CHADEMA wamefanya makubwa Tanzania: Tutarajie mapambazuko zaidi ya kifikra!

Mbelwa Germano

JF-Expert Member
May 7, 2011
789
289
Heshima Kwanza!

"KAMA watu wawili wana fikra sawa na mtazamo sawa katika kila kitu cha kila jambo, basi, kuwa na uhakika kwamba ni mmojawao tu ndiye mwenye kufikiri”-Lyndon Baines Johnson (LBJ) raisi wa 36 wa Marekani (1963-1969)(Tafsiri).

Ipo mitazamo na imani mbalimbali za kibaguzi iliyojaribu kujengwa dhidi ya vyama vya upinzani toka kuanza kwa mfumo wa vyama vyingi nchini inayolenga kudumaza changamoto za kifikra. Wapo watu wengi walioamini/wanaoamini upinzani ni njama ya kihaini, kashfa, mauaji, matusi, uzushi, au machafuko yanayoondoa dhana halisi ya kichocheo cha changamoto za demokrasia au maendeleo. Wapo baadhi ya viongozi wa kisiasa waliamini/wanaamini kwamba ukubwa wao au mali zao zinastahili kuwalinda hata wanapofanya maovu, hujifikiria wao zaidi na wanaowahusu kuliko manufaa ya taasisi au eneo waliomo na kujidanganya kwa kudhani siku zote watakuwa katika hali na nafasi waliyonayo.

Wakati huu ambapo CHADEMA kinazidi kukubalika kwa kasi kuna baadhi ya watu wanahoji: Je hao CHADEMA wamefanya nini? Ni haki yao ya kimsingi kuhoji lakini naomba niwakumbushe: wamesahau kwamba leo hii kila jambo wanalofanya CCM wanatazama upande wa pili CHADEMA watasema nini?, wanaangalia mbele, wananchi kwa ujumla watasema nini? Nadhani sasa tuweke wigo mpana wa kifikra kutazama nini kazi ya upinzani katika kuleta ushindani wa kisiasa, kudumisha demokrasia, kuimarisha utawala bora na kujenga misingi imara zaidi ya maendeleo?

Kwa nafasi waliyonayo CHADEMA kama chama kikubwa cha upinzani nchini wanastahili sifa na heshima kubwa. Kujenga na kuimarisha chama cha siasa si kazi lelemama, ni kazi inayohitaji UMAKINI, UVUMILIVU na UJASIRI. Kazi kubwa ya chama chochote cha upinzani ni kupima na kupinga ufanisi duni wa serikali ya chama kinachotawala na kujiweka katika nafasi ya kuaminiwa na wananchi ili kupewa ridhaa ya kuongoza na kuongeza ufanisi katika kusukuma gurudumu la maendeleo. Na haya ndio baadhi ya machache ambayo CHADEMA inafanya kama chama cha upinzani Tanzania.Tayari CHADEMA wamefanya na wanafanya, sasa tuwaulize wale wanaosema CHADEMA wamefanya nini walitaka wafanye nini?

Bila ujasiri wa wabunge wachache wa CHADEMA kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 jamii ilikuwa imefunikwa kwenye wingu kubwa la kufungwa kufikra juu ya mustakabali wa nchi yao. Wamesahau kwamba bila CHADEMA leo hii usingesikia wimbo wa kujivua MAGAMBA ndani ya CCM.

CHADEMA wamefungua minyororo ya kifikra na kuleta mapamazuko mapya. Ieleweke kwamba maendeleo yoyote ya kiuchumi na kijamii yanaanza na mapambazuko ya kifikra. "Hakuna jibu moja linaweza kutumika wakati wote na mahali pote","bila kutambua kwa utashi, kuelewa na kukubali juu ya matatizo yetu, hatuwezi kufanya maamuzi sahihi katika kudai haki za kimsingi katika jamii. Dhana ya kufikiri kwa bidii dio nyenzo muhimu ya kulinda uzalendo na uadilifu bila kuathiri utu wetu.
“…kuchaguliwa kuunda utawala wa kuongoza nchi hakumaanishi kuchaguliwa kujitawalia mamlaka ya umma na kisha kutumia mamlaka hayo kuwakandamiza “waliokuchagua” kwa sababu tu ya kutetea maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma”. (Katiba ya CHADEMA)

Uwepo wa CHADEMA haulengi kugawa wananchi katika jamii yetu ili kudhoofisha maendeleo kama baadhi ya watanzania wenzetu wanavyotaka tuamini, bali ni njia ya kulinganisha sera, fikra na mitazamo katika kuchochea maendeleo.

Think Twice...Act and react wise!
 
Siku zote sehemu ambayo hakuna upinzani/ushindani hakuna maendeleo au changamoto.Wanao wabeza upinzani ni kwajili ya maslahi yao binafsi.

Kaskazini kulikuwa na maendeleo sababu walianza upinzani/kutofautiana na mwalimu tangia enzi za chama kimoja,Vikaja vyama vya upinzani kaskazini wakawa wakwanza kuanzisha vyama vya upinzani na ndiyo maana kukawa na maendeleo, mtu akichaguliwa ni lazima afanye maendeleo ktk jimbo lake sababu alijua wazi asipofanya kitu hawezi chaguliwa tena, ila kule kwa wenzangu na mie mtu alikuwa hajishughulishi sababu alijua akisha pata ni mpaka yeye amue kuachia ngazi na si kuwajibishwa na wanachi/upinzani na ndiyo maana mpaka leo kusini inaendelea kuwa nyuma kimaendelea na kuwa kambi ya wale wale.

Wakidanganywa ya kuwa mkiwachagua CHADEMAupinzani watawagawa ki kanda na kidini,je mbona hao ambao hawajawagawa kidini na kikanda wamewagawa kielimu kiafya na kimaendele hawajawakataa. Kusini tafakari chukua hatua.Kusini nako ni sehemu ya tanzania tunataka upinzani na maendeleo viwepo.
 
Heshima Kwanza!..."KAMA watu wawili wana fikra sawa na mtazamo sawa katika kila kitu cha kila jambo, basi, kuwa na uhakika kwamba ni mmojawao tu ndiye mwenye kufikiri"-Lyndon Baines Johnson (LBJ) raisi wa 36 wa Marekani (1963-1969)(Tafsiri).
Nakupongeza kaka...ni wachache wanajua lakini kwa move hii atimaye kila mtu sasa atajua maana ya vyama vya upinzani...maana cc sasa ni mabalozi kama wewe
 
Kuna msemo wa kiswahili unaosema "usilolijua ni sawa na usiku wa giza", laiti kama tungekuwa tunakumbushana mara kwa mara ule wajibu tulio nao wa kufikiri kwa bidii leo hii tungekuwa tumepata mapambazuko makubwa ya kifikra juu ya mustakabali wa nchi yetu chini ya mfumo wa vyama vingi.

Katika nyakati hizi ambapo siasa ya Tanzania imejaa hadaa na uongo mwingi lazima wananchi na viongozi wa kisiasa waonyeshe umuhimu wa kufikiri kwa bidii na kufanya maamuzi yenye tija kwa maslahi ya nchi yetu. Tuondoe fikra za kibaguzi zinazoondoa dhana halisi ya demokrasia, haki, utu wa binadamu na utawala bora. Lazima tufikiri kwa bidii kwanini nchi yetu imezubaa kimaadili na kizalendo, nini fursa ya mtanzania? Je fursa hizo tunazitumia ipasavyo? Na nini suluhisho?

CHADEMA wameonyesha njia sasa ni wakati wa wanawake wa Tanzania kuanza kufunga vilemba vya maarifa, Wazee wa Tanzania kuvaa kofia za hekima na busara na Vijana kuvaa kofia za fikra pevu. Tutarajie mapambazuko zaidi.
 
Mkuu tuongeze ari hii ya kuwaelezea wananchi kuhusu CDM na kikubwa ni Vijana wengi tujipambanue na CDM ili kuwa aminisha wengine
 
uchambuzi wako umekaa vizuri sana na niweza kuona hata uwezo wako wa kufikiri ni mkubwa vile vile CHADEMA kama chama makini kimeweza kutoa changamoto kubwa sana kwa hawa wanaojiona wafalme wa hii nchi na kwa hili wanahitaji pongezi..kwa kawaida ukiona unaowaamini kuwa ni wakubwa wanahaha kutokana na uwepo wako basi ujue umewabana kuliko
 
Mkuu tuongeze ari hii ya kuwaelezea wananchi kuhusu CDM na kikubwa ni Vijana wengi tujipambanue na CDM ili kuwa aminisha wengine

Moja ya sifa kuu ya kijana ni kupenda kujua vitu tafauti tofauti kwa maana ya kutopenda kuishi kwa mazoea. Tofauti kati ya kijana na kijana haitokani na umri tu bali ni pamoja na utofauti wa kifikra katika kukabiliana na changamoto mbalimbali.

Angalizo: Tusikubali kufanywa kama ndege waendao mtegoni wakati wanamuona mtegaji kwasababu tu ya tamaa ya mali au kama ng'ombe waendaye machinjoni wakati wanamuona mchinjaji. Lazima tujenge utamaduni wa kuchagua viongozi wa kisiasa wanaohubiri mipango na kutekeleza wakipata nafasi ya kushika madaraka ya nchi, tuachane na ushabiki usiokuwa na tija, hakuna binadamu anayezaliwa na chama cha siasa.
 
Kimsingi hata CHADEMA wakichukua nchi -Mungu apishili mbali- watakuwa na matatizo pengine makubwa zaidi hata kuliko ya CCM.
Kioganaizesheni bado CHADEMA ni cha mtoto kwa CCM, na bado kuna sehemu nyingi tu nchi ambako CHADEMA haijulikani.

Lazima tuelewe ukweli kuwa umaarufu wa CHADEMA ni kutokana na MAKOSA ya CCM na si sera mbadala na nzuri za CDM.
Hilo ni jambo la msingi sana na CHADEMA wasisahau hilo.
Kimsingi CCM walipoteza touch na wananchi baada ya kuanza kukumbatia matajiri.
Walipokifikisha chama cha CCM matajiri hao, leo CCM inajuta-lakini walionywa hawakusikia.
Pamoja na wizi, kashfa ambazo hazijashughulikiwa umaarufu wa uongozi wa CCM umetia wananchi mashaka.
Hilo ndo kosa kubwa la CCM.

Kwa hiyo CHADEMA msije kubweteka, CCM waijisahihisha makosa yao bado sera za chama hiki zinaeleweka ukilonganisha na CHADEMA.

Kwa hiyo CDM usipime nguo kabla mwana hajazaliwa.
 
Kimsingi hata CDM wakichukua nchi -Mungu apishili mbali- watakuwa na matatizo pengine makubwa zaidi hata kuliko ya CCM.
Kioganaizesheni bado CDM ni cha mtoto kwa CCM, na bado kuna sehemu nyingi tu nchi ambako CDM haijulikani.

Lazima tuelewe ukweli kuwa umaarufu wa CDM ni kutokana na MAKOSA ya CCM na si sera mbadala na nzuri za CDM.
Hilo ni jambo la msingi sana na CDM wasisahau hilo.
Kimsingi CCM walipoteza touch na wananchi baada ya kuanza kukumbatia matajiri.
Walipokifikisha chama cha CCM matajiri hao, leo CCM inajuta-lakini walionywa hawakusikia.
Pamoja na wizi, kashfa ambazo hazijashughulikiwa umaarufu wa uongozi wa CCM umetia wananchi mashaka.
Hilo ndo kosa kubwa la CCM.

Kwa hiyo CDM msije kubweteka, CCM waijisahihisha makosa yao bado sera za chama hiki zinaeleweka ukilonganisha na CDM.

Kwa hiyo CDM usipime nguo kabla mwana hajazaliwa.

Jambo la muhimu tunalopaswa kutambua ni kwamba, kila binadamu anafanya makosa lakini hatupaswi kujiridhisha na makosa yetu bila kutumia fikra zetu kutafuta ufumbuzi mkubwa kusahihisha makosa yetu. Ukweli hautaki kupuuzwa hivyo tusijidanganye wenyewe na kujiridhisha kana kwamba matatizo na shida zetu hazihitaji fikra za juu zilizojaa hekima, ubunifu, uadilifu na busara.

Vilevile tunapaswa kutambua kwa dhati kwamba kutambua ukweli ndio njia ya kuamsha fikra na kuamini matendo chanya, kukubali ukweli wa maisha na kupambana kubadilika kuelekea kwenye mafanikio zaidi, hivyo lazima tutazame kwa ukaribu changamoto za nyakati.
 
nakupongeza kaka...ni wachache wanajua lakini kwa move hii atimaye kila mtu sasa atajua maana ya vyama vya upinzani...maana cc sasa ni mabalozi kama wewe
mkuu heshima mbele umechangia vizuri lkn unacopy story yoote unaboa wengine tunatumia cm so ni usumbufu
unataka
 
Jambo la muhimu tunalopaswa kutambua ni kwamba, kila binadamu anafanya makosa lakini hatupaswi kujiridhisha na makosa yetu bila kutumia fikra zetu kutafuta ufumbuzi mkubwa kusahihisha makosa yetu. Ukweli hautaki kupuuzwa hivyo tusijidanganye wenyewe na kujiridhisha kana kwamba matatizo na shida zetu hazihitaji fikra za juu zilizojaa hekima, ubunifu, uadilifu na busara.

Vilevile tunapaswa kutambua kwa dhati kwamba kutambua ukweli ndio njia ya kuamsha fikra na kuamini matendo chanya, kukubali ukweli wa maisha na kupambana kubadilika kuelekea kwenye mafanikio zaidi, hivyo lazima tutazame kwa ukaribu changamoto za nyakati.

Mkuu unamwaga filosofia ambayo kila mtu mwenye hekima anaifahamu.

Bado hujajibu counter argument yangu kuwa CDM in capitalize kisiasa kwa makosa ya CCM na si vinginevyo.
Makosa ya CCM hata wanaCCM wanaya fahamu, na kwa hivi sasa inaelekea CCM imexinduka kutoka kwenye usingizi mzito wa kiitikadi.

Sera za CCM zitabaki kuwa safi na kungwa mkono na wananchi walio wengi-arimradi CCM wakijipanga vizuri, na hili naona wameliona.
Hekima peke yake hailiwi balikuifanyia kazi hekima hiyo ndio jambo la msingi.

Sera za CDM bado ni kitendawili na nasisitiza kuwa CCm ikijipanga CDM itakuwa haina hoja ya msingi.
Kinachowaunganisha CDM ni makosa ya CCM na si sera za CDM.
 
Lengo la upinzani ni kuchukua madaraka, kama bado hawajachukua basi wakae tu uani, barazani wawaachie wazee wa kazi.
 
Mbelwa Germano,

CHADEMA is Evanescent, it only flourishes now due some weaknesses within CCM. The moment CCM get her act together, CHADEMA will take a back seat that is the truth:):A S shade:
 
Mbelwa Germano,

CHADEMA is Evanescent, it only flourishes now due some weaknesses within CCM. The moment CCM get her act together, CHADEMA will take a back seat that is the truth:):A S shade:

And the true democracy will start to prevail

Hata Democrat wanapata nguvu kutokana na makosa ya Republican and viceversa, ninachosisitiza kwenye uzi wangu ni Watanzania kupevuka kisiasa na kufikiri nje ya boksi, ukweli ni kwamba CCM hakiwezi kutawala daima na CHADEMA hawawezi kupendwa milele. Vileviele kumbuka leo hii Tanzania tuna vyama vya siasa zaidi ya 18, lakini ni vichache tu vimeweza kustahimili siasa za ushindani nchini na usifikiri kwamba CDM hapa kilipo fika ni kazi lelemama.

"Wapo watu wengi walioamini/wanaoamini upinzani ni njama ya kihaini, kashfa, mauaji, matusi, uzushi, au machafuko yanayoondoa dhana halisi ya kichocheo cha changamoto za demokrasia au maendeleo"

Sasa watanzania wameamka na kuanza kuelewa nini maana ya mfumo wa vyama vingi tofauti na nyuma kutokana na hayo makosa uliyosema ya CCM kwa kusahau itikadi yake wakati kinaanzishwa na kukumbatia ufisadi.
 
Mkuu unamwaga filosofia ambayo kila mtu mwenye hekima anaifahamu.

Bado hujajibu counter argument yangu kuwa CDM in capitalize kisiasa kwa makosa ya CCM na si vinginevyo.
Makosa ya CCM hata wanaCCM wanaya fahamu, na kwa hivi sasa inaelekea CCM imexinduka kutoka kwenye usingizi mzito wa kiitikadi.

Sera za CCM zitabaki kuwa safi na kungwa mkono na wananchi walio wengi-arimradi CCM wakijipanga vizuri, na hili naona wameliona.
Hekima peke yake hailiwi balikuifanyia kazi hekima hiyo ndio jambo la msingi.

Sera za CDM bado ni kitendawili na nasisitiza kuwa CCm ikijipanga CDM itakuwa haina hoja ya msingi.
Kinachowaunganisha CDM ni makosa ya CCM na si sera za CDM.

Nimefurahi kwamba wewe binafsi unakiri kwamba CCM kina matatizo lakini unafikiri ni kwa nini hayo makosa yameshindwa kuvipandisha chati UDP, CHAUSTA, NLD n.k na iwe CHADEMA. Na mimi sikuanzisha mada ili kushambulia CCM zaidi ya kueleza nafasi ya vyama vya upinzani ikiwepo CHADEMA katika kuleta mapambazuko ya kifikra nchini.

Nimeshaandika "...bila CHADEMA leo hii usingesikia wimbo wa kujivua MAGAMBA ndani ya CCM" na sijaona hizo unazoziita argument zako ambazo sijazijibu. Rudi kwenye mada, bado ni mwepesi sasa kujenga arguments zenye mashiko.
 
Mkuu wewe si mwanafunzi mzuri wa historia.

Dont try to give Cdm credit for what it is not.

Kujivua gamba ndani ya CCM haikuanzia na CHADEMA na haitaishia na chama hicho.

Soma vizuri on the Rules of Social Contradictions katika jamii.

Unawakumbuka Christopher Mtikila na Mapalala? Mababa wa upinzani wa kisiasa?

Walimpinga hata Mwalimu Nyerere at the pain ya kuswekwa kizuizini,na walikuwepo wengine.

CHADEMA wameflourish baada ya wao kuruhusiwa kuishi kisiasa. Kwa mtu ambaye ni mgeni katika siasa hataweza kukumbuka kuwa hapo nyuma palokuwepo kitu similar na kujivua gamba.

Soma historia ya CCM na utaona kulikuwepo na OPERATION TUJISASAHIHISHE,KUNG'ATUKA, UFAGIO Wa CHUMA- hatua maalum zilizochukuliwa ili kukinusuru chama cha Mapinduzi.
Hayo yote yalitokana na shinikizo toka NDANI ya CCM, na wala si chama kingine cha siasa, ambavyo havikuwepo anyway.

CHADEMA is right now only riding a wave of social discontent into the unknown, and when the water is calm, sink it will!
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom