CHADEMA wamjibu Dk. Nchimbi, wagoma kuhojiwa na Polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA wamjibu Dk. Nchimbi, wagoma kuhojiwa na Polisi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 10, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema hakiwezi kukubali viongozi wake wanaodaiwa kutishiwa maisha kuhojiwa na Jeshi la Polisi kama imevyoelekezwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi kwani hawana imani na Polisi.

  Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Peter Slaa alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari Makao Makuu ya chama hicho Kinondoni jijini Dar es Salaam.


  Akitoa tamko hilo ambalo limepitishwa na Kikao cha Kamati Kuu iliyokutana tangu juzi, Dk. Slaa amesema hawaoni sababu ya kuhojiwa na Jeshi la Polisi kwa kuwa wamewahi kuwapa taarifa nyingi za vitisho dhidi yao na hakuna hata moja imefanyiwa kazi.


  "Hatuwezi kwenda Polisi kwa sababu tumekuwa tukipeleka mambo mengi ya vitisho lakini hayafanyiwi kazi…na hili tulisha waambia hatuendi kwao labda watukamate," alisema Dk. Slaa akizungumza na waandishi wa habari.  Alisema yeye mwenyewe licha ya kuwasilisha madai mbalimbali aliwahi kutegeshewa vinasa sauti na kutoa taarifa polisi lakini tangu wachukue vifaa hivyo hawajasema chochote hadi leo, jambo ambalo limewafanya waamini hata wakienda huko hakuna chochote kitafanyika.  Dk. Slaa alisema leo asubuhi alipigiwa simu na mmoja wa maofisa upelelezi kutoka Makao Makuu ya Polisi akiomba miadi ya kukutana naye, jambo ambalo amesema hayupo tayari kuhojiwa na wanausalama hao wa raia labda wamkamate.  Alisema tayari baadhi ya viongozi wa Serikali wameanza kuipuuza malalamiko yao dhidi ya vitisho wakidai huenda viongozi wa CHADEMA wanatafuta umaarufu wa kisiasa kwa kutoa taarifa hizo, kitendo ambacho amesema umaarufu wao hautatokana na viongozi wa Serikali au CCM bali ni kwa kazi wanazozifanya kwa wananchi.  Juzi Dk. Nchimbi alisema taarifa za kutishiwa maisha dhidi ya viongozi wa CHADEMA ni nzito hivyo haziwezi kupokelewa kirahisi Jeshi la Polisi linaanza kazi ya kuwahoji wahusika ili kulifanyia kazi jambo hilo. Alisema suala la usalama wa raia si hiyari bali ni la lazima hivyo hata kama wahusika hawataki lazima taratibu zifanywe kuhakikisha usalama kwa wahusika.
  Wakati huo huo CHADEMA inaanza ziara ya Oparesheni Sangara ambayo itafanyika katika mikoa mitano ya Tanzania ikiwemo Dodoma, Morogoro, Iringa na Manyara. Akizungumzia ziara hiyo ambayo itashirikisha viongozi wa juu wa CHADEMA, Wabunge, Wajumbe pamoja na viongozi wengine wa ngazi mbalimbali.

  Dk. Slaa amesema ni ziara ya kukiimarisha chama ikiwa ni pamoja na kuangalia mchakato wa uchaguzi wa chama hicho unaoendelea ngazi za chini.  Alisema katika ziara hiyo ambayo kauli mbiu yake ni "Hakuna Kunywa, Kula wala Kulala" inatarajiwa kuzunguka katika majimbo ya uchaguzi 44 ya mikoa hiyo, Kata 806 na vijiji 4,000. Ziara hiyo inatarajia kutumia siku 104.


  Akifafanua zaidi kuhusiana na ziara hiyo amesema CHADEMA ni chama ambacho kinajitofautisha na vyama vingine katika utendaji wake na ndiyo maana wanaendelea kufanya ziara zao vijijini kuangalia maisha ya wananchi mpango ambao ni mpya.


  "Kuna taarifa za baadhi ya watu wanabeza ziara zetu kwamba zinalenga posho…no CHADEMA hakuna posho, kwenye ziara zetu tunakula hadi kwa mama ntilie (chakula cha kawaida), tutaendelea kupiga kelele hadi pale haki za Watanzania zitakapokuwa zikipatikana bila vikwazo…tunapigania haki ya kila mmoja awe mwanafunzi, wafanyakazi, wakulima na hata madaktari," alisema Dk. Slaa.


  *Habari hii imeandaliwa na Mtandao wa Thehabari.com (www.thehabari.com)


  [​IMG]   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jul 10, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Hata Mimi nisingekwenda huko Polisi, haujui utarudi na vidole au Meno au la... kama ni kwenda ni kubeba umati wa

  watu kama mashahidi na lawyer wako awe pembeni. Hii ya kuamini POLISI anayefanya kazi chini ya chama tawala

  Hapana kabisa. Nchi yetu imeharibika tulikuwa hatuna matatizo kama hayo, naona mali zinawawesua viongozi

  Madarakani...
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  Jul 10, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  kesho nitatuma vijisenti vyangu kutunisha kimfuko kuwa wezesha makamanda kwenye hiyo kampeni...
   
 4. t

  thatha JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Wanaogopa kuumbuka mana walikurupuka kutoa habari za uongo,hatudanganyiki.
   
 5. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #5
  Jul 10, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  a migomo;4214452]Wanaogopa kuumbuka mana walikurupuka kutoa habari za uongo,hatudanganyiki.[/QUOTE
   
 6. t

  thatha JF-Expert Member

  #6
  Jul 10, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  za sabodo zinmeliwa na wajanja wachache,we utatoa ngapi zitoshe.peleka watu wamalizie kujenga majumba yao.
   
 7. t

  thatha JF-Expert Member

  #7
  Jul 10, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Hawa jamaa sasa ni wasanii rasmi.
   
 8. m

  markj JF-Expert Member

  #8
  Jul 10, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  nyumba ya dr ulimboka ! ile ya salasala anayomjengea josefina ! rais wa migomo acha acha ntamwaga mchele wote unajua!
   
 9. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #9
  Jul 10, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Hiki chama kinajengwa na wenye mapenzi mema kwa Tanzania siyo wenye mapenzi mema kwa CCM kama wewe
   
 10. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #10
  Jul 10, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Kama wewe ni mtoto wa kiume,wazazi wako wamekula hasara!
   
 11. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #11
  Jul 10, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Nadhani amesahau pamoja na kula kwa mama ntilie pia hupita kwenye nyumba za viongozi wa serikali na kula.source Lema na Ole Milya kwa Mh Membe.
   
 12. M

  Magesi JF-Expert Member

  #12
  Jul 10, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 2,590
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Habari zipi za uongo unaekurupuka uwezo wako wa kufikiri umeishia hapo2
   
 13. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #13
  Jul 10, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nani aende kutolewa meno na kucha? Dr usiende huko polisi acha waje kuwakamata nguvu ya umma waone matokeo yake.
   
 14. Ndoa

  Ndoa JF-Expert Member

  #14
  Jul 10, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Nguvu ya uma. Sauti ya wengi husikika.
   
 15. M

  Mabala The Farmer Member

  #15
  Jul 10, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata kama mimi siendi,tena mkuu we President wetu 2015 usiendee,Tuhuma ngapi walizonazo mezani na zina ushahidi hawajatoa majibu? Wao wamzoea kulinda mabenki na sisiemu,kazi ya kuhoji wanaitoa wapi? Walikula kiapo cha kuuwa na kutesa sasa mwambieni Mh.Nchimbi na yeye ataomba kuhamishwa uwizara maana anafikiri pale ni jukwaa la siasa. Hebu atujibu tuhuma zifuatazo majibu yapo wapi?
  1.Kuuwa kwa Kombe
  2.Kolimba
  3.Mtoto wa Malecela
  4.Kumwagiwa Tindikali Said Kubenea
  5.Kutaka kubambikiwa kesi ya Drugs mtoto wa Mengi
  6.Waliotiwa mbaroni vifo vya Ndg wauza Madini kutoka Ulanga
  7.Aliyetambuliwa na Dr.Ulimboka
  8.Waliotaka kumua Mh.Dr Mwakyembe
  kwa hizo chache tu tunaomba majibu.
  Kwanza pia naomba kuuliza Jeshi la Polisi halina msemaji na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tz hakuna!
   
 16. S

  SHEMGUNGA JF-Expert Member

  #16
  Jul 10, 2012
  Joined: Jan 13, 2012
  Messages: 653
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  nitaipenda cdm daima mpaka kieleweke sina meng wakubwa!
   
 17. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #17
  Jul 10, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,246
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  In Chadema we trust!
   
 18. T

  Topical JF-Expert Member

  #18
  Jul 10, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Aisee hata akiwa rais atawafukuza polisi wote Tanzania (maana hawafai)..(makofi tafadhali..)

  Atawafukuza Usalama wa taifa wote (maana hawafai)...(Makofi tafadhali..)

  Atawafukuza Magereza wote (maana hawafai)..makofi tafadhali..

  Slaa we kiboko..ha ha ha ha..
   
 19. kinya

  kinya JF-Expert Member

  #19
  Jul 10, 2012
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 483
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  kazi halisi/mahususi ya hela ni kutumika/kuliwa,kama hela inaliwa /inatumiwa na watu ninao waamin na kuwakubali kwani wakifanyacho nakiona nakikihisi wacha wale kule hawa wengine wanaichukua hela yangu bila hiari kupita PAYE na wanaitumia watakavyo BILA MIMI KUONA NA KUHISI CHOCHOTE CHA KIMABADILIKO.
  WACHA MAJEMBE YALE HELA YANGU WANILETEE UKOMBOZ
   
 20. chitalula

  chitalula JF-Expert Member

  #20
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,307
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hapa ndipo ninapompendea dr, huwa anafanya vitu ambavyo watu hawavitarajii kabisa na vinavyohitaji ujasiri
   
Loading...