Matonange
Member
- Nov 11, 2010
- 62
- 6
Stella Aron na Christina Gauluhanga, jijini
SAKATA la Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Mbeya, Sambwee Shitambatala, kujiuzulu kwa tuhuma za kupokea rushwa ya sh. milioni 600 ili kukipa kukihujumu chama hicho dhidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kiibuke na ushindi, limeingia katika sura mpya baada ya viongozi wa CHADEMA kumwangukia mwenyekiti huyo kwa kumsafisha.
Akizungumza leo asubuhi na gazeti hili kwa njia ya simu, Katibu wa Mkoa wa Mbeya, Eddo Makata, amesema katika uchunguzi uliofanyika umebaini kuwa Shitambala hana harufu ya rushwa wala hakuchukua kitu kidogo kwa ajili ya kuiumiza CHADEMA katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 31, mwaka huu.
Amesema kikao cha Baraza la Mashauriano la Mkoa huo lililokaa Novemba 27, mwaka huu mkoani hapo, kimethibitisha kuwa Shitambala hakuhongwa kiasi hicho cha fedha ambacho baadhi ya wanachama walikuwa wakimtuhumu.
Makata amesema kutokana na uchunguzi huo baraza linatarajia kumpa ofisi Desemba 11, mwaka huu na ameomba radhi kwa usumbufu alioupata kutokana na kashfa hiyo.
Sisi kama chama mkoani hapa tumekaa kikao ili kujiridhisha kuhusu uvumi huu lakini tumebaini kuwa haukuwa na ukweli na ndiyo maana tumeamua kutoa kauli hii na tutamrejesha katika ofisi yake Desemab 11, mwaka huu, amesema Makata.
Hivi karibuni Shitambala alitangaza hadharani azma yake ya kujivua wadhifa huo kwa madai kuwa anapisha uchunguzi wa kashfa dhidi yake ya kupokea rushwa kutoka CCM ili kumsaidia mgombea wa chama hicho kushinda Ubunge wa jimbo hilo.
Source: Dar Leo, Wednesday, 01 December 2010