Chadema wakishinda Urais 2015 ina maana wakuu wa Wilaya na Mikoa, wote kubadilishwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema wakishinda Urais 2015 ina maana wakuu wa Wilaya na Mikoa, wote kubadilishwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Synthesizer, Aug 16, 2012.

 1. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Wakuu wa mikoa na wilaya kutokuwa sehemu ya siasa ni jambo ambalo limepigiwa sana kelele na upinzani, na CCM kulizibia masikio. Hii ina maana Chadema wakishinda uraisi 2015, itabidi wabadilishe wakuu wote wa wilaya na mikoa kwa mpigo!

  Tukiweka ushabiki wa kichama pembeni, nadhani hili ni suala linalopaswa kuangaliwa kwa umakini katika mabadiliko ya katiba. Huenda hata ni vema kutokuwa na nafasi za wakuu wa wilaya na mikoa bali wakurugenzi ambao hawapaswi kuwa na mfungo wa kisiasa. Wakuu wa wilaya na mikoa hawana lolote la maana wanalochangia zaidi ya propaganda, na mara nyingi kuwa kikwazo kwa wakurugenzi wa wilaya na mkoa.
   
 2. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Aiseee baba yangu ni kweli kabisa unachosema hawa wakina mek sadiki hawana lolote kwanza ndio wanachochea ongezeko la garama ndani ya serekali,,wanatembelea ma vx si bora wafutwe 2

  ngoja niagize mbege
   
 3. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #3
  Aug 16, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  wakuu wa wilaya wa nini? wakuu wa mikoa wanatosha na madiwani...wapigwe chini wote...cdm nina uhakika itatafuta kila jinsi kusave hela za walipa kodi kwenye gharama kama za wakuu wa wilaya hizo hela zitumike kuboresha huduma na kulipa wafanya kazi mishahara mizuri
   
 4. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #4
  Aug 16, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kusema ukweli wakuu wa wilaya na mikoa ni mzigo.

  Tungeamua kuwa na mwakilishi mmoja kanda ya kaskazini ambaye atafanya mambo yote ya kiserekali , mmoja kusini,mmoja mashariki mwengine magharibi baasi. Hawa wawe na mamlaka mazito ya kuhakikisha harakati za serikali zinafanikiwa. Na wenyewe wana m brief Mr President mara kwa mara ajue kinachoendelea kwenye maeneo yao.

  Tatizo wale makada wa CCM waliojazana watakula wapi?:happy:
   
 5. KIJOME

  KIJOME JF-Expert Member

  #5
  Aug 16, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 3,079
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Tena watafute pa kukimbilia...hawana lolote zaidi ya kutuongezea gharama za bure tu,wengi wao ni vimada wa magamba.
   
 6. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #6
  Aug 16, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,382
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Leo Mh Wenje alimuuliza Waziri mkuu khuhusu mkuu wa wilaya ya Nyamagana kuhutubia kwenye mkutano wa ccm akiwa amevalia shati zao za kijani na ksema "Mimi nimeletwa hapa Nyamagana na Rais ili kukilinda chama cha mapinduzi". Sasa undhani CDM ikiingia madarakani hawa ni watu wakuachwa madarakani?

  Hata hivyo sera ya CDM nikupunguza ukubwa wa serikali na hivyo kuendeleza sera ya majimbo, viongozi watakaochaguliwa moja kwa moja na raia na sio wateule wa rais. Kwa hakika hao wakuu wawilaya na mikoa siku zao zinahesabika.
   
 7. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #7
  Aug 16, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,852
  Likes Received: 493
  Trophy Points: 180
  Kwani Mkuu wa Mkoa Kazi yake ni nini hasa? Si Kumpokea rais wa nchi Mkoani kwake na kuupokea mwenge Mkoani kwake? Au Kuna Jingine Tujuzane Wana jamvi!! Ila home-works Jingine ni kupanga namna ya Kuukandamiza Upinzani (Vyama / Individuals) Kama tulivyoona hivi karibuni Mtu ananyima Kulala kwenye Nyumba ya wageni Ndani ya Nchi yake!!
   
 8. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #8
  Aug 16, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,852
  Likes Received: 493
  Trophy Points: 180
  Hawa ni wenyeviti wa Wilaya wa Chama with Government Pay!! Mark Pinda's word!!
   
 9. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #9
  Aug 16, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  hivi kumbe kuna wakati akili zako zinakuwa positive eee naona m4c IMEKUINGIA AKILINI WE NEED FEW PEOPLE TO UTILIZE THEM AND PAY THEM IN GRANT.Kwa mara ya pili nakugongea 'LIKE"
   
 10. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #10
  Aug 16, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Haya mengine mambo ya msingi na yapo wazi hayahitaji ushabiki wa siasa.
   
 11. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #11
  Aug 16, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,847
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Siyo kubadilihswa kwa wakuu wa wilaya na mikoa tu , bali hata kupunguza baadhi ya mikoa iliyokatwa kisiasa kwa mfano,KATAVI, SIMIYU, NJOMBE, GEITA.
   
 12. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #12
  Aug 16, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mkuu nakurekebisha sio watabadilishwa ila WATAPIGWA CHINI hawana kazi yoyote hawa! Tutaokoa mamilioni ya fedha za walipa kodi
   
 13. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #13
  Aug 16, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280

  Sawa Mkuu Ernesto Che, nakubaliana nawe kabisa. Ila sijajua kama wakuu wa wilaya na mikoa ni suala la kikatiba. Hivi hizi nafasi ni kwa mujibu wa katiba au ni jambo ambalo TANU na ASP waliamua? Kama sio suala la kikatiba tutakuwa na hali kwamba kila chama kinachoshinda uraisi na kushika serikali kinawarudisha au kuwaondoa. Inabidi kutokuwapo kwao liwe jambo la kikatiba.
   
 14. k

  kijereshi JF-Expert Member

  #14
  Aug 16, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 257
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Binafsi nadhani sio vibaya kuwa na hivyo vyeo ni vile tu hao wenye dhamana navyo wanavitumia vibaya na kuvifanya vionekane kama ni vya kisiasa au labda kutokana na mashinikizo ya aliyewateua,lakini kama kweli wangekuwa na dhamira ya dhati kutumikia kazi zao wako na nafasi kubwa sana kuchangia kuendeleza jamii wanazoziongoza mfano hawa wanaweza wakawa ni waibuaji wa miradi mbalimbali ya mendeleo na kuweza kutoa fursa kwa vijana kujiajiri na kujipatia kipato katika maeneo yao kuliko kukaa na kuanza kufanya shughuli za kisiasa wakati wanawaongoza watu wa vyama mbalimbali.Nadhani wa wakati wa kuwa na viongozi wenye mawazo ya kijasiliamali zaidi ili kuweza kusukuma gurudumu la maendeleo kuliko kuwa na viongozi mara zote ni siasa zisizo na malengo zaidi ya kutawala.
   
 15. brazilian

  brazilian JF-Expert Member

  #15
  Aug 16, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 607
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wasiwepo kabisa maana wanakula mshahara wa bure kabisa. Labda tuwachague kwa kura ili wananchi waweze kuwawajibisha
   
 16. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #16
  Aug 16, 2012
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Si tu CDM ikishinda, Hata kwenye katiba mpya hao watu wasiwepo wanakula hela ya serikali kwa kazi ya Chama! Kazi zenyewe wanapeana kishikaji. Stella Manyanya, Ishingoma wamekaa bungeni muda wote wa budget, Iringa na Rukwa kazi zinaenda kama kawa. Hiyo ni ishara kuwa hawana mchango wowote kwenye Mikoa hiyo.
   
 17. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #17
  Aug 16, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  CDM wakishinda urais nchi itaingia kwenye roller coaster...
   
 18. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #18
  Aug 16, 2012
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,276
  Trophy Points: 280
  Kuna post moja niliongelea hili wazo ni nyuma sana.

  Wakuu wa mikoa na wale wa wilaya waondolewe na nafasi zao zitajazwa na mameya wa miji na madiwani.

  Kwa kupata maendeleo ya haraka na uboreshwaji wa ukusanyaji wa mapato na matumizi, mameya wa miji na madiwani itabidi wachaguliwe na wananchi kwa kura.

  Halafu mameya watatafuta maofisa watendaji wakuu wenye sifa za utendaji na uchapaji kazi kwenye manispaa na miji hiyo kusimamia maendeleo.
   
 19. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #19
  Aug 16, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kwani hawa wa nini, tutawapeleka kufundisha shule za kata na msingi na kazi nyingine zinazowafaa. Wenyeviti wa wilaya na mikoa wanatosha, Ni ubadhirifu tu. Huu ulikuwa mfumo wa bwana DC na Gavana wao.
   
 20. M

  Masayi77 Member

  #20
  Aug 16, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu wa wilaya na mikoa hawapaswi kuwepo, sababu wanamwakilisha rais kichama zaidi wakati kuna wenyeviti wa mikoa wa chama huku ni kufuja rasilimali zetu.
   
Loading...