CHADEMA wamlima Rais Kikwete Barua juu ya mauwaji katika mikutano yao

Hawa CHADEMA naona wanataka adhabu kutoka kwa Rais, vifo wasababishe wao halafu wanaomba hatua zichukuliwe? kaz kweli kweli.

Nadhania Rais akiamua na sheria zikapitiwa vizuri, ni wazi CDM wataingia matatani, ngoja tusubiri reaction ya Rais.
kweli wewe m.atako kwa fikra zako rais wa nchi hii atachukuwa hatua juu ya mambo hayo?kwa ufinyu wa fikra zako jaribu tena kufikiria sawa?
 
mtu wanayemwamsha mbona amejifunika blaketi nzito usingizi njwiiiiiiiii! hana hata fahamu kama kuna kitu kama hicho kinaendelea
 
Hakika imefika mwisho, watawala hawa wasio na fikra za maendeleo, wanafikiria kuua raia ili kuwatisha. Hakuna atakayetishika na tunataka MABADILIKO. Mauaji ya Arusha, Songea, Morogoro, Iringa na hatihati ya kutaka kutoa maisha ya Ulimboka ni chachu ya mabadiliko. Hakuna kulala mpaka kieleweke, nchi hii lazima iokolewe kutoka kwenye mikono ya mafisadi.
 
Changa la macho hilo ili kujikosha na kashfa ya kutoa kafara watoto wa watu. Kuna ulazima gani wa rais kutoa kauli wakati ambapo hatua zimeshachukuliwa? Mbayuwayu in action.

kwa hiyo CCM ndo mashetani wanaopokea au kula damu za kafara wa CDM??? Kwa utetezi huu unakimalizia kiCCM choo la shimo.
 
Sijaona tatizo kwa nini Rais asipewe barua kama amekaa kimya,kwa chama makini nilazima kiweke rekodi zake sawa juu ya matukio yanayogusa masilahi ya wananchi,nadhani pia kwakuwa Rais wetu ni muungwana atawajibu Chadema,na sisi tutajua kwanini Rais amekuwa kimya.
 
Wwe mamasara,kwasasa hivi u Ccm katika mambo ya kisheria uutoe, haiingii hakililni kama adhabu ya mikutano au kuandamana ni kutoana roho, unapotoka. Kama chadema walivunja sheria halali za nchi viongozi wake wapo ilibidi wakamatwe,kma hawjakamatwa WHY, . KAMA TUMEKUBALI MFUMO WA VYAMA VINGI, MAANDAMANO NA MIKUTANO NDIO DEMOKRASIA YENYEWE. UFISADI UMETAMALAKI,UCHUMI MBOVU,AJIRA,UMEME, MAJI HAKUNA, WANANCHI WANAONYESHA UJASIRI WA KUWAKATAA MNAWAUA KUWATISHA. THEN MNALETA UTETEZI NA PROPAGANDA ZENU ZISIZO NA MASHIKO. HIKI KIZAZI CHA DOT.COM SIO S.L.B. HATUDANGANYIKI. HAYA BUBUBU JE?. SHAME ON YOU!!!!.
 
Hawa CHADEMA naona wanataka adhabu kutoka kwa Rais, vifo wasababishe wao halafu wanaomba hatua zichukuliwe? kaz kweli kweli.

Nadhania Rais akiamua na sheria zikapitiwa vizuri, ni wazi CDM wataingia matatani, ngoja tusubiri reaction ya Rais.

we acha kuwasitua wajikoki wenyewe.wanadhani wako kwenye nafasi ya kumuamuru mr presdent.
Ombi lao halitatekelezwa na wakiitisha maandamano huo ndo utakua mwisho wa chadema kama chama cha siasa.
 
Wewe kama upo tayari kufa kwa ajiri ya mabadiliko kufa peke yako, sisi watanzania tunataka amani iendelee kuliko hata hayo mabadiliko yako.

Tuna watoto wachanga, tuna mama zetu wasioweza kukimbia, tuna bibi zetu halafu unaongea pumba kwamba hata wakituua sawa tena kwa kutaka wenyewe. Acheni kupelekwa pelekwa.

"wajinga ndio waliwao".
 
Mkuu nipo na simu ningekuwa na pc ningekugongea boonge la LIKE. Yaani hapa sawa sawa na mwizi kuuawa wakati anatuhumiwa. Hata kama CDM ndio wanasababishi polisi wanapata wapi haki ya kuua raia?
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wamemwandikia barua rasmi rais Jakaya Kikwete juu ya mwenendo wake wa kukaa kimya na kutochukua hatua yoyote kwa baadhi ya matukio yanayoonuesha kupangwa na wahusika kutowajibika hivyo wanamtaka rais awawajibishe.

Baadhi ya hao wanaotakiwa kuwajibishwa ni kamanda wa polisi wa Iringa, Morogoro, Arusha, Tabora na waziri wa mambo ya Ndani bwana Nchimbi


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemwandikia barua Rais kwa lengo la kumtaka achukue hatua, kwa mujibu wa mamlaka yake na kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuhusu mauaji ya kisiasa.


Katika barua hiyo ya tarehe 10 Septemba 2012 iliyoandikwa na Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe (Mb) pamoja na hatua nyingine CHADEMA imetaka Rais achukue hatua ya kuwafukuza kazi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Ndugu Emmanuel Nchimbi, IGP Said Mwema, Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja, RPC wa Mkoa wa Morogoro Faustine Shigolile na RPC wa Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda kwa kutowajibika kufuatia mauaji yaliyotokea mkoani Morogoro na Iringa.


Aidha, CHADEMA kimetaka Rais aunde tume ya Kijaji/ Kimahakama ya uchunguzi wa vifo vilivyotokea katika mikusanyiko, mikutano, maandamano au mazingira ya kisiasa yaliyohusisha CHADEMA. Vifo hivi ni vile vilivyotokea Arusha (05/01/2011), Igunga (Novemba 2011), Arumeru Mashariki (Aprili 2012), Iramba (Julai 14, 2012), Morogoro (27/08/2012) na Iringa (02/09/2012).


Wakati CHADEMA kikisubiria hatua za Rais pamoja na majibu ya barua hiyo, CHADEMA kinawaagiza viongozi na wanachama wake kutokutoa ushirikiano kwa kamati iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Ndugu Nchimbi pamoja na timu zilizoundwa na Jeshi la Polisi kuchunguza mauaji yaliyofanywa na askari katika mikoa ya Iringa na Morogoro.


Itakumbukwa kuwa katika maandamano yaliyoitishwa na CHADEMA tarehe 05/01/2011, Jijini Arusha, watu watatu walipoteza maisha baada ya Jeshi la Polisi kutumia nguvu na risasi za moto kutawanya waandamanaji.


Katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga pamoja na matukio mengine yaliyojitokeza na yaliyohusisha vurugu kinyume cha Sheria, Ndugu Mbwana Masoud mwanachama wa CHADEMA alitekwa, kuteswa na kunyongwa katika mazingira ya kutatanisha. Mpaka sasa hakuna hatua stahiki zilizochukuliwa kufanya uchunguzi kuhusu kifo hicho.


Mara baada ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki, kiongozi wa Kata wa CHADEMA Ndugu Msafiri Mbwambo alichinjwa na chanzo chake kudaiwa kusababishwa na masuala ya kisiasa.


Hivi karibuni yalitokea mauaji katika Kijiji cha Ndago, Wilaya ya Iramba Mkoani Singida ambapo kikundi cha watu kilivamia na kushambulia mkutano wa CHADEMA kwa mawe, huku Polisi wakiwepo bila kuchukua hatua. Baada ya mkutano kumalizika na viongozi wa CHADEMA kuondoka eneo la mkutano kijana mmoja anayedaiwa kuwa kiongozi wa Kata wa UVCCM alikutwa amepoteza maisha katika kijiji hicho, jirani na eneo ulipofanyika mkutano wa hadhara.


Hivi karibuni tena katika maandamano ya mapokezi ya viongozi wa CHADEMA Mkoani Morogoro Polisi walimshambulia Ndugu Ally Zona na kupoteza maisha, na baadae Polisi wakatoa taarifa kuwa aligongwa na kitu kizito.


Mkoani Iringa wakati wa kufungua matawi ya Chama kwenye kata ya Nyololo, Polisi walimlipua kwa bomu Mwandishi wa Habari Ndugu Daudi Mwangosi. Pamoja na Polisi kuhusika na mauaji hayo bado Waziri wa Mambo ya Ndani, Ndugu Nchimbi, IGP Mwema, Kamanda wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Chagonja, RPC wa Mkoa wa Morogoro Shigolile na RPC wa Mkoa wa Iringa Kamuhanda hawakuchukua hatua yoyote ya kuwajibika kwa kuhusika moja kwa moja na matukio haya au kiutendaji katika Jeshi la Polisi kwa ujumla.


Ili kupata ukweli wa sababu za vifo hivyo, mauaji yote haya hayajafanyiwa uchunguzi wowote wa Kimahakama/ Kijaji kwa mujibu wa Sheria za nchi yetu kinyume na ahadi ya Waziri Mkuu Bungeni wakati akihitimisha hoja yake katika Bunge la Bajeti la mwaka 2011/2012. Hakuna uchunguzi wa kifo “inquest” uliofanyika na hakuna Mahakama ya korona “coroner’s court” iliyoanzishwa ili kuchunguza vifo hivi.


Kufuatia hali hiyo, Kamati Kuu ya CHADEMA ilifanya kikao maalumu siku ya Jumapili Tarehe 09 Septemba 2012 katika Hoteli ya Blue Pearl, Jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kilijadili hali ya siasa nchini kufuatia mfululizo wa mauaji yanayofanywa na Jeshi la Polisi katika shughuli za kisiasa za CHADEMA na mipango ya baadhi ya viongozi wa Serikali ya kudhibiti vuguvugu la mabadiliko (M4C) kwa mbinu haramu.


Kamati kuu ilizingatia masuala mbalimbali na kupitisha maazimio nane na kuamua kumuandikia barua Rais kwa lengo la kumtaka achukue hatua za utekelezaji kwa mujibu wa mamlaka yake na kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Iwapo Serikali haitazingatia, CHADEMA kitawaongoza wananchi kwa njia za kidemokrasia ikiwemo maandamano ya amani kushinikiza hatua za haraka kuchukuliwa kwa maslahi ya taifa.


Katika majadiliano ya kina kabla ya kufikia maazimio na maamuzi hayo, Kamati Kuu ilizingatia kuwa hali ya siasa nchini ni tete, Serikali inayoongozwa na CCM imeshindwa kusimamia vizuri rasilimali za nchi ikiwemo kudhibiti mfumuko na ongezeko la bei, hivyo kuchangia katika ugumu wa maisha kwa wananchi na migogoro ya kijamii na ufisadi nchini.


Taifa limegubikwa na tuhuma za vyombo vya Serikali kutenda kinyume na haki za kikatiba na kutumiwa kudhibiti mabadiliko kwa njia haramu ikiwemo kuteka na kutesa (Mf. Tukio la Dr Ulimboka), kulifungia gazeti la Mwanahalisi na kufanya vurugu na mauaji katika shughuli halali za kisiasa za CHADEMA.


Pamoja na hali hiyo, Kamati Kuu iliazimia kuwa Operesheni ya M4C iendelee na kazi zake kwa kufuata kikamilifu ratiba iliyopitishwa na Baraza Kuu na Kamati Kuu katika vikao vya awali kiwa ni sehemu ya kutimiza dhima yake ya kuleta uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganizesheni thabiti kwa maendeleo endelevu ya Tanzania.


Imetolewa tarehe 19 Septemba 2012 na:


John Mnyika (Mb)

Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
 
Changa la macho hilo ili kujikosha na kashfa ya kutoa kafara watoto wa watu. Kuna ulazima gani wa rais kutoa kauli wakati ambapo hatua zimeshachukuliwa? Mbayuwayu in action.

Mbona Kikwete haongei chochote juu ya mauaji haya ya kinyama, angekuwa hana tabia ya kuwa karibu na misiba angalau tungemuelewa.
 
Vipi waraka wa kususia TBC bado unapikwa au mnaufanyia tahariri?
 
Sheria ni msumeno, Ningekuwa Rais ningeanza na kuchukua hatua dhidi ya CHADEMA kwa sababu, chanzo cha vifo vya watanzania wasiyo na hatia ni maandamano na mikutano yao isiyo rasmi.

Mauaji ya kupangwa haya, yaani CDM wawaite watu kwenye mikutano halafu wawaue, it defies logic. Mbona waislam wamefanya maandamano majuzi na hakuna aliyeuawa wala kujeruhiwa. Kuna nini hapa.
 
We unadhani baada ya janja yao kubwainika, watajisafishaje? Mfa maji haishi kutapatapa.
 
Hivi mizoga kama hii JF imefikaje?Toka lini taasisi,kampuni au chama kikashtakiwa kwa kosa la jinai tena mauaji.
 
Back
Top Bottom