johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,897
- 141,830
Kitendo kile tu cha kuwapokea mawaziri wakuu wastaafu kujiunga na Chadema kilitosha kabisa kutoa taswira kwamba chama hicho kinaelekea kufani. Pamoja na ukweli kwamba watu hao " bado" ni watu wa serikali lakini hata ushawishi wao kwa umma ulishakwisha, hivyo uwepo wao Chadema ulikuwa ni wa manufaa ya muda mfupi. Wabunge wengi wa upinzani hasa Chadema walichaguliwa kwa mtindo wa " bendera fuata upepo" hivyo unahitajika upepo mdogo sana kuwarejesha walikotoka. Chukulia mfano, Lowassa, Mollel, Mwambe hawa walikuja Chadema baada ya kukatwa kule CCM na kilichowaleta ni maslahi ya kiuongozi na si chama hivyo wao kurudi CCM ni swala dogo sana. Nimalize kwa kusema chadema mmechelewa mno na hamna la kufanya tena, kinachotokea sasa ni kulipa deni mlilokopa huko CCM, ndio maana Dr Slaa aliwauliza huyu jamaa siyo " liability" kweli?!!....Hamkumuelewa. Ahsante!!