CHADEMA wampokea Lijualikali kutoka gereza la Ukonga, atoa ya moyoni

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,189
2,970
Siku moja baada ya Mbunge wa Kilombero (Chadema) Peter Lijualikali kuachiwa huru na mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam, ametoa ya moyoni na kusema kuwa alichofanyiwa ni uonevu.

Ameyasema hayo leo baada ya Waziri Mkuu Mstaafu, na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Frederick Sumaye, kukamilisha taratibu za kumtoa gerezani.

Lijualikali amefutiwa mashtaka yake jana na mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam baada ya kukaa jela kwa zaidi ya siku 70 akituhumiwa kufanya vurugu katika uchaguzi wa mwaka 2015. Katika hukumu hiyo, Lijualikali alihukumiwa bila kupewa ya faini.

Chanzo: Mwananchi

Rejea kuhusu hukumu yake kutenguliwa =>Mahakama Kuu yatengua Hukumu ya Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali

Jamani wapenda haki na maendeleo wote , kwanini tuschange buku buku walau apitie pale
magereza recreation akapige supu mtori na chapati kabla hajasepa...?? 9ikizingatiwa hapo maeneo ni pua na mdomo tu NA UKONGA MAXIMUM PRISON.
kama vipi twendeni nae akazimue chai kwenye baa za hapo magereza ukonga au tumpeleke java pande za banana
akapige vyombo kuzimua mwili.
 
badala ya kwenda kumpokea waziri mkuu wa Ethiopia wanaenda kumpokea mhalifu....polisi kamata hao wahuni mara moja
Hii nchi ina Vituko kiukweli
huyo kwani kwa Nchi kama Tanzania!!
Ujinga ujinga ndio unawapotezea muda watanzania kuliko vitu vya msingi
kesho anakuja mtu kulalamika mfukoni hakuna kitu!!
hakuna kitu umekalia ujinga utegemee kupata kitu!!
Nchi inahitaji kuombewa hii
 
Mmeruhusiwa kukusanyika? Maana....
Acha mikwara bana ikizingatiwa wewe ni mwanasheria unayejua sheria za mikusanyiko, lakini leo
wajitoa ufahamu kabisa kisa wanakusanyika kumlaki mwana UFIPA.
kwanza wao wamevunja sheria gani , wakivunja sheria hapo sawa ila kama hakuna kuvunja sheria hakuna kosa hapo
na kama huamini , na hata hap wazee wa kutuliza ghasia kambi yao ya FFU iliyopo Ukonga ni mwendo wa dk 2 tu mpaka hapo Magereza, ila kwa kuwa wanaelewa hakuna kosa walilofanya wala hawatathubutu kuwabughudhi zaid ya kuwapa ulinzi mujarabu.
 
Wamecheza kama Pele kuingia ndani. Maana...
 
Back
Top Bottom