Mwana Mtoka Pabaya
JF-Expert Member
- Apr 22, 2012
- 15,118
- 16,470
Mkuu MMP, inaumiza sana kuona kuwa katika nchi hii kuna watu tena kwenye nafasi muhimu katika ofisi za umma ni waongo na wanafiki hata kuliko shetani. Binafsi sijawahi kuvutiwa na Lowassa kiasi hicho, lakini kama kweli watu wana hasira na ufisadi wanawezaje kuchukuliana na kuridhika na Mwakyembe aliyetamka kwa kinywa chake kuwa kamati yake ilificha mambo ili kuilinda serikali ya kikwete? Chenge je, yuko wapi?! Hawa wanaochukia hivyo ufisadi lakini wako kimya kuhusu Lugumi! Kivuko feki cha Dar-Bagamoyo?! Ufisadi woote uliofanyika nchi hii kwa nini wanakuwa kimya na kubaki kudanganya umma kuwa ufisadi uko upinzani?! Na hata kama uko huko kwa nini wasiwachukulie hatua za haki?!
Kuna kitu nimejifunza kutokana na siasa za wenzetu na historia ya Demokrasia huko ilikoanzia Ugiriki. Hatua za mwanzo za Demokrasia zilibeba utambuzi wa makundi ya watu kwa ubaguzi (huko Ugiriki) kiasi ungejiuliza dhana yenyewe ya Demokrasia iko wapi ikiwa watu wanabaguliwa.
Miongoni mwa Wagiriki wa kipindi hicho cha kina Plato, ukisema mtu ilimaanisha MWANAUME HURU. Wanawake na watumwa hawakuwa na nafasi za kimaamuzi na sababu ziliwekwa wazi. Mtumwa kwao alikuwa ni kifaa tu kama vilivyo vifaa vingine kama jembe, nyundo na toroli. Mtumwa hana haja ya kufikiri zaidi ya kufanya lile analoambiwa na bwana wake. Kwa maana hiyo, kumpa nafasi ya kuamua au kuchagua mtu wa namna hiyo ilifananishwa na kumpa mbuzi karatasi ya kura.
Wanawake nao (kwa kipindi hicho) hawakuwa sehemu ya uchangiaji wa maamuzi sababu hawakuwa responsible kwa yatukiayo kwa uchaguzi wao. Kwa mifano hii, nikiingiza Tanzania kwenye nafasi ya jamii ya Wagiriki ya wakati ule, naona tulipaswa kufika huko.
Tunapoenda kupiga kura (hapa Tanzania) makundi yote yana haki sawa ya kuchagua...kigezo pekee ni umri. Lakini ukiangalia nani anaathirika vipi na maamuzi yanayofanywa na kura hizi za jumla utagundua kuna wanaoathirika zaidi ya wengine kwa kuwa tunatofautiana malengo na matarajio. Mtu anayekatwa P.A.Y.E anajua uchungu wa kodi, leo hii chaguo lake lenye tija linashindwa kwa wingi wa kura za watu waliohongwa khanga na Tshs 2000 pamoja na disko kwenye kampeni na kumuwekea kiongozi kwa kuwa tu 'ni haki ya kila Mtanzania' kupiga kura.
Mimi nikirudisha kumbukumbu nyuma miaka michache, ninaona picha ya WATUMWA waliopewa haki ya kuchagua Rais. Kuna uchaguzi hapa, watu walichagua kiongozi kwa ushabiki 'presidaa sura babuu, tusiharibu noti', na kweli washabiki hao walifanya hivyo kwa hamasa kubwa. Unajiuliza, wafanyabiashara, na wawekezaji wanaotaka kulinda mitaji yao nao wangechagua sura? Ingekuwa tumegawanywa makundi kwa ufahamu wetu, hata mchaguliwa angekuwa na amani kuona kura zake zimetoka kwa watu wa aina gani?
Hapa kuna shida Mkuu. Kuna kundi kubwa la watu wasiojua wanafanya nini, wasio na kumbukumbu na wasiotaka kufikiri wanatumia haki yao kuchagua. Baada ya kuchagua, malalamiko kila uchao lakini uchaguzi ukija ndio wao wataalam wa kuimba mipasho na kumsifia mgawa tshirt. Kila ninapowafikiri hawa, huwa namkumbuka Mungu wangu...tumaini langu la mwisho!