CHADEMA wamekosea, sio UKUTA bali ni CHAKUTA

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
34,962
41,534
Baada ya CHADEMA kuweka mkakati kwa mpango ambao tayari umeshafeli kabla ya utekelezaji wake walioupa jina la UKUTA, ningependa kuwasahihisha kidogo na kuwakumbusha kua neno sahihi linalofaa badala ya hilo wanalolitumia ni CHAKUTA.

CHAKUTA ni neno sahihi kwani mwenendo mzima wa CHADEMA umekuwa ni katika kupinga kila jambo linalofanyika sasa, ninaposema CHAKUTA namaanisha Chama cha Kupinga Kila kitu Tanzania, hilo linafaa sana kwa sasa.

Hivyo basi badala ya kupoteza muda kwenye UKUTA, ni vyema wakaelekeza nguvu na kili katika CHAKUTA maana huko kuna uwezekano wa kufanikiwa zaidi kuliko huko walipokuanza.

Vile vile nishauri kwamba UKUTA haitafanikiwa kwani siasa za nchi hii zimebadilika sana, na wananchi hawapo tayari tena kuona wakipata matatizo kwa ajili ya lengo lisilokuwa na faida kwao, CHADEMA kimewakwaza watu wengi hivyo imani imewatoka kabisa.

Ukiachana na hilo la kupoteza imani kwa wananchi, Serikali ya sasa inaonekana kufanya kazi yake kwa kugusa mambo nyeti yaliyokua yakipiganiwa na wengi kwa muda mrefu, hivyo movement hii kuonekana kama jitihada za makusudi za kukwamisha nia njema iliyopo kwa serikali ya sasa.

Wanachi wameamua kuachana na siasa za maandamano na kufanya kazi.
 
Majizi Chadema hatuna hamu nao huku Arusha.

Wametuibia vibanda vyetu
 
Ccm mmepagawa, hali yenu mbaya zile kura m.6 zimeongezeka kwa wafanyabiashara wote, watumishi wote, na wasiokunywa chain wote.
 
UKUTA waleta taharuki kila sehemu ni UKUTA kila mtu ni UKUTA.

Source: Magazetini.
 
Majizi Chadema hatuna hamu nao huku Arusha.

Wametuibia vibanda vyetu
Mlizoea kuiibia halmashauri mpendavyo, karibu viongozi wote wa ccm Arusha walijikodishia vibanda kwa zaidi ya miaka 20 utadhani wengine hawataki kufanya biashara, sasa mmekutana na UKUTA mnaanza kulialia, na bado mtaisoma zaidi.
 
huo ni upeo wako wa mwisho wa kufikiri
Baada ya Chadema kuweka mkakati kwa mpango ambao tayari umeshafeli kabla ya utekelezaji wake walioupa jina la UKUTA, ningependa kuwasahihisha kidogo na kuwakumbusha kua neno sahihi linalofaa badala ya hilo wanalolitumia ni CHAKUTA.

CHAKUTA ni neno sahihi kwani mwenendo mzima wa Chadema umekua ni katika kupinga kila jambo linalofanyika sasa, ninaposema CHAKUTA namaanisha Chama cha Kupinga Kila kitu Tanzania, hilo linafaa sana kwa sasa.

Hivyo basi badala ya kupoteza muda kwenye UKUTA, ni vyema wakaelekeza nguvu na kili katika CHAKUTA Maana huko kuna uwezekano wa kufanikiwa zaidi kuliko huko walipokuanza.

Vile vile nishauri kwamba UKUTA haitafanikiwa kwani siasa za Nchi hii zimebadilika sana, na wananchi hawapo tayari tena kuona wakipata matatizo kwa ajili ya lengo lisilokuwa na faida kwao, Chadema kimewakwaza watu wengi hivyo imani imewatoka kabisa.

Ukiachana na hilo la kupoteza imani kwa wananchi, Serikali ya sasa inaonekana kufanya kazi yake kwa kugusa mambo nyeti yaliyokua yakipiganiwa na wengi kwa muda mrefu, hivyo movement hii kuonekana kama jitihada za makusudi za kukwamisha nia njema iliyopo kwa serikali ya sasa.

Wanachi wameamua kuachana na siasa za maandamano na kufanya kazi.
 
....polisi usinikamate ntakupa buku shing'tano!
..Ukonga,Keko,Segerea!..chakula bure,kulala bure...,
..UKUTA bure!
 
Hujui hata namna ya kufupisha na kutengeneza finyazo
Mkuu hapa hakuna mashindano ya namna ya kutengeneza finyanzo, ila what surprises me most ninamna watu wazima kabisa tena kamati kuu ya Chama imekaa na kutengeneza neno UKUTA, Doesn't that sound childish to you??
 
Talk is cheap, mtoa mada huna jipya, onea huruma muda wetu si kwa mashudu haya
Ajabu ya karne ni kwa Chadema kupoteza muda kuja ya hilo tamko la kisekondari, Ujinga hujibiwa na Ujinga, UKUTA size yake ni CHAKUTA...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom