CHADEMA wamefanya Maamuzi makini na magumu-Waziri Kombani

Greenwhich

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
1,337
968
WAZIRI AIPONGEZA CHADEMA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Celina Kombani, amekipongeza Chadema kwa utaratibu kilichoutumia kuwawajibisha viongozi wake kwamba ulikuwa ni mzuri na ulifuata taratibu za haki kwa pande zote.

Kombani alitoa kauli hiyo bungeni jana na kufafanua kuwa utaratibu wa kila upande kusikilizwa ni mzuri katika kutafuta makosa ya mtu.

Alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali (NCCR-Mageuzi) ambaye alitaka kujua kuhusiana na uamuzi wa serikali kuhamishwa kwa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kasulu (DMO), na kupelekwa mkoani Iringa huku akiacha tuhuma mbalimbali dhidi yake.

Aidha, katika swali lake la msingi mbunge huyo alitaka kujua ni sababu gani zinazoifanya Serikali kutowafukuza au kuwaachisha kazi watumishi wabadhilifu katika Halmashauri mbalimbali na badala yake baadhi wanahamishwa kutoka halmashauri moja kwenda nyingine.

Kombani alisema nidhamu katika utumishi wa umma iimewekwa kwa mujibu wa kisheria, kanuni na taratibu hivyo kama kuna ukiukwaji ni makosa na kuongeza kuwa mtu anapoachishwa kazi lazima taratibu husika zinafuatwe.

CHATO WAUNGA MKONO

Uongozi wa Chadema wilaya ya Chato, mkoani Geita, umesema unaunga mkono hatua iliyochukuliwa na Kamati Kuu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa Chadema wilaya ya Chato, Mange Ludomya, alisema uamuzi wa viongozi hao kuvuliwa nyadhifa zao ni hatua madhubuti na ya kupongezwa.

Alisema viongozi hao kwa muda mrefu wamekuwa mzigo kwa chama hicho kutokana na kuendekeza siasa za kimakundi, hatua ambayo imekuwa ikisababisha mgawanyiko kwa baadhi ya viongozi na wanachama.

Ludomya alisema uamuzi huo ulifuata katiba ya Chadema Ibara ya 7:7.16 kifungu kidogo (v) Inayoeleza kuwa ina wajibu wa kumwachisha ujumbe wa Kamati Kuu mjumbe mteule ambaye atakwenda kinyume cha katiba, kanuni na maadili au kushindwa kukidhi matakwa ya kuteuliwa kwake.

Alisema maamuzi magumu yaliyochukuwa dhidi ya viongozi hao yataendelea kukiimalisha chama hicho kutokana na msimamo wake wa kusimamia ukweli badala ya kuendelea kuleana na kuoneana aibu.

KUSINI WAUNGA MKONO

Uongozi wa Chadema Kanda ya Kusini inayoundwa na mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi umeunga mkono maamuzi ya Kamati Kuu ya kuwavua uongozi Zitto, Dk. Kitila na Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.

Akihutubia mkutano wa hadhara katika soko kuu ya mjini Songea jana, Mwenyekiti wa Chadema wa Kanda hiyo, Matiko Matare, alisema maamuzi hayo wanayaunga mkono kwa kuwa ni sahihi.

Alisema Zitto awali alionekana mzuri, lakini baadaye ilibainika kwenda kinyume cha taratibu za chama na kupendekeza kwamba wanaomuunga mkono ikiwezekana waondolewe ndani ya chama kwa kwua wanaweza kukiteka.

Source:Nipashe
 
Bora ningekuwa sijamsikia waziri nimemsikia neno baada ya neno....Huu ni uongo mwingine wa kimataifa.
 
[h=5]HISTORIA FUPI YA MAREHEMU CHADEMA

MAREHEMU ALIZALIWA 1992 NA AMEFARIKI 2013 , ALIPITIA CHANGAMOTO NYINGI SANA, KWANI MAREHEMU HAKUWAHI KWENDA SHULE KABISA. MAREHEMU AMEFARIKI AKIWA ANATIBIWA NA DAKTARI ALIYEPATA ZIRO FORM SIX BADALA YA KUMPASUA MAREHEMU MGUU AMEMPASUA KICHWA NA KUTOA UBONGO (ZITTO).

MAREHEMU AMEACHA MAMBULULA WENGI SANA MTAANI AMBAO HAWANA MSAADA WAMEBAKI OMBA OMBA.

CCM ILITOA NA CCM IMETWAA. JINA LA CCM LIDUMU
[/h]

bora ningekuwa sijamsikia waziri nimemsikia neno baada ya neno....huu ni uongo mwingine wa kimataifa.

kwahiyo kama ni uongo tuambie basi alisemaje... Inawezekana ulimsikia ila hukumuelewa coz wewe ni kilaza
 
HISTORIA FUPI YA MAREHEMU CHADEMA

MAREHEMU ALIZALIWA 1992 NA AMEFARIKI 2013 , ALIPITIA CHANGAMOTO NYINGI SANA, KWANI MAREHEMU HAKUWAHI KWENDA SHULE KABISA. MAREHEMU AMEFARIKI AKIWA ANATIBIWA NA DAKTARI ALIYEPATA ZIRO FORM SIX BADALA YA KUMPASUA MAREHEMU MGUU AMEMPASUA KICHWA NA KUTOA UBONGO (ZITTO).

MAREHEMU AMEACHA MAMBULULA WENGI SANA MTAANI AMBAO HAWANA MSAADA WAMEBAKI OMBA OMBA.

CCM ILITOA NA CCM IMETWAA. JINA LA CCM LIDUMU

mkuu huwezi kuacha ujinga wako na upumbavu wako.
 
tuambie mkuu, alisema nini? maana mleta mada ame quate chombo cha habari na vp we tukuamini kama nani?
 
historia fupi ya marehemu chadema

marehemu alizaliwa 1992 na amefariki 2013 , alipitia changamoto nyingi sana, kwani marehemu hakuwahi kwenda shule kabisa. Marehemu amefariki akiwa anatibiwa na daktari aliyepata ziro form six badala ya kumpasua marehemu mguu amempasua kichwa na kutoa ubongo (zitto).

Marehemu ameacha mambulula wengi sana mtaani ambao hawana msaada wamebaki omba omba.

Ccm ilitoa na ccm imetwaa. Jina la ccm lidumu

uongozi ni kipaji wewe... Mbona jk ana gentleman kidogo adisko.. Uongozi mubovuuuuu
 
Gazeti la NIPASHE tunajua mnamtumikia nani (MENGI NA MTEI NI MARAFIKI) ptuuu
 
Back
Top Bottom