CHADEMA wakubali yaishe majimbo baada ya serikali tatu kukubalika katiba mpya

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,883
img2383.JPG

​


  • IDADI YA MAWAZIRI
Inapendekezwa Rais aunde Serikali ndogo iliyo na Mawaziri wasiozidi kumi na tano na mawaziri hao wasiwe wabunge. Mawaziri hawatahudhuria vikao vya Bunge isipokuwa kama watahitajika kutoa ufafanuzi kwenye kamati za Bunge.


  • BAADHI YA MAMBO AMBAYO HAYAMO KWENYE RASIMU YA KATIBA
    • Serikali ya Majimbo
Ndugu Wananchi,
Tume ilipokea maoni kuhusu mambo mengine muhimu ambayo hayamo katika rasimu hii. Moja ya mambo hayo niSerikali za Majimbo. Tume ilichambua maoni na sababu za wananchi kupendekeza Serikali za Majimbo lakini Tume ilibaini changamoto nyingi na ikaamua kutopendekeza muundo huu.

Kwanza, baada ya kuamua kupendekeza Muundo wa Muungano wa Serikali Tatu, ilionekana ni dhahiri kuongeza ngazi nyingine ya Serikali ingeleta gharama kubwa. Serikali nyingine kumi zingekuwa na Wakuu wa Majimbo, Mabaraza ya Mawaziri na Mabunge na gharama yake ingekuwa kubwa.

Pili, katika kutembelea nchi Tume ilishuhudia dalili za wazi za mivutano ya Udini, ukanda,malalamiko ya upendeleo wa baadhi ya maeneo na ukabila. Dalili zilikuwa wazi kwamba utawala wa majimbo ungeirudisha nchi kwenye utawala utakaoigawa nchi kwa misingi ya ukabila, udini na ukanda na kuzigawa rasilimali za taifa kikanda na hivyo kuleta tofauti kubwa ya kimaendeleo katika nchi.



  • TUME YA UCHAGUZI
Tume imefanya uchambuzi wa maoni ya wananchi kuhusu Tume ya Uchaguzi. Tume inapendekeza jina la tume liwe Tume Huru ya Uchaguzi. Tume pia inapendekeza sifa za wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi ziwekwe kwenye Katiba. Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi watapatikana kutoka miongoni mwa watu wenye sifa zilizoainishwa ndani ya Katiba kwa kuomba. Majina ya waombaji yatachambuliwa na Kamati ya Uteuzi ambayo Mwenyekiti wake atakuwa Jaji Mkuu na wajumbe wengine sita ambao ni Majaji Wakuu wa nchi Washirika, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Maspika wa Mabunge wa nchi Washirika na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu.

Kamati ya uteuzi itapendekeza majina ya watu wanaofaa kwa Rais ambaye atateua Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wengine. Bunge litathibitisha uteuzi wao. Wabunge na viongozi wa aina hiyo hawatakuwa na sifa za kuwa wajumbe wa tume ya uchaguzi.


  • MUUNDO WA MUUNGANO
Wananchi waliopendekeza muundo wa Serikali tatu walikuwa wengi kuliko makundi yote. Sababu zao zilikuwa nzito lakini pia kulikuwa na changamoto nyingi na nzito. Pamoja na maoni ya wananchi Tume ilirejea sababu za kupendekeza muundo huu zilizotolewa na Tume zilizopita na Tafiti zilizofanywa na Tume kuhusu aina mbalimbali za Muungano. Baada ya yote hayo Tume ilifikia uamuzi wa kupendekeza mfumo wa Serikali tatu. Yaani Serikali ya Shirikisho, Serikali ya Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.


  • ORODHA YA MAMBO YA MUUNGANO
Ndugu Wananchi,
Tume imependekeza katika Rasimu ya Katiba kuwa orodha ya Mambo ya Muungano yawe 7 badala ya 22 yaliyopo sasa.
Mambo ya muungano yanayopendekwa ni:


  1. Katiba na Mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  2. Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  3. Uraia na Uhamiaji
  4. Sarafu na Benki Kuu
  5. Mambo ya Nje
  6. Usajili wa Vyama vya Siasa
  7. Ushuru wa bidhaa na mapato yasiyo ya Kodi yatokanayo na Mambo ya Muungano.
 
Demokrasia ni pana, busara, uvumilivu na ustahimilivu ni muhimu kwa ajili ya umoja wa kitaifa. Pamoja na kila mmoja kuwa na maoni ya mtazamo binafsi licha ya mtazamo wa vyama vya siasa, taasisi, mashirika nk, hatimaye katiba inayopatikana haiwezi kumridhisha kila mmoja, ikitokea kumridhia kila mtu, kila taasisi, kila chama cha siasa dhahiri itakuwa na mapungufu makubwa maana itakuwa imeudhwa kuridhia kila mtu kitu ambacho kwa mwingine hakiungi mkono nk.

Kuna maoni kadhaa ya Chadema yanaonekana kukubalika katika rasimu ya katiba mpya, ingawa kuna ile ya serikali ya majimbo inaonekana kugonga mwamba. Busara kuwa tayari kupokea ambayo yanaonekana kukubalika na wengi maana muundo wa serikali tatu utaondoa kero kadhaa ambazo zilikuwa zinaielemea serikali mbili ya Muungano na ile ya Zanzibar.
 
Serikali za majimbo ndio jibu mwafaka wa kufuta ufisadi wa wanasiasa wa CCM unaofanywa kwa njia ya centralization of power. Bado tawala za majimbo itakuwa ni mojawapo ya ilani ya Uchaguzi ya CDM mwaka 2015, ilani itakayokuwa mwiba mkuu kwa mafisadi!!!!
 
"Serikali za MAjimbo zitaongeza Gharama!?!!"
but hapohapo tuna wakuu wa mikoa wenye mlolongo wa wakurugenzi, huku tukipendekeza serikali tatu badala ya mbili.

Aibu iliyoje!!!
 
tunaelekea pazuri,katiba ni ya watu na watu ndio wakusikilizwa wanataka nini japo km ulivyosema haiwezi kumridhisha kila mtu ila naamini inaweza kuwridhisha walio wengi na hilo ndio muhimu
 
Bunge la CCM hawawezi ipitisha rasimu hii iwe katiba!
Vipengele vilivyonifurahisha:
Serikali 3
Mawaziri wasizidi 15 na wasiwe wabunge
Wakuu wa Wilaya wajadiliwe kwenye serikali ya Zanzibar na ya Tanganyika
Deni la Taifa sasa liwe ndani ya katiba
KILICHO NIHUZUNISHA:
Rasimu haija dhibiti safari za Rais maana JK anachokifanya anaweza akaja Rais mwingine akaiga haya mambo;Safari karibia 400 nje ya nchi ndani ya miaka 8 ni mzigo sana kwa tax payers!
 
CCM hawawezi kukubali wananchi wenyewe wasimamie raslimali zao. Wanataka mapato yote yaendelee kupelekwa Dar es salaam ili yawanufaishe wao na familia zao. Wanatoa visingizio kwamba: "Suala hilo litatugawa". Ajabu na kweli! Wananchi kusimamia raslimali ni marufuku kwa kuwa watagawanyika!!! Sijui iwapo watanzania wana mang'amuzi ya kutosha kwa jambo hili.
 
Nawashauri CDM wala wasihangaike tena na Serikali ya Shirikisho (Muungano) bali sasa wajikite zaidi katika Serikali ya Tanganyika!!! Huo ndio mwisho wa muungano fake na kifo cha CCM!!!!!!!!!!!!!!
 
Bunge la CCM hawawezi ipitisha rasimu hii iwe katiba!
Vipengele vilivyonifurahisha:
Serikali 3
Mawaziri wasizidi 15 na wasiwe wabunge
Wakuu wa Wilaya wajadiliwe kwenye serikali ya Zanzibar na ya Tanganyika
Deni la Taifa sasa liwe ndani ya katiba
KILICHO NIHUZUNISHA:
Rasimu haija dhibiti safari za Rais maana JK anachokifanya anaweza akaja Rais mwingine akaiga haya mambo;Safari karibia 400 nje ya nchi ndani ya miaka 8 ni mzigo sana kwa tax payers!

Kuna mengi katika rasimu hii ya katiba yanayotia moyo mojawapo ni kwamba:
Mchakacho wa kupata tume ya uchaguzi, hali kadhalika tume hiyo iwe ndiyo yenye mamlaka katika usajili wa vyama vya siasa badala ya Tendwa ambayo ame-hang mahali pasipoeleweka.
 
Upande wa madaraka ya rais hayajadhibitiwa ipasavyo, pia suala la presidential debate ni muhimu ingawa sijaliona! Labda tuzingatie kwenye katiba ya tanganyika!
 
Mkuu Tanzania si nchi ya Bunge la CCM bali ni nchi ya Watanzania. Kama Watanzania tutakuwa makini basi wakigoma kuipitisha hii rasimu basi kwenye kura ya maoni kama katiba mpya ikubaliwe au la basi katiba hiyo ambayo CCM wataitaka ili kutimiza lengo lao la "kuitawala Tanzania milele" ipigwe chini.

Bunge la CCM hawawezi ipitisha rasimu hii iwe katiba!
Vipengele vilivyonifurahisha:
Serikali 3
Mawaziri wasizidi 15 na wasiwe wabunge
Wakuu wa Wilaya wajadiliwe kwenye serikali ya Zanzibar na ya Tanganyika
Deni la Taifa sasa liwe ndani ya katiba
KILICHO NIHUZUNISHA:
Rasimu haija dhibiti safari za Rais maana JK anachokifanya anaweza akaja Rais mwingine akaiga haya mambo;Safari karibia 400 nje ya nchi ndani ya miaka 8 ni mzigo sana kwa tax payers!
 
Inapendeza kuhusu tume ya uchaguzi. Hope it will change things round.

Katika hiyo ya mawaziri, wangepewa contracts renewable za miaka 2 na performance appraisal system!
 
Maoni ya tume juu ya serikali ya majimbo ni DHAIFU na ya WOGA! GHARAMA wanazosema za uendeshaji hazilingani na gharama za mikoa na wilaya!
 
why Tanzania Bara na sio Tanganyika?

Nimeona kwenye rasimu hiyo imependekezwa jina Tanzania liendelee kutimika hata kwa serikali tatu ya Jamhuri ya Muungano, ya Bara na ya Visiwani. Sijaona kuna ubaya maana tukianza kubadili jina na kuweka la Tanganyika mambo mengi yatafutata ambayo pendine kutugharibu kiuchumi na kimahusiano kimataifa, na kama inabaki kama ilivyopendekezwa na kuzoeleka sijaona athari yake kwa jamii na taifa.
 
Ina maana kwa mfumo wa serikali tatu, bara tutakuwa na rais wa bara, bendera, katiba na wimbo wa taifa? kama sivyo bas bado ni tatizo.

Pili tuendelee kukomaa kinga ya rais iondolewe, hii kinga ni kwa misingi ipi? maana katiba hiyohiyo inasema hakuna aliejuu ya sheria , sasa hii kinga si kumweka juu rais?

tatu nado rais ana madaraka makubwa kweli, yan kumruhusu jaji kuteuliwa na rais ingawa atapendekezewa, bado jaji atawajibika kwa aliemchagua.

yatizo lingine kama la hapo juu ni kwa tume ya uchaguzi, et rais bado anapewa uwezo wakumchagua mwenyekiti wa tume baada ua kupendekezewa, japo atathibitishwa hapa bado, huyu atawajibika kwa rais.
 
"Serikali za MAjimbo zitaongeza Gharama!?!!"
but hapohapo tuna wakuu wa mikoa wenye mlolongo wa wakurugenzi, huku tukipendekeza serikali tatu badala ya mbili.

Aibu iliyoje!!!
serikari ya majimbo wanaikwepa tu kwa kisingizio na hoja nyepesi lakini Utawala wa Majimbo ni wa Gharama nafuu zaidi ya serikari tatu endapo watazingatia Majimbo mawili
 
Maoni ya tume juu ya serikali ya majimbo ni DHAIFU na ya WOGA! GHARAMA wanazosema za uendeshaji hazilingani na gharama za mikoa na wilaya!

Kuna baadhi ya mambo ni bora kuyasitisha inapotokea kutotoa mwanga wa moja kwa moja. Pengine hayo wanaopigia filimbi wakishakuwa na nguvu za kuongoza serikali inawezekana kuwa na amendments kitu ambacho hakibadili katiba. Kuna maengi ambayo yamependekezwa kuwa yawe sheria za kawaida badala ya kuyaweka katika katiba.
 
Ina maana kwa mfumo wa serikali tatu, bara tutakuwa na rais wa bara, bendera, katiba na wimbo wa taifa? kama sivyo bas bado ni tatizo.

Pili tuendelee kukomaa kinga ya rais iondolewe, hii kinga ni kwa misingi ipi? maana katiba hiyohiyo inasema hakuna aliejuu ya sheria , sasa hii kinga si kumweka juu rais?

tatu nado rais ana madaraka makubwa kweli, yan kumruhusu jaji kuteuliwa na rais ingawa atapendekezewa, bado jaji atawajibika kwa aliemchagua.

yatizo lingine kama la hapo juu ni kwa tume ya uchaguzi, et rais bado anapewa uwezo wakumchagua mwenyekiti wa tume baada ua kupendekezewa, japo atathibitishwa hapa bado, huyu atawajibika kwa rais.

Serikali tatu jibu lake bara tutakuwa na rais wetu, visiwani rais wao na kutakukwa na rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye atakuwa juu ya yale mapendekezo saba yaliyotokezwa. Mengine yanawahusu marais wa serikali ya bara na ya visiwani.
 
Back
Top Bottom