Chadema walamba Dume, Mzunguko wa Kwanza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema walamba Dume, Mzunguko wa Kwanza

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Gurudumu, Dec 17, 2010.

 1. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kama mchezo wa karata vile. Nadra mchezo kukamilika kabla ya mizunguko kadhaa. Safari yao ni katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. mkakati wao wa kwanza ukawa kutokukubali ushindi wa JK, halafu kususia hotuba yake huku wakitoa wito wa madai yao. Yakasikika ndani na nje ya nchi, mijadala ikapamba moto.

  Wameitwa majina, wamebezwa, wametengwa, na wamefitinishwa. Wakashindwa kuzima moto, na hatimaye ccm wakaona wakichelewa watashindwa kuja kusema wao ndio walioanzisha mjadala na mchakato. Ingawa walishakengeuka kupitia yule mama kilaza aliporopoka kwamba Tz haihitaji katiba mpya, wakaona bora wale matapishi yao mapema kweupe kupitia Waziri Mkuu. Hivyo guu lisijeota tende!

  kwanini ni ushindi wa chadema hatua ya kwanza. huoni huo ni mtego? Kwamba rais atateua jopo ambalo litamshauri.
   
 2. a

  awtu Member

  #2
  Dec 17, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :embarrassed:

  Hakuna cha dume kulambwa hapa. Hii ni geresha tu ya CCM.
  Wataunda tume, report itawasilishwa kwa rais kwa mbembwe,
  Naye JK atasema amewapa waalam kuifanyia kazi,
  alafu watasema muda hautoshi kubadili katiba nzima bali kuweka viraka vya hapa na pale
  Bunge la CCM watapiga kura kuipitisha 2014
  Mchezo kwisha!
  Au?
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  Dec 17, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Michezo kama hiyo walifanikiwa tu kuhusu mgombea binafsi! Sasa hivi mambo yamekaa tenge, maana Katiba yenyewe inamtambua Waziri Kiongozi wa Zenj ambaye hayupo! Sasa kama hawatabadili Katiba hata kwa hilo wanahitaji kutimuliwa Ikulu "kwa njia nyingine!"
   
 4. nginda

  nginda JF-Expert Member

  #4
  Dec 17, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 745
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inabidi cdm na uma kuongeza kuni moto uwake wa kutosha ili li-sisem liivie huko huko.
   
 5. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #5
  Dec 17, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Hakuna kitakacho simamisha hii TSUNAMI ya katiba Tanzania na tena it is spreading steadily in the whole African continent. Kiongozi yeyote muelewa na makini anatakiwa kufahamu hilo. African minds are changing and this change is nothing less its a Tsunami in the continent and its natural and it happens everywhere and in every developing society. Aristotle once wrote and warned in one of his books that "GOING AGAINST NATURE IS LIKE EATING SOUP WITH A SHARP KNIFE".
   
 6. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #6
  Dec 17, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Usisaha Alegory of the cave! Wanaodai katiba mpya hawajui kwa nini wanadai na hii tuliyonayo ina makosa gani
   
 7. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #7
  Dec 17, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,067
  Likes Received: 3,999
  Trophy Points: 280
  tuache tambo zisizo na manufaa ya mustakabali wa nchi yetu hapa suala ni hali ya nchi inahitaji katiba mpya na si suala la chama flani kimeanzisha hoja
   
 8. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #8
  Dec 17, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Pole mkuu, huwa inatokea
   
 9. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #9
  Dec 18, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Haya, mhariri wa gazeti la uhuru la leo asema kuandika katiba mpya ni kazi ya serikali. Kwamba serikali imeshachukua jukumu lake, watu binafsi na vyama wasijipendekeze kutafuta mtaji wa kisiasa
   
 10. Bams

  Bams JF-Expert Member

  #10
  Dec 18, 2010
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 3,592
  Likes Received: 2,976
  Trophy Points: 280
  Jambo kubwa kwa sasa siyo kuridhika kuwa jitihada za kuandika katiba mpya zimeanza bali ni kuzidi kujadili katiba tunayoitaka. Serikali na CCM waendelee na mambo yao lakini sisi wananchi kwa kupitia vyama vya siasa, taasisi mbalimbali na wananchi wote kwa ujumla tuendelee kujadili, kuelimishana, na kuunda kamati zetu zitakazoandaa mwongozo wa katiba tunayoitaka ili serikali itakapokuja na mwongozo wake tuweze kuangalia na kuona kama una mambo muhimu yote ambayo sisi wananchi tunayataka.

  Jukumu la kuandaa katiba ni la sisi wananchi na siyo la serikali. Serikali na taasisi zake isimamie process ya wananchi kuandaa katiba wanayoitaka na siyo wao watuandalie katiba sisi wananchi.
   
 11. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #11
  Dec 18, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  katiba inabidi iandikwe kwa matakwa ya watanzania siyo ya Kifisadifisadi.....walikuwa wapi kuandika zamani kwani kilio cha katiba mpya ilianza juzi?
   
 12. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #12
  Dec 18, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo ina maana sasa serikali imetoa ruksa kwa majukwaa yote ya kujadili katiba kuwa halali na wazi? nakumbuka Mwanakijiji alipoitisha mkutano huko kimara kujadili wazo la katiba mpya kuna watu wachache wakahofia kwenda kwa sababu za usalama wao. Ingawa watu waoga kwenye jamii yoyote hawakosekani.
   
 13. R

  Rafikikabisa JF-Expert Member

  #13
  Dec 18, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Suala la Katiba ni suala la Watanzania wote wapenda amani na maendeleo.

  Ni suala lisilo hitaji mzaa, ni suala lisilo taka visingizio vya aina yoyote.

  Hata awe Rais wa Tanzania wa sasa suala hili la katiba mpya ni suala muhimu kwa maisha yake ya baadaye (baada ya urais).

  Hata awe waziri, yes hivi ni watanzania wangapi wamekuwa mawaziri, makatibu wakuu, viongozi waandamizi serikalini, wakuu wa mikoa na wilaya, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama na sasa hivi wanaadhirika na katiba mbovu tuliyo nayo? katiba ya 47 hivi.

  Sasa hivi tunakumbana na changa moto mpya changa moto za utandawazi, changa moto za vijana wasio na ajira, changa moto za wazee, changa moto za kiutawala hatuna budi kuliona hili na kuangalia mbali na kuhakikisha ifikapo 2013 tayari Tanzania ina katiba mpya yenye kukidhi matarajio ya watanzania.

  Pamoja na kusifu Chadema kwa kuanzisha mjadala(hapa wanastahili pongezi) na kuwa chachu, lakini pia katika hili suala tuache ushabiki wa kisiasa, awe mwana Chama Cha Mapinduzi, mwana CUF, mwana TLP, mwana NCCR Mageuzi, mwana CHADEMA hili suala ni muhimu kwake na katika kuleta mstakabali wa taifa letu hapo baadaye tusilifanye la kiitikadi tukapoteza maana.

  Kuhusu mambo ya uchaguzi kilichotokea mwaka huu katika baadhi ya mikoa (Mwanza, Shinyanga, Mbeya, Arusha, Dar es salaam, tandahimba nk) viwe viashiria vya kutaka mabadiliko kabla ya 2015 vinginevyo tusikaribishe yale yanayotokea katika baadhi ya nchi, nchi yetu inasifika kwa amani na utulivu.

  Kumbukeni ni watanzania wachache sana au inawezekana wasiwepo wanaofaidika na katiba iliyopo sasa hivi. Haiwezekani pamoja na maendeleo yaliyotokea duniani tuendelee kuweka viraka katika katiba ya zamani, andikeni katiba upya inayokwenda na wakati yenye kuweza kumkomboa mtanzania kutoka katika wimbi la umasikini, tusiwaibie watanzania haki zao kwa visingizio vya kisiasa.
   
 14. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #14
  Dec 18, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Geza Ulole upo?
   
 15. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #15
  Dec 18, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,473
  Likes Received: 4,130
  Trophy Points: 280
  wengi hata hiyo katiba hawaifahamu.
   
 16. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #16
  Dec 18, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,473
  Likes Received: 4,130
  Trophy Points: 280
  Wameanza!
   
 17. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #17
  Dec 18, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0


  Heshima juu mkuu, sijakupata hapo kwenye rangi nyekundu.
   
 18. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #18
  Dec 18, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nadhani kuelimisha watanzania kuhusu katiba iliyopo na kasoro zake ndiyo iwe kazi ya vyama vya siasa vya upinzani kuwanzia sasa hivi. Tunategemea mengi zaidi kutoka kwa wale wenye ruzuku kubwa. Kwa kuwa chadema wamefanikiwa kulianzisha hili, hatua ilipofikia sasa wanatakiwa wajumuishe vyama vingine. kwenye hili sidhani kama vyama vya upinzani vitakuwa na maslahi yanayokinzana, labda baadhi waamue kuwa vibaraka wa ccm
   
 19. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #19
  Dec 18, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  ulitegemea nini? kumbuka hoja za ufisadi zilivyotekwa nyara na kupotoshwa? sasa hivi tumebakia kupiga domo tu kuhusu ufisadi wakati wenyewe wanapeta. Mwakembe?
   
 20. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #20
  Dec 18, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,473
  Likes Received: 4,130
  Trophy Points: 280
  Kweli jambo la muhimu ni elimu kutolewa kwa watu wengi kuhusu umuhimu wa katiba mpya!
   
Loading...