Robert S Gulenga
JF-Expert Member
- Jan 3, 2013
- 2,160
- 1,492
Katika hali isiyo kuwa ya kawaida Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimetoa shutuma kali kwa Wanaharakati na Asasi/Mashirika ya kutetea haki za binadamu kuwa yamewatelekeza katika harakati zao.
Kwa muda tofauti, Viongozi wa Chadema wamekuwa wakilalamika kuwa Asasi na Mashirika ya kutetea haki za binadamu zimewatelekeza katika mapambano hayo, Catherine Ruge amesema mashirika haya yamekuwa yakipokea fedha za bure bila kutaja ni akina nani wanawapa.
Ushauri wa Bure kwa Chadema na Mwenyekiti Freeman Mbowe. Watanzania sasa wanataka Maendeleo, wanataka kusikia mkiwaunganisha Watanzania katika kuhakikisha Tanzania inasonga mbele, Watanzania na Wadau mbali mbali watawaunga mkono kama tu Mtakuwa wa kweli kusaidiana na Serikali kuhakikisha mnawaletea Watanzania Maendeleo
Mh. Rais anapambana kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora za Elimu, Afya, Maji, Serikali hailali kuhakikisha miradi yote inakamilika, Watanzania wako pamoja na Mh. Rais katika kuhakikisha tunafikia malengo tuliyojiwekea na si kila siku kufanya siasa za kufitinisha Wananachi na Serikali yao.
Mwezi wa Kumi na Mbili tukiwa tunaenda zetu Moshi tutapita kwenye daraja jipya la pale Wami litakuwa limekamilika kwa asilimia mia moja.
Kazi Iendelee
Mwenyezi Mungu ibariki Tanzania
Mwenyezi Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.