security guard
JF-Expert Member
- Sep 27, 2011
- 799
- 603
katika mkakati wake wa kukwamisha maendeleo ya wananchi na Taifa kwa Ujumla, inaripotiwa kuwa Madiwani wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya wamekwamisha ujenzi wa Chuo Kikuu Cha Mzumbe katika eneo la IWAMBI jijini Mbeya. Imedaiwa kuwa licha ya chuo hicho kulipa sh. bilioni moja kati ya mbili zinazotakiwa na Halamashauri ili kukipa ardhi ya kujenga chuo hiko, bado madiwani wa Chadema wamekuwa mstari wa mbele kupinga kuanza kwa ujenzi wa chuo hicho wakidai mpaka kimalize fedha yote iliyosalia. Meya wa Jiji la Mbeya Athanas Kapunga alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na wakazi wa Jiji hilo katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la soko Matola jijini hapa. Alisema mkoa wa Iringa unaongoza kwa kuwa na vyuo vikuu vingi, lakini Mbeya ina matawi ya vyuo vikuu huku kukiwa na vyuo vikuu kamili viwili ambavyo ni cha sayansi na teknolojia Mbeya (MUST) na kile cha Teofilo kisanji (TEKU) kwa mujibu wa Kapunga Mzumbe Kujenga Chuo kikuu eneo la Iwambi watakuwa wanazidi kuliboresha jiji hilo. Pia watasaidia kutoa ajira kwa wakazi wa jiji hilo na vitongoji vyake. Aidha alisema Halmashauri ya jiji itanufaika na ukusanyaji wa kodi ya majengo yatakayojengwa huku mamlaka ya Maji safi na Usafi wa mazingira jiji la Mbeya, Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Mbeya nao wataweza kuongeza wateja hivyo kuinua zaidi uchumi wa jiji hilo. Meya huyo alisema CHADEMA kupitia madiwani wao, wanakwamisha kuanza kwa ujenzi huo, kwa madai kuwa jiji linataka kutoa eneo bure kwa Chuo hicho ama kuwauzi akwa bei nafuu.