Chadema wamezidi kuanguka Uzini ukilinganisha na Uchaguzi wa 2010 - Jussa

Jussa ni mbabaishaji,tathmini ya cuf ameshindwa kueleza anadandia ya cdm.kama anasema siasa za uzinzi wanaijua basi wameuza ushindi na kupokea fungu,inakuaje kama mtoto wako hajui kusoma umpeleke form one.?
 
Huyu Jusa atakuwa anamatatizo katika mathematics. Inabidi arud darasan akafundishwe mathematics mana naona anazidi kuchanganyikiwa kila siku ni heri ya jana

Buto,
Ebu tuambie matatizo ya Jussa ni yapi? Jussa kasema kura za Chadema zimeshuka kutoka 617 hadi 281.
 
Na wewe Jussa ebu tumia akili kidogo,hauoni hata idadi ya wapiga kura imepungua?maana hata idadi ya kura kwa vyama vyote ilivyokua 2010 ni pungufu ya sasa!hacha fikra mgando!

kutokana na matokeo ya mwaka 2010

kura waliuzopata

CCM 6,651

CHADEMA 617

CUF 524

kura walizopata kwenye uchaguzi mdogo

CCM 5,377
CHADEMA 281

CUF 223

kutokana na data hizo hapo utagundua vyama vyote vimepata kura pungufu ukilinganisha na 2010 utaona wote wameanguka asilimia zifuatazo?

sasa kupungua kwake

CCM 19.2%
CHADEMA 54.5%

CUF 57.4%

kwa hio utagundua kuwa CHADEMA na CUF wote wameanguka zaidi ya nusu ya kura walizopata mwaka 2010. ni kweli CHADEMA ukilinganisha na CUF wao slightly wako afadhali ukilinganisha na CUF lakini kwa kiwango hicho, na nguvu zilizotumika inaonekana chadema wakiri bado hawakubaliki
 
Na wewe Jussa ebu tumia akili kidogo,hauoni hata idadi ya wapiga kura imepungua?maana hata idadi ya kura kwa vyama vyote ilivyokua 2010 ni pungufu ya sasa!hacha fikra mgando!

Hizo zaitwa fikra na akili za Kijusa-jusa.
 
kutokana na matokeo ya Uchaguzi uliofanyika uzini, ukweli ni kuwa chadema wamezidi kuanguka na sio kuipiku CUF kama ilivyokuwa ikinadiwa hapa.

haya ni maneno ya Jussa alioandika kwenye facebook akiambatanisha na takwimu za uchaguzi uliofanyika mwaka 2010

Nimeulizwa sana kuhusu matokeo ya Uzini. Bahati mbaya kama ilivyo kawaida ya Watanzania walio wengi huwa hatufanyi utafiti, uchambuzi wala upembuzi na badala yake tunakuwa wepesi wa ku-draw conclusion. Kumekuja analysis kuwa Chadema sasa inaipiku CUF kwa kushika nafasi ya pili na wengine wakadiriki kusema kufukuzwa kwa Hamad Rashid kunakiathiri Chama. Niwarejeshe kwenye matokeo ya 2010 kwa nafasiya Ubunge jimbo la Uzini ambapo CCM ilipata kura 6,651, Chadema 617 na CUF 524. Aliyekuwa mgombea wa Chadema kwa nafasi hiyo ni huyu Ali Mshimba Mbarouk ambaye amegombea Uwakilishi mara hii. Sasa kutoka kura 617 hadi 281 amepoteza mvuto kiasi gani? Isitoshe, CUF kwa kuzielewa siasa za Zanzibar hatukusumbuka kutumia fedha nyingi. Tumetumia milioni 7 tu wakati Chadema wamenambia wametumia milioni 60 (haidhuru mimi naamini wametumia zaidi kwa mambo tuliyoyaona kule). Sasa katika hali hiyo, kuna lipi jipya? Nani aliyepoteza? CUF inajua inachokifanya.

Tuungane wapenda amani wote kupinga udini
 
Jussa anajiliwaza kupitia mgongo wa chadema. Jussa faraja yako iko CUF.........................Hongereni CDM kwa kuwabwaga CUF.
CCM sio saizi yenu.
 
Hamna wanachoelwa hao maandazi, wanropoka tuu, wameshakuwa na uhakika wa kupokezana madaraka wanafuraahi. Hakuna kiongozi wa CUF atapata uraisi visiwani, CCM haikubaliani na hilo hata kidigo, watendelea kufuata tuu kwa stail hii. Chama kinapoteza mvuto kwenye maskani yake ya asili na bado wanajipa moyo, damn fools
 
inasikitisha sana kuona matokeo haya kushangiriwa kwa vyama vya CUF na Chadema.ukweli wote wamepoteza tena kwa san

uk
 
kutokana na matokeo ya Uchaguzi uliofanyika uzini, ukweli ni kuwa chadema wamezidi kuanguka na sio kuipiku CUF kama ilivyokuwa ikinadiwa hapa.

haya ni maneno ya Jussa alioandika kwenye facebook akiambatanisha na takwimu za uchaguzi uliofanyika mwaka 2010

Nimeulizwa sana kuhusu matokeo ya Uzini. Bahati mbaya kama ilivyo kawaida ya Watanzania walio wengi huwa hatufanyi utafiti, uchambuzi wala upembuzi na badala yake tunakuwa wepesi wa ku-draw conclusion. Kumekuja analysis kuwa Chadema sasa inaipiku CUF kwa kushika nafasi ya pili na wengine wakadiriki kusema kufukuzwa kwa Hamad Rashid kunakiathiri Chama. Niwarejeshe kwenye matokeo ya 2010 kwa nafasiya Ubunge jimbo la Uzini ambapo CCM ilipata kura 6,651, Chadema 617 na CUF 524. Aliyekuwa mgombea wa Chadema kwa nafasi hiyo ni huyu Ali Mshimba Mbarouk ambaye amegombea Uwakilishi mara hii. Sasa kutoka kura 617 hadi 281 amepoteza mvuto kiasi gani? Isitoshe, CUF kwa kuzielewa siasa za Zanzibar hatukusumbuka kutumia fedha nyingi. Tumetumia milioni 7 tu wakati Chadema wamenambia wametumia milioni 60 (haidhuru mimi naamini wametumia zaidi kwa mambo tuliyoyaona kule). Sasa katika hali hiyo, kuna lipi jipya? Nani aliyepoteza? CUF inajua inachokifanya.

Jussa sisi tulidhani kwamba kutokana na vikaratasi vya udini vilivyosambazwa uzini dhidi ya chadema na taarifa za kuihusisha chadema na ukristo kungeweza kuisidia CUF kuwa mbele ya chadema kama sivyo basi CUF mmekwisha tuhuma hizo ilikuwa ni ushindi tosha kwenu CUF kuwa namba 2
 
inasikitisha sana kuona matokeo haya kushangiriwa kwa vyama vya CUF na Chadema.ukweli wote wamepoteza tena kwa san

uk

chama cha kikristo kama kinavyoitwa na baadhi ya wanasiasa wa maji taka kimefanya vizuri kushika namba 2 kuliko 3 kwenye ngome ya waislamu wengi. Katika matokeo ya mtihani namba 2 ni bora kuliko 3.
 
Jussa sisi tulidhani kwamba kutokana na vikaratasi vya udini vilivyosambazwa uzini dhidi ya chadema na taarifa za kuihusisha chadema na ukristo kungeweza kuisidia CUF kuwa mbele ya chadema kama sivyo basi CUF mmekwisha tuhuma hizo ilikuwa ni ushindi tosha kwenu CUF kuwa namba 2

mbona hata 2010 walikuwa wa pili ? sasa upili kama ni hoja basi hilo lilikuwa liwe tokea 2010. ukweli ni kuwa mmepoteza na huu ndio ukweli mchungu. kubali mapungufu yako
 
Back
Top Bottom