CHADEMA wampongeza Rais Magufuli kwa kutoifunga nchi wakati wa Corona

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,607
141,429

Chadema mkoa wa Tabora wamemshukuru na kumpongeza Rais Magufuli kwa kutoifunga nchi wakati wa Corona.

Akiongea kwa niaba ya uongozi wa mkoa wa Chadema, mbunge wa viti maalumu mh Mwaisonga amesema wao kama chama wanamshukuru Mungu kwa maono aliyompa Rais Magufuli na hatimaye ametuvusha salama.

Mh Mwajuma amesisitiza kuwa Chadema itaendelea kumpa ushirikiano Rais Magufuli kwa mambo yote yenye manufaa kwa taifa letu.

Source: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Nimefurahishwa na kitendo cha CHADEMA kumpongeza Rais Magufuli kwa kutokufunga mipaka ya nchi katika kipindi hiki kigumu cha COVID19.

Hakika huo ndiyo uzalendo

Chanzo: ITV
 
Toka lini mbunge wa viti maalum akaawa msemaji wa chama ngazi ya mkoa!

Hii itakuwa ni propaganda kuelekea uchaguzi maana wabunge viti maalumu inaonekana wengi wameshanunuliwa na wanatumika kumutafutia Magufuli uhalali ambao hana.
 
Mbona Sugu huwa anaongelea mambo ya Chadema mkoa wa Mbeya!
 
Toka lini mbunge wa viti maalum akaawa msemaji wa chama ngazi ya mkoa!

Hii itakuwa ni propaganda kuelekea uchaguzi maana wabunge viti maalumu inaonekana wengi wameshanunuliwa na wanatumika kumutafutia Magufuli uhalali ambao hana.
Kwani chadema ina msemaji maalum pale kila mtu ni msemaji kwa wakati wake iwe lema, h. Mdee, bulaya sugu nk yoyote tu yule alie karibu na Mbowe ni msemaji
 
Back
Top Bottom