CHADEMA wamruhusu Zitto kufanya apendacho

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Jul 5, 2007
5,185
58
Ingawa taarifa ninazopata zinaonyesha kuwa kinachoendelea ndani ya CHADEMA ni mjadala mkali na wala sio mgogoro kama magazeti ya Mwizi na mkoloni Rostam Aziz yanavyoripoti nyumbani, bado kuna sababu ya kusisitiza uhuru wa maoni ndani ya CHADEMA.

Mkutano wa kesho ambao kutokana na report ya Mnyika utaongelea mambo mengi tu na sio suala la zitto peke yake, ni vizuri ikawa wazi kuwa CHADEMA kama chama inabidi wamruhusu Zitto kufanya kile yeye anachojisikia kuwa ni kizuri.

Kama Zitto ameamua kuingia kwenye hiyo tume/kamati/usanii/sijui nini ya Raisi, basi ni vyema akapewa nafasi na chama kufanya hilo apendalo.

Chama ni zaidi ya mtu mmoja, na inabidi mambo makubwa kama haya yakaendelea kupewa demokrasia zaidi na watu wengi zaidi wakapata muda wa kujadili ingawa mwisho wa siku inabidi zitto afanye kile anachoona ni chema maana huu ndio uhuru ninaoutaka kuwepo Tz kwa vyama vyote vya siasa.

Zitto, fanya kile upendacho, na taifa linakuombea uendelee kuwatetetea wale ambao wametengwa na kuonewa. CHADEMA - huu ni wakati wa nyie kuonyesha kuwa mtaendeleza huu uhuru wa kuruhusu debate katika mambo muhimu ya taifa.

Asante.
 
Jambo la mhimu zaidi kwa CHADEMA wakati huu sio kumwongelea Kabwe na Kamati; 2007 hii ni kuweka mikakati imara ya kuongeza wabunge 2010. Wajizatiti kuyatumia matukio haya ya 'Kamati' kuwaelezea wananchi mapungufu yaliyopo katika uwakilishi wa wananchi bungeni.
 
Itakuwa ni makosa makubwa kwa CHADEMA kutomruhusu Zitto kushiriki katika kamati ya madini iliyoundwa na Muungwana. Kwa sababu umaarufu wa Zitto mpaka kuteuliwa na Muungwana kwenye kamati hiyo unaweza kuleta motivation kubwa kwa chama chao kwamba wanayoongea viongozi wa chama hicho akiwamo Zitto yanasikilizwa mpaka Ikulu. Pia Watanzania ambao walikuwa hawakipi chama hicho umuhimu wowote, wataanza kukiangalia mara mbili mbli na hatimaye inawezekana kikaongeza idadi ya wanachama kupitia mgongo wa Zitto. Hata muasisi wa chama hicho Edwin Mtei ameshasema kwamba itakuwa ni kosa kubwa kwa Zitto kutoshiriki kwenye kamati hiyo.
 
kwa nini chadema wamfanye zitto ajisikie kama he is unwanted ndani ya chama kwa kumwabia afanye apendacho ?? kama kweli wamesema hivi, kwa mtazamo wangu nadhani sio dalili nzuri maana wanamkatisha tamaa zitto, sasa sijui huko mbeleni kutakuwaje ?

hizi habari kama ni za kweli basi zinaweza zikawa za furaha na huzuni kwa wengine, maana zitto akiwa huko chadema akiwa backed up na wanachama wenzake na hoja zake, kumetokea mchakato kisiasa hadi mambo yanakuwa interesting, na hapo democrasia ilionekana imeshamiri tanzania, lakini kama huu moto utazimwa basi kutarudi kule kule kuboa !

chadema badirisheni uamuzi wenu !
 
1. I am not really impressed by Zitto, desoite the valuable expose, he still sounds like a desperately populist Mremaist.

2.Nevertheless CHADEMA should support him as other members suggested.Kama mnapiga kelele kuhusu ufisadi kila siku, leo Kikwete anawapa chance kwenye kamati kufichua ufisadi halafu mnakataa mnaonekana wajinga na mnababaisha.Ndiyo mambo yanayomfanya Musharraf apete mpaka kesho Pakistan, kwa sababu wapinzani ingawa walikuwa na nguvu ya kumdondosha, wamegomea uchaguzi.

3.Hapa tatizo letu la kila siku katika siasa za Afrika linajitokeza tena.Inaonekana hatuna siasa za kufuata policy na manifesto za vyama bali tunafuata personality cults.Inaonekana kuna watu ndani ya CHADEMA badala ya kufurahia ushindi wa Zitto kama ushindi wa CHADEMA na sera zake, wanaona kuwa huu ni ushindi wa Zitto na anawashinda umaarufu.Sad indeed!
 
Asante Bubu kwa kuweka hili wazi.

Ikumbukwe pia kuwa hata kama Mtei amesema kuwa ni vyema zitto aingie, bado debate ya nguvu lazima ifanyike ndani ya CHADEMA.

So far kinachoendelea ni kitu kizuri sana maana miaka ile ya ndio mzee imekwisha. Debate kubwa lazima ifanyike na mawazo yote yafanyiwe kazi. Hata hivyo, mwishoni wa siku, inabidi pia maoni na chaguzi binafsi ziheshimiwe.

Mimi napinga hii kamati/tume/usanii/sijui jina lake. Lakini pia siwezi na sitaki kumuamulia zitto cha kufanya. inabidi CHADEMA pia baada ya debate hii wampe Zitto nafasi ya kufanya kile apendacho maana hiyo ndio demokrasia.

Mimi sioni mgawanyiko bali demokrasia katika vitendo.
 
It sound kama ni mambo ya ndani ya Chadema, kwenye taifa sidahni kama yanatuhusu, naona tuwaachie Chadema waamue mambo yao ya ndani kwa mujibu wa katiba yao,

Isipokuwa tu, wakifikia uamuzi wa kumzuia Zitto, kwenye kamati basi hapo ndipo tutapiga filimbi, so far ni internal affairs za Chadema, tunawatakia mafanikio mema na mikutano yao ya ndani ya chama.

Na ndio hasa maana ya sera za kidemokrasia za nchi yetu, yaani wananchi wanaruhusiwa kujadili mustakabali wao katika vyama vyao vya siasa, ndani ya taifa bila ya kuingiliwa na usalama, wala polisi kama huko Pakistan, ambako majuzi tumesikia kiongozi wa upinzani Mama Bhutto akiwekwa under house arrest, kwa kujaribu ku-organize siasa za upinzani ambazo hapa kina Chadema wanaruhusiwa bila matatizo,

Mungu Aibariki Tu Bongo Yetu, pamoja na matatizo yetu lakini angalau wakiitwa wenye demokrasia tutaenda tunachechemea, maana Pakistani hawawezi hata kujaribu kuitika, licha ya kujitokeza!

Wakati mwingine ni vyema kushukuru kidogo ulichonacho, kuliko kulilia makubwa tu in the process hata vidogo vizuri ulivyonavyo unashindwa kuviona, ambavyo huko Pakistani hawana kabisaaa!
 
1. I am not really impressed by Zitto, desoite the valuable expose, he still sounds like a desperately populist Mremaist.

2.Nevertheless CHADEMA should support him as other members suggested.Kama mnapiga kelele kuhusu ufisadi kila siku, leo Kikwete anawapa chance kwenye kamati kufichua ufisadi halafu mnakataa mnaonekana wajinga na mnababaisha.Ndiyo mambo yanayomfanya Musharraf apete mpaka kesho Pakistan, kwa sababu wapinzani ingawa walikuwa na nguvu ya kumdondosha, wamegomea uchaguzi.

3.Hapa tatizo letu la kila siku katika siasa za Afrika linajitokeza tena.Inaonekana hatuna siasa za kufuata policy na manifesto za vyama bali tunafuata personality cults.Inaonekana kuna watu ndani ya CHADEMA badala ya kufurahia ushindi wa Zitto kama ushindi wa CHADEMA na sera zake, wanaona kuwa huu ni ushindi wa Zitto na anawashinda umaarufu.Sad indeed!

Well, why do you think so? If you know of something just let us know so that we dont make wrong decisions!
 
he still sounds like a desperately populist Mremaist.

Lakini at least aliyoyaa-accomplish kwenye taifa letu hakuna anayemfikia so far toka tupate uhuru, I sill belive in him.
 
Zito kwa umri wake na mambo ambayo ameya-accomplish ni wachache wataweza kulingana au kusogelea. Tuache wivu usio na msingi na tuangalie Taifa litafaidika na nini ambacho atachangia.
 
1. I am not really impressed by Zitto, desoite the valuable expose, he still sounds like a desperately populist Mremaist.

2.Nevertheless CHADEMA should support him as other members suggested.Kama mnapiga kelele kuhusu ufisadi kila siku, leo Kikwete anawapa chance kwenye kamati kufichua ufisadi halafu mnakataa mnaonekana wajinga na mnababaisha.Ndiyo mambo yanayomfanya Musharraf apete mpaka kesho Pakistan, kwa sababu wapinzani ingawa walikuwa na nguvu ya kumdondosha, wamegomea uchaguzi.

3.Hapa tatizo letu la kila siku katika siasa za Afrika linajitokeza tena.Inaonekana hatuna siasa za kufuata policy na manifesto za vyama bali tunafuata personality cults.Inaonekana kuna watu ndani ya CHADEMA badala ya kufurahia ushindi wa Zitto kama ushindi wa CHADEMA na sera zake, wanaona kuwa huu ni ushindi wa Zitto na anawashinda umaarufu.Sad indeed!

Well, I am for this kind of populist anytime anywhere. Populist mwenye uwezo wa kujenga hoja kama ile ya 'Mswada Binafsi' aliyoitoa bungeni - tunawahitaji 'populists' wengi wa aina hiyo, hasa wakati huu wa ufisadi mwingi.
 
Mimi nahisi kuna watu wametumwa na hata aibu hawana, wewe mtu amepewa shughuli kwenye kamati na ataweza ku-influence pale halafu bado watu wengine wanataka asiende kule? Embu nyie kina sijui Wenge acheni ujinga kabisa, mwacheni kijana akafanye vitu vyake na akiona kuna mizengwe basi anaweza kung'atuka katika kamati.

Zitto mwanangu nenda kawachemshe bongo kule hamna noma wala nini sisi wanyonge tuko nyuma yako.
 
Haya ndiyo mambo tusiyoyataka, akiamua kuendelea kuwemo, awemo hadi mwisho. Mambo ya mbele ya safari kujitoa hamna agangamale mumo kwa mumo. Anayo chance ya kujitoa sasa; na kama anataka kuendelea kuwemo basi awemo hadi mwisho! Na kama ataona kuna haja ya kuandika dissenting report basi atafanya hivyo..
 
Kujitoa sasa bila kujua kulikoni kwenye kamati haina dili na hailipi.

Cha maana ni kuingia kwenye kamati na kufanya kazi, kama akiona kamati inaletewa mizengwe na kuwa-influenced kisiasa bila hoja nzito na kuona kwamba kamati haina maslahi kwa wananchi na nchi kwa ujumla, basi anaweza kuamua kujitoa na sababu ya kufanya hivyo itakuwepo, lakini kwa sasa hakuna sababu ya kujitoa hata kidogo, tumuache kijana akafanye vitu roho yake inapenda yaani kutetea maslahi ya hii nchi.
 
kwa nini chadema wamfanye zitto ajisikie kama he is unwanted ndani ya chama kwa kumwabia afanye apendacho ?? kama kweli wamesema hivi, kwa mtazamo wangu nadhani sio dalili nzuri maana wanamkatisha tamaa zitto, sasa sijui huko mbeleni kutakuwaje ?

hizi habari kama ni za kweli basi zinaweza zikawa za furaha na huzuni kwa wengine, maana zitto akiwa huko chadema akiwa backed up na wanachama wenzake na hoja zake, kumetokea mchakato kisiasa hadi mambo yanakuwa interesting, na hapo democrasia ilionekana imeshamiri tanzania, lakini kama huu moto utazimwa basi kutarudi kule kule kuboa !

chadema badirisheni uamuzi wenu !

Kada,

Mkutano wa CHADEMA haujafanyika bado, kwahiyo hakuna maamuzi yoyote ambayo yameisha tolewa. Ukisoma kichwa cha habari cha hii mada halafu ukiisoma mada yenyewe utaona kuwa haya ni maoni binafsi ya Mwafrika Wa Kike. Anashauri kuwa, "uamuzi wa mkutano umruhusu zito afanye apendacho."

Umepandwa na jazba mpaka umeshindwa kumuelewa MwK, ukahitimisha kuwa uamuzi umeisha tolewa tayari. HAPANA, kikao bado hakijafanyika na uamuzi haujatolewa bado, TAMAT.
 
Chadema wakimwacha Zitto kwenye kamati wamejimaliza na wamemmaliza Zitto. Kadhalika wakisusia wamejimaliza na wammemaliza Zitto. Therefore, this is lose-lose situation itakayowalazimisha Chadema wamruhusu Zitto kuendelea kwenye kamati.

Utabiri wangu: Zitto ataruhusiwa na Chadema kushiriki katika kamati. Mapema baada ya kamati kuanza kazi Chadema watalalamikia nyenendo za kamati (creating another issue)na hapo ndipo watamtoa Zitto kwenye kamati bila kumpunguzia umaarufu na bila kuondoa credibility ya Chadema.

Siasa ni kama mchezo wa bao, unapanga mbinu za kula kwa kutegeshea mlo.
 
Kada,

Mkutano wa CHADEMA haujafanyika bado, kwahiyo hakuna maamuzi yoyote ambayo yameisha tolewa. Ukisoma kichwa cha habari cha hii mada halafu ukiisoma mada yenyewe utaona kuwa haya ni maoni binafsi ya Mwafrika Wa Kike. Anashauri kuwa, "uamuzi wa mkutano umruhusu zito afanye apendacho."

Umepandwa na jazba mpaka umeshindwa kumuelewa MwK, ukahitimisha kuwa uamuzi umeisha tolewa tayari. HAPANA, kikao bado hakijafanyika na uamuzi haujatolewa bado, TAMAT.

ndo maana sehemu nyingi nikarudia kusema kama hizi habari ni za kweli, kupandwa kwangu kwa jazba kuko wapi ? au unataka uwe kwenye spotlight kwa kumshambulia kada ?? maana mtu akitaka kitu fulani tu hapa basi wao ni kumshambulia kada, huwezi kutoa point bila ya kunishambulia, ??

kichwa cha thread kilinichanganya ndo maana nikatoa maoni niliyotoa, ha nakuhakikishia kama ulisoma vizuri BASI HAKUNA HATA CHEMBE YA JAZBA NILIYOTOA, nikiwa na jazba nitatoa hadi itaeleweka kwamba hiyo ni jazba and i know it will cost me speaking in jazba, kwa hiyo kama ningeongea kwa jazba mzee TRUST ME the whole forum ingenisikia, so hayo ni maneno yako binafsi and i take that !
 
CHADEMA wamruhusu ni tungo tata, inaweza kumaanisha wameshamruhusu tayari au inaweza kumaanisha ni ombi kwamba wamruhusu. Eti sister, ulikuwa unamaanisha nini?

Asha
 
Huko nyuma ktk mada nyinginezo nimeuliza maswali mawili na yote yamekosa majibu toka pande zote mbili zinzobishana juu ya uchaguzi wa Zitto.
Kinachonishangaza mimi ni pale tunapoweka ubishi ktk swala ambalo hakuna kati yetu analifahamu vizuri zaidi ya kuwa Zitto kachaguliwa na Muungwana kuunda kamati ya madini. Yaani hilo neno KAMATI YA MADINI ndio imezua yote haya pasi kuelewa hiyo kamati ina majukumu gani mbele.
Kisha ningependa kuongezea swali moja hapa, hivi kweli kuna sheria inayompa ruksa mwananchi bila kujali chama chake kukataa kazi aliyoteuliwa na rais wake ktk kulihudumia taifa bila kuwa na sababu maalum. Maanake hapa mjomba ukiteuliwa kuunda Jury (wazee wa baraza) ktk mahakama, huwezi wala huruhusiwi kukataa bila sababu ya kimsingi tena basi sio kazi yako kujikata ila jukumu la Mahakama, Prosecutor ama Defence kutoa Uamuzi huo...Hata mwajiri wako haruhusiwi kabisa kukuzuia kushiriki.
Kuna mshikaji wangu alipighwa bonge la fine kwa kutohudhulia mchujo wa hii jury na barua kali ilotaka kufahamu sababu zilizomfanya asihudhulie. Huo ni mfano tu nimejaribu kuutazama kwa sura ya uchaguzi huu wa Zitto ktk kamati hii ya madini kwani sidhani kama sababu za chama Chadema zinaweza kuwa na Uzito kufunika madaraka aliyokuwa nayo Muungwana.

Can U say - NO, thank U Mr. Presidaa - I can't serve my country.
 
Hivi Zitto atakuwa anafanya kazi peke yake kwenye hiyo kamati? Yaani yatakayofanywa na kamati yatakuwa yamefanywa na Zitto? Je huyu Zitto anaweza kulazimisha msimamo wake uwe ndio msimamo wa kamati? Au conclusions za Zitto peke yake ni lazima zichukuliwe na kamati kuwa ndizo conclusions za kamati nzima? Mbona sasa madai mengi yanayosemwa hapa ni kama vile ati Zitto ndiye anayekwenda kuendesha hiyo Kamati? Kwa uelewa wangu Zitto ni mjumbe katika hiyo kamati kama wengine, na atachangia kwa uwezo wake, lakini mwisho wa zoezi hilo mapendekezo yatakuwa ya Kamati na si ya Zitto. Sasa why all this fuss about Zitto? Au kuna anayedhani kamati itakwenda kuchukua mawazo ya Zitto kama yalivyo na bila kuyajadili? Sasa kama ikiwa hivyo wengine kwenye kamati hiyo watafanya kazi gani? Huu mjadala kwamba Zitto aende au asiende kwenye hiyo Kamati ni immaterial and baseless. Ameteuliwa na Rais akashiriki kwenye Kamati kwa faida ya taifa, na hata kama kwa sehemu itakuwa ni kwa faida yake pia, kuna ubaya gani? Mcheza kwao hutuzwa. Anastahili, au sivyo jamani?
 
Back
Top Bottom