CHADEMA wamsafisha Shitambala

Matonange

Member
Nov 11, 2010
62
6
Stella Aron na Christina Gauluhanga, jijini

SAKATA la Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Mbeya, Sambwee Shitambatala, kujiuzulu kwa tuhuma za kupokea rushwa ya sh. milioni 600 ili kukipa kukihujumu chama hicho dhidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kiibuke na ushindi, limeingia katika sura mpya baada ya viongozi wa CHADEMA kumwangukia mwenyekiti huyo kwa kumsafisha.

Akizungumza leo asubuhi na gazeti hili kwa njia ya simu, Katibu wa Mkoa wa Mbeya, Eddo Makata, amesema katika uchunguzi uliofanyika umebaini kuwa Shitambala hana harufu ya rushwa wala hakuchukua kitu kidogo kwa ajili ya kuiumiza CHADEMA katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 31, mwaka huu.

Amesema kikao cha Baraza la Mashauriano la Mkoa huo lililokaa Novemba 27, mwaka huu mkoani hapo, kimethibitisha kuwa Shitambala hakuhongwa kiasi hicho cha fedha ambacho baadhi ya wanachama walikuwa wakimtuhumu.

Makata amesema kutokana na uchunguzi huo baraza linatarajia kumpa ofisi Desemba 11, mwaka huu na ameomba radhi kwa usumbufu alioupata kutokana na kashfa hiyo.

“Sisi kama chama mkoani hapa tumekaa kikao ili kujiridhisha kuhusu uvumi huu lakini tumebaini kuwa haukuwa na ukweli na ndiyo maana tumeamua kutoa kauli hii na tutamrejesha katika ofisi yake Desemab 11, mwaka huu,” amesema Makata.

Hivi karibuni Shitambala alitangaza hadharani azma yake ya kujivua wadhifa huo kwa madai kuwa anapisha uchunguzi wa kashfa dhidi yake ya kupokea rushwa kutoka CCM ili kumsaidia mgombea wa chama hicho kushinda Ubunge wa jimbo hilo.

Source: Dar Leo, Wednesday, 01 December 2010
 
Inawezekana wanaCHADEMA waliamini wangeshinda, na ikatokea wengine hawakwenda kupiga kura wakiamini ushindi tayari umepatikana. Uchaguzi ujao wajifunze, wahamasishe watu wakajisajili, wakapige kura na wazilinde.

Kama imethibitika hana kosa, arudi kwenye uongozi kuendeleza chama, waTz wanataka mabadiliko na wako tayari kwa chama kilicho makini kitakachochukuwa nafasi ya CCM. Kwa sasa CHADEMA ndio wenye nafasi ya kuwa chama mbadala, wajenge chama tayari kwa 2014, kwenye chaguzi za serikali za mitaa na 2015 uchaguzi mkuu.
 
Safi shitambala rudi ofisini endelea na kazi ya kukijenga chama,maaana huuu ni mwanzo tu.
 
Stella Aron na Christina Gauluhanga, jijini

SAKATA la Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Mbeya, Sambwee Shitambatala, kujiuzulu kwa tuhuma za kupokea rushwa ya sh. milioni 600 ili kukipa kukihujumu chama hicho dhidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kiibuke na ushindi, limeingia katika sura mpya baada ya viongozi wa CHADEMA kumwangukia mwenyekiti huyo kwa kumsafisha.

Akizungumza leo asubuhi na gazeti hili kwa njia ya simu, Katibu wa Mkoa wa Mbeya, Eddo Makata, amesema katika uchunguzi uliofanyika umebaini kuwa Shitambala hana harufu ya rushwa wala hakuchukua kitu kidogo kwa ajili ya kuiumiza CHADEMA katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 31, mwaka huu.

Amesema kikao cha Baraza la Mashauriano la Mkoa huo lililokaa Novemba 27, mwaka huu mkoani hapo, kimethibitisha kuwa Shitambala hakuhongwa kiasi hicho cha fedha ambacho baadhi ya wanachama walikuwa wakimtuhumu.

Makata amesema kutokana na uchunguzi huo baraza linatarajia kumpa ofisi Desemba 11, mwaka huu na ameomba radhi kwa usumbufu alioupata kutokana na kashfa hiyo.

"Sisi kama chama mkoani hapa tumekaa kikao ili kujiridhisha kuhusu uvumi huu lakini tumebaini kuwa haukuwa na ukweli na ndiyo maana tumeamua kutoa kauli hii na tutamrejesha katika ofisi yake Desemab 11, mwaka huu," amesema Makata.

Hivi karibuni Shitambala alitangaza hadharani azma yake ya kujivua wadhifa huo kwa madai kuwa anapisha uchunguzi wa kashfa dhidi yake ya kupokea rushwa kutoka CCM ili kumsaidia mgombea wa chama hicho kushinda Ubunge wa jimbo hilo.

Source: Dar Leo, Wednesday, 01 December 2010

Mmekamilisha jukumu lenu kwa hiyo mnarudi tena kusubiri kupangiwa mengine, lakini hakuna kisichokuwa na mwisho hata hizi hila zenu zina mwisho wake
 
Safi Shitambala, umeonyesha kuwa wewe ni Kiongozi. Hebu wanaJF niambieni katika zama hizi za UFISADI, ni Kiongozi gani wa ccm ambaye yupo tayari kujivua madaraka yake ili uchunguzi wa tuhuma ufanyike dhidi yake? Niambieni kama yupo! Hosea ametuhumiwa mara ngapi?
 
Mungi habari za Endamarariek??? I had a wonderful time in Endabash and i had to visit Endamarariek too

Back to topic, the real thing is that Shitambala has that kind of leadership traits that we miss in most of those in power; Personal accountability........We need these kind of leadership in Tanzania.

Big up Shitambala and resume for work katika kuleta mageuzi Tanzania
 
binafsi ninapongeza hilo ila nina reservation kwani madai ya kunyimwa viti maalumu aliyoapendix kwangu hayakuwa na maana.pia nina mashaka na gazeti hili kuandika habari ambayo ina tija kwa cdm.
 
Pole sana mdogo wangu Shitambala, lakini umeonesha mfano kiongozi anavyostahili kuwa.

Namfahamu Shitambala, ningeshangaa sana kama tuhuma hizo zingeonekana ni za kweli. Watanzania wa Mbeya, mpeni ushirikiano wa kutosha Shitambala. Huyu ni kati ya watanzania wachache waliojitolea kwa uwezo wao wote kuijenga CHADEMA na kuhakikisha mabadiliko ya kweli yanapatikana kwa watanzania wote.
 
Hongera Shitambala wana Mbeya popote tulipo hata huku Arusha ,tunakuaminia ulikuwa uamuzi mzuri sana wa uwajibikaji wa hali ya juu ni viongozi wachache wanaoweza kupisha uchunguzi hekoooooooooooo bwana mdogo shikilia usukani sasa imarisha chama chako
 
Hivi karibuni Shitambala alitangaza hadharani azma yake ya kujivua wadhifa huo kwa madai kuwa anapisha uchunguzi wa kashfa dhidi yake ya kupokea rushwa kutoka CCM ili kumsaidia mgombea wa chama hicho kushinda Ubunge wa jimbo hilo.

Hapo kwenye RED panaonyesha kuwa wewe ni kiongozi bora! I admire u 4 that! Itabidi uwape tuition viongozi wengi hapa Africa.
 
huu ndio mfano wa demokrasia kwamba anayetuhumiwa anakaa pembeni, uchunguzi unafanyika, ripoti inakuwa wazi na kama mtu amekosewa anaombwa radhi. chadema endeleeni kutuonesha mfano wa utawala wa kidemokrasia.
 
Safi Shitambala, umeonyesha kuwa wewe ni Kiongozi. Hebu wanaJF niambieni katika zama hizi za UFISADI, ni Kiongozi gani wa ccm ambaye yupo tayari kujivua madaraka yake ili uchunguzi wa tuhuma ufanyike dhidi yake? Niambieni kama yupo! Hosea ametuhumiwa mara ngapi?
Kumbukumbu zangu zinaniambia kwa CCM hakuna kitu kama cha kiongozi kujiuzulu kupisha uchunguzi. Refer the late Kighoma Malima na Prof. Mbilinyi. Hawa walikuwa Mawaziri wa Fedha kwa nyakati tofauti na katika vipindi vyao vya uongozi yalitokea mambo yaliyohitaji wao kujiuzuru. ilikuwa kazi kubwa sana mpaka jumuiya ya kimataifa ilipoingilia kati kwa kutishia kuzuia misaada kwa TZ ndipo walipotolewa / jiuzulu.
 
naona hakuna anayechunguza mantiki ya shitambala kulalamika kuwa amenyimwa viti maalum? Aliomba chama kimpe majibu,pia haijajulikana kama shitambala mwenyewe kakubali kurudi kwani alikuwa katoa a controversial statement kuhusu viti maalumu na nasiki alikuwa akilalamika by implication kwani mke wake ndiye alikuwa likely ku win
 
kunja ngumi, kunja ngumi, kunja ngumi, kunja ngumi
PEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEPLE'S

Umma: Poooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooowers
 
Walichofanya CHADEMA ni jambo sahihi kabisa na linatakiwa liungwe mkono na wazalendo wa kweli. Huu ni mfano kuona ni jinsi gani CHADEMA ilivyo serious katika kushughulikia tuhuma zinazo wakabili viongozi wake. Hata wakichukua nchi mwendo ni huo huo, tuhuma zozote zinafanyiwa kazi ndani ya muda mfupi na maamuzi sahihi yanatolewa watu wanasonga mbele!

Kitendo cha Ndugu Shitambala kukubali bila malumbano kukaa pembeni wala bila kukimbia chama inaonyesha ni jinsi gani alivyo Kiongozi BORA asiyesukumwa na uroho wa madaraka. NDUGU SHITAMBALA amekomaa kisiasa ni kiongozi wa ukweli, wanambeya mpeni ushirikiano ili aendeleze yale yote aliyo yapigania, na yeye asiwe na kinyongo bali afanye kazi kwa moyo mmoja ili ngome ya CHADEMA Mbeya isiyumbe.

Big up Ndugu Shitambala!
 
Hebu wanaJF niambieni katika zama hizi za UFISADI, ni Kiongozi gani wa ccm ambaye yupo tayari kujivua madaraka yake ili uchunguzi wa tuhuma ufanyike dhidi yake?

Ati nini?
Thubutu!
 
kimsingi angechunguzwa na takukuru na si chadema wenyewe; lakini bado ironical kwani takukuru hawawezi kuichunguza ccm na kuichukulia hatua endapo watabaini kama ni kweli ccm walitoa rushwa hiyo. hayo ni mambo ya siasa tu na huyo jamaa alijua kabisa uchunguzi usingefanikiwa kumtia hatiani.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom