Opportunity Cost
JF-Expert Member
- Dec 10, 2020
- 9,035
- 6,907
Ukiwa na akili timamu huwezi wasikiliza CDM wameshikwa pabaya sasa wanatafuta attention kwa lazima na ambavyo serikali imetangaza ajira za ma pot ndio wamechanganyikiwa kabisaWanaukumbi.
CHADEMA tuelezeni hizo Tozo Mpya zinaingizia serikali kiasi gani cha Pesa Kisha mtueleze matumizi ya serikali kama mnavyodai zinaenda kununua mabomu na kulipa polisi mishahara.
Serikali inasema hizo Tozo zitakwenda Tamisemi kujenga madarasa na zahanati zingine zinaenda Taruru kujenda barabara vijijini.
Heche na Lema wanawajaza watu ujinga huko Space, mnawambia watu et wafanye boycott Campaign hii mara nyingi inatumika kwa bidhaa au huduma mfano kampeni za kususia Coca Cola nunua Pepsi au kususia vifurushi vya Vodacom nunua Tigo. Lengo ni kunyoosha kampuni kama haisimamii haki. Unasusia serikali ili umuumize nani kodi zinamnufaisha nani?
Ukisusia kununua Petrol utauza gari au kulipaki nyumbani ukisusia kununua vifurushi tuanze kuandikiana barua au tupeleke salamu kwa mkono?
Ukisusia maji, vinywaji, vyakula utaishi au utakufa.
Miradi ya maendeleo kama Barabara, Huduma za Afya, Shule, zinamnufaisha nani?