Kweli jambo la muhimu ni elimu kutolewa kwa watu wengi kuhusu umuhimu wa katiba mpya!
ukweli ni kwamba hatutakiwi kuwa na uhakikika kama vili serikali ya ccm haijulikani kwa michezo yao ya hovyo hovyo.Iyo issue haitafanyiwa kazi wala nini,
kwa maslahi ya nchi watu woote tuungane kutengeneza katiba bila kujali chama na WABUNGE wasiangalie uvyama ni hatali hasa kwa wabunge wa ccm.na ukumbuke sasa baadhi ya vyama vya upinzani na baadhi ya wabunge na viongozi wa upinzani katika hatua hii wanaweza kununuliwa. Siyo kila mwanasiasa anayelilia katiba mpya ana nia ya dhati ya katiba mpya, bali wengine wanajua mchakato utawaletea mafao. umakini ni muhimu kwani siyo kweli kwamba madabiliko tunayoyataka ya katiba ni matamu kwa ccm na serikali. tunaweza kujikuta tunaendelea na mvinyo ule ule kwenye chupa mpya.
Michezo kama hiyo walifanikiwa tu kuhusu mgombea binafsi! Sasa hivi mambo yamekaa tenge, maana Katiba yenyewe inamtambua Waziri Kiongozi wa Zenj ambaye hayupo! Sasa kama hawatabadili Katiba hata kwa hilo wanahitaji kutimuliwa Ikulu "kwa njia nyingine!"
Haya, mhariri wa gazeti la uhuru la leo asema kuandika katiba mpya ni kazi ya serikali. Kwamba serikali imeshachukua jukumu lake, watu binafsi na vyama wasijipendekeze kutafuta mtaji wa kisiasa
Nadhani kuelimisha watanzania kuhusu katiba iliyopo na kasoro zake ndiyo iwe kazi ya vyama vya siasa vya upinzani kuwanzia sasa hivi. Tunategemea mengi zaidi kutoka kwa wale wenye ruzuku kubwa. Kwa kuwa chadema wamefanikiwa kulianzisha hili, hatua ilipofikia sasa wanatakiwa wajumuishe vyama vingine. kwenye hili sidhani kama vyama vya upinzani vitakuwa na maslahi yanayokinzana, labda baadhi waamue kuwa vibaraka wa ccm
Huyu ni mtu anayetumiwa, halafu yeye ni kama kasuku....kama ujuavyo kasuku yeye kazi yake ni kunakili kila kitu kama kilivyo hana uwezo wa kujua anafanya nini na ni kwa nini....yeye ndiyo alivyoumbwa. Sasa ni sawa na huyu muhariri..........unakuwa kibaraka mpaka unapoteza hata uwezo wako wa kufikiri na kuamua Shame...
kwa maslahi ya nchi watu woote tuungane kutengeneza katiba bila kujali chama na WABUNGE wasiangalie uvyama ni hatali hasa kwa wabunge wa ccm.
Haya, mhariri wa gazeti la uhuru la leo asema kuandika katiba mpya ni kazi ya serikali. Kwamba serikali imeshachukua jukumu lake, watu binafsi na vyama wasijipendekeze kutafuta mtaji wa kisiasa
Jamani madai ya katiba mpya hayana chama. Kila mtanzania mwenye kuipendea mema nchi hii anahitaji katiba mpya.
Hata hivyo lazima tukubali kuwa Chadema na cuf ni waanzilishi wa mjadala huu tangu wakati wa kampeni na ilikuwa ahadi yao katika manifesto zao. Hilo halipingiki.
na ukumbuke sasa baadhi ya vyama vya upinzani na baadhi ya wabunge na viongozi wa upinzani katika hatua hii wanaweza kununuliwa. Siyo kila mwanasiasa anayelilia katiba mpya ana nia ya dhati ya katiba mpya, bali wengine wanajua mchakato utawaletea mafao. umakini ni muhimu kwani siyo kweli kwamba madabiliko tunayoyataka ya katiba ni matamu kwa ccm na serikali. tunaweza kujikuta tunaendelea na mvinyo ule ule kwenye chupa mpya.
Kama mchezo wa karata vile. Nadra mchezo kukamilika kabla ya mizunguko kadhaa. Safari yao ni katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. mkakati wao wa kwanza ukawa kutokukubali ushindi wa JK, halafu kususia hotuba yake huku wakitoa wito wa madai yao. Yakasikika ndani na nje ya nchi, mijadala ikapamba moto.
Wameitwa majina, wamebezwa, wametengwa, na wamefitinishwa. Wakashindwa kuzima moto, na hatimaye ccm wakaona wakichelewa watashindwa kuja kusema wao ndio walioanzisha mjadala na mchakato. Ingawa walishakengeuka kupitia yule mama kilaza aliporopoka kwamba Tz haihitaji katiba mpya, wakaona bora wale matapishi yao mapema kweupe kupitia Waziri Mkuu. Hivyo guu lisijeota tende!
kwanini ni ushindi wa chadema hatua ya kwanza. huoni huo ni mtego? Kwamba rais atateua jopo ambalo litamshauri.