama vyote...) CCM itasimama? Uwe mkweli sometimes! Kwanza LISU alishinda!
 
Unasema sisiem wote hawaamin kuhusu katiba mpya ilhali haohao sisiem ndio walioasisi mchakato wa katiba mpya

Ccm hawakuasisi mchakato wa katiba mpya, bali baada ya uchaguzi wa 2010 ccm kusumbuliwa na hoja ya katiba mpya na cdm, JK kwa shingo upande ikabidi akubali mchakato wa katiba mpya ili kupooza joto lilikuwepo. Usichanganye JK kukubali mchakato wa katiba mpya kama rais, na uasisi wa hoja hiyo. Jitahidi kutengenisha mambo hayo.
 
Back
Top Bottom