Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Nimesikia miruzi eti CHADEMA wanachukua jukumu la kulisha wenye njaa Tanzania nzima. Kwa hakika nimeupenda sana huu msimamo na kama utatekelezwa naamini kuwa CHADEMA watakuwa wamebadilika kutoka kikundi cha harakati hadi chama cha siasa.
Hata hivyo, najitokeza kifua mbele kuwaambia Watanzania kuwa CHADEMA hawatanunua hata gunia moja la Mahindi. Hali ya mwenyekiti Mbowe kifedha si nzuri na kwa kawaida si utamaduni wa CHADEMA kuwasaidia wenye shida. Hii walikuwa wanatafuta kick tu baada ya Rais Magufuli kawafunika katika kila eneo. Naahidi kuwa ikiwa CHADEMA watajitwisha jukumu la kulisha wenye njaa, nitaacha rasmi kuishabikia CCM na nitaungana nao kwenye harakati zao za kisiasa.