CHADEMA wamtelekeza Mwenyekiti wa BAVICHA wilaya ya Geita, Mhere Mwita baada ya kupata ajali Dodoma

Status
Not open for further replies.

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,372
image.jpg


Wadau, Amani iwe kwenu.

Hakika hujafa hujaumbika. Kwanza kabisa nitumie fursa hii kumpa pole Kamanda MHERE MWITA, Mwenyekiti wa BAVICHA wilaya ya Geita kutokana na maumivu anayopata sasa. Mhere Mwita alipata ajali tarehe 3 Oktoba 2016 Mjini Dodoma alipoenda kushuhudia hukumu ya viongozi wa BAVICHA Taifa walioshtakiwa kwa makosa ya uchochezi.

Mhere alienda Dodoma akitokea kwao Geita alipoenda kusimamia Operesheni ya Simika Bendera za CHADEMA. Kwa maana nyingine ni kwamba Mhere alipata ajali akiwa kazini, Ajali Kazini! Kwa hapa CHADEMA hawawezi kukwepa uwajibikaji.

Chanzo cha ajali mpaka sasa hakijaelezwa na CHADEMA wamefanya siri kuu kueleza nini kilitokea. Tunaambiwa kuwa baada ya kupata ajali hiyo ambayo ilisababisha Mhere kuvunjia mguu kwenye maungio ya kiuno na mguu, alisafirishwa hadi Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kitengo cha MOI tarehe 4 Oktoba 2016.

Katika hali ya kushangaza, usiku huo huo wa tarehe 4 Oktoba, wafuasi wa CHADEMA ambao ni wanachama wa BAVICHA walionekana wakifanya tafrija Jijini Dar es Salaam kusherehekea ajali hiyo ijapokuwa ilielezwa kuwa ni sherehe ya kuzaliwa ya Ben Saanane.

Tulihoji hapa iweje CHADEMA waandae tafrija karibu na Muhimbili ilhali mwenzao yupo hoi kitandani? Hatukupata majibu. Miongoni mwa waliokuwemo kwenye sherehe hiyo ni ELIZABETH MAMBOSHO aka KWINTARA KWINYARA, BEN SAANANE, MALISA GJ, HILDA NEWTON, DR. CRHSTOPHER CYRILO nk.

Baada ya kukaa Muhimbili kwa muda mrefu, Mhere Mwita alitolewa Hospitalini hapo na kupelekwa kwa ndugu yake kutokana na gharama za matibabu kuwa kubwa huku wafuasi wa BAVICHA wakipungua hospitalini hapo siku hadi siku..

Mhere ameishi kwa ndugu yake kwa mateso makubwa kutokana na maumivu aliyopata. Jitihada za kupata msaada kutoka kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, FREEMAN MBOWE ziligonga mwamba.

Kutokana na ugumu huo, ndipo alipopata wazo la kushiriki kampeni za Uchaguzi Mdogo, Kata ya Kijichi ambako alitegemea atapata chochote kitu. Mbuzi wa Maskini hazai. Licha ya kutumika kote, CHADEMA hawakumpa chochote kitu zaidi ya kumnunulia maji ya kunywa. Inasemekana kuwa Ally Bananga aliyeteuliwa kuongoza kampeni kwenye Kata hiyo aliwadhulumu wenzake kiasi kikubwa cha fedha.

Kutokana na dhuluma hiyo, ndipo tarehe 8 Februari 2017 alipolazimika kuondoka Jijini Dar es Salaam na kurejea kwao Geita ili akapate uangalizi wa karibu kutoka kwa Baba yake Mzazi, Mzee Mwita. Hata hivyo, pamoja na mapenzi aliyonayo kwa mwanaye, Mzee Mwita hana fedha za kugharamia matibabu ya mwanaye.

Kiasi kinachohitajika ili apate matibabu kwa ukamilifu wake ni zaidi ya milioni 3.5. Ndipo Mhere Mwita alipopata wazo la kuuza kiwanja chake kilichopo Geita Mjini ili apate kiasi hicho cha fedha ili kunusuru maisha yake.

Nimesikitika sana. Nimeumia sana. Imenishangaza sana. Hawa CHADEMA ambao walichanga zaidi ya milioni 7 kama dhamana kwa kijana mmoja aliyehukumiwa kwa kuwatukana viongozi wa Serikali ijapokuwa hana mamlaka yoyote kwenye chama wameshindwaje kumsaidia Mwenyekiti wa BAVICHA Wilaya ya Geita?

Ni kweli wameshindwa ama hawataki kumsaidia? Na kama hawataki kumsaidia, tatizo hasa ni nini? Amewakosea nini CHADEMA? Au kwa kuwa yeye hatoki Arusha au Kilimanjaro? Yaani yule mtukanaji kwa kuwa tu alitoka Arusha fedha chap chap zaidi ya milioni 7 zilichangwa. Ila huyu Mkurya wa Geita wanamuacha ateseke kwa milioni tatu tu!

Nitumie nafasi hii kuwasihi sana wana CHADEMA. Jalini utu wa mwenzenu. Si vema kumuacha anatesema hivi. Kwa idadi ya wanachama mlionao, hata kila mmoja atachanga senti Hamsini tu mtapata fedha za kutosha. Haya mnayofanya leo Mungu atawahukumu 2020

=======

Habari hii imekanushwa;

=======
Nimesoma Machapio ya baadhi ya watu wanaccm na wanachadema juu ya post yangu ya Facebook ya kuuza kiwanja changu ili niweze kupata matibabu zaidi ya Nyonga ilivunjika mkoani Dodoma Tarehe 03/10/2016.

Nimeona propaganda za maadui wa chadema wakijaribu kuonyesha eti wameumizwa sana na Mimi kupata matatizo na kuanza kuwabeza viongozi wangu wa chama ususani Mwenyekiti wangu Bw Freeman Mbowe kwa kunitelekeza kumbe ni unafiki na ukosefu wa ubinadamu na kutumia siasa kwenye maisha ya watu tena mtu anaumwa kama Mimi huu ushetani kuzidi wa warusifer.

Napenda kuwaambia wapenda mabadiliko wote chama changu cha chadema hakijaniacha Mimi Mhere Mwita, Mwenyekiti wangu Freeman Mbowe Hajanitupa wapuuzeni kwa hizi Propaganda kitoto za madui wa chama chetu.

Nilipopata Ajali tarehe 03/10 mwaka Jana chadema Kanda ya kati ndio walinipeleka Hospitalini Dodoma na kesho yake kuamua kunisafirisha kwenda Mhimbili kwa matibabu zaidi chadema hawakunitupa Bali walinibeba kwa mikono miwili.


Nilipofika Mhimbili nilipokelewa na wanachadema Kamanda Manawa Bukwimba, Dr Kilawa shindo, Malisa GJ, Yericko Nyerere, Wamajiwa Teute, Mashiku Chokala Ben Sanane na Dada yangu Eliza Beth na kunishughulikia mpaka kuhakikisha ninapata huduma ya kwanza na kitanda cha kulala siku hiyo hawakulala.

Chadema hawajaniacha kuanzia mwanzo mpaka Mwisho ninaagwa Mhimbili wanachama na viongozi wa kitaifa walikuja kunijulia hali na kunifariji bila kujali mda wao waliotumia wanachadema walichanga michango yao tena kwa hamsa kubwa chini ya uratibu wa Malisa GJ.

Ukwel ni kwamba mchango wa chadema ndio ulionifanya nitibiwe nipate chakula bila wasi wasi wowote katika Maisha yangu ya Mwezi Mmoja mhimbili asanteni sana chadema kwa niaba familia tunashukuru sana kwa mchango wenu.

Nimechukua hatua hii ya kuuza kiwanja changu baada ya kuona sasa yatosha wanachama wenzangu wamebeba mzigo mzito wa kunipigania mhimbili sasa ni wakati wangu wa kujipigania maana chama changu na wanachama wenzangu wamenipa ushirikano wa kutosha.

Nimejiuliza sana mda wote kukaa kukitegemea chama chetu na wakati chama chetu kinatakiwa kuendesha programme zake hivi chadema inaweza kuwahudumia wanachadema wangapi ambao wako kwenye matatizo na Mimi ni bora kuliko wanachadema wengine ambao hawajulikani na wanafanya kazi ya chama.

Hapana sio jukumu la chadema kunisaidia mimi Bali ni jukumu langu kukisaidia chama changu Kiwanja changu hakina thamani yoyote kukizidi chama changu kwa maana hiyo basi viwanja vipo vingi vinauzwa ila chadema ni moja tu.

Chadema imenifanya kuheshimika, chadema imenifanya kutambulika, chadema imenithaamini sana wanaoleta propaganda nawaambia Mimi nahitaji chadema kuliko yenyewe inavyonihitaji Mimi.

Wanachadema wenzangu asanteni sana kwa kunipigania mwanzo mpaka sasa msikatishwe tamaa na Propaganda za maadui wangu na wachama chetu wanaojifanya kunipenda wakati Mimi ni MTU mzima ninajua wanaonipenda kwa Dhati kwa hiyo waacheni wajichetue tu.

Nilitumia Facebook kwa sababu niliamini kuna wanGeita wako wengi Facebook na ningeweza kukiuza kwa haraka zaidi ili nipate matibabu kumbe wenzetu wameona Matatizo yangu yanaweza kuwanusuru na Gharika na kuifanya kuwa propaganda ya kuwabeba hawana hoja.

Samahani sana Wanachadema wenzangu kwa propaganda hii ya kukichafua chama chetu Mimi nia yangu ilikuwa ni njema kuliko kupiga kelele kuupa mzigo chama Mimi ndio nibebe mzigo huo ili nipone haraka niweze kuendeleza ujenzi wa chama ninatamani sana ninanyanyuke hapa kitandani nikijenge chama chetu ili watanzania wanufaike nacho dah siwezi bora niuze kiwanja changu nitapata kingine.

Ninatambua chama chetu kinamzigo mzito nikibaki kukitegemea chama kila kitu nitarudisha nyuma ujenzi wa chama viwanja vipo nikiuza cha Geita Leo kesho nitanunua Mbezi Beach ila chadema ni moja tu nikiikosa Leo nitajuta maishani mwangu pote maana kimebeba tumaini langu.

Asanteni sana

Ni Mimi Mhere Mwita wa Geita
 
We jamaa una tofauti na shetani,kama wewe si wakike jichunguze tena vizuri!Utadhani mke wa balozi wa nyumba kumi ulivyo na mdomo.Haipendezi mtoto wa kiume kuwa kama wewe,utakuwa mzigo kwa wazazi na ndugu zako.Ya nymba ya jirani yana kuwaashia nini?Au buku saba
 
We jamaa una tofauti na shetani,kama wewe si wakike jichunguze tena vizuri!Utadhani mke wa balozi wa nyumba kumi ulivyo na mdomo.Haipendezi mtoto wa kiume kuwa kama wewe,utakuwa mzigo kwa wazazi na ndugu zako.Ya nymba ya jirani yana kuwaashia nini?Au buku saba
Hapana Mkuu. Hili la Mhere Mwita limeniuma sana. Kama wanachanga fedha kulipa faini ya watukanaji, wanashindwaje kuchanga fedha za matibabu?
 
Na huyo mwita ni kiherehere sana anajufanya anajua na ku kupenda, chama alafu chama hakimpendi
Sasa umekua mzigo kwa baby yake
 
Mhere Mwita ni mtanzania mwenzetu, ni mwanachama na kiongozi wa BAVICHA wilaya ya Geita. Alipata ajali alipokuwa anatimiza majukumu yake ya kichama.

Leo ameandika kwenye ukurasa wake wa facebook kuwa anahitaji kuuza kiwanja chake kilichopo wilaya geita mjini ili aweze kukamilisha matibabu yake.

Mimi ni mwanachama wa CCM na yeye ni mwanachama wa Chadema ila sisi wote ni watanzania na utu, ubinadamu na kusaidiana ndio tabia zetu watanzania.

Tafadhali sana wanajamvi la facebook badala ya kumpigia simu ya kutaka kiwanja chake, bali tumchangie fedha hiyo ya Mil. 3.5 ili akatibiwe na akiwa na afya njema akatumie kiwanja chake kwa ajili ya kuzalishia taifa.

Namba ya kumchangia ni 0742530600 (Mhere Mwita)


LikeShow more reactions
Comment
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom