Chadema wakimpendekeza Dr Slaa tume ya katiba, Jk atamteua au atamtosa? Usalama wake vipi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema wakimpendekeza Dr Slaa tume ya katiba, Jk atamteua au atamtosa? Usalama wake vipi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gurti, Mar 6, 2012.

 1. G

  Gurti JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa kuwa Dr Slaa ni mwanasheria na ndo aliyepeperusha bendera ya Chadema 2010 akinadi kuwa mchakato wa katiba mpya utaanza ndani ya siku chache baada ya kuingia madarakani. Napendekeza Dr Slaa apendekezwe na Chadema kuingia ktk tume hiyo mpya ya katiba.

  Hata hivyo, sina hakika kama JK atataka Dr Slaa awepo katika tume hiyo kwa kuwa anajua kuwa ana msimamo mkali.
  Lakini je, Dr Slaa akiteuliwa si yatamkuta yale ya Mwakyembe? CCM wakiona katiba mpya imemzuia uchakachuaji wa kura nahisi watataka kabla ya mwaka 2010 Dr Slaa asiwepo duniani. Maana ngoma itakuwa nzito zaidi. au?

  Wengine ambao uwepo wao utakuwa na tija ni Prof Abdallah Safari, Prof Baregu, Wakili Mabere Marando.

  Nawasilisha.
  Naomba maoni yenu.
   
 2. G

  Gurti JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mods naombeni muiache hii thread kwa at least siku moja, pamoja na kuwa kuna thread inayozungumzia nani awepo ktk wajumbe hao. Tuijadili kipekee nafasi ya Dr Slaa kwa namna tofauti kidogo.
   
 3. kadoda11

  kadoda11 JF-Expert Member

  #3
  Mar 6, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 16,215
  Likes Received: 8,278
  Trophy Points: 280
  ...ngoja wahusika waje nione msimamo wao.
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  Mar 6, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Mkuu una hofu na uwepo wa thread yako?

  Mkuu tume haitakuwa ya wanasheria tu! Tunataka akina Sugu, Chiku Abwao na mchanganyiko mwingine.

  Umempendekeza Dr. halafu unasema usalama wake mbona mambo mengi kwa mpigo? Karibu
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Mar 6, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ebu tuonmyeshe hiyo namna ya pekee ambayo unataka tumjadili Dr Slaa/ La sivyo, usiwanung'unikie mods wiapo wataiunganisha thread yako hii na ile nyingine
   
 6. n

  ngilenengo1 JF-Expert Member

  #6
  Mar 6, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 933
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  Dr. Slaa asiwepo kwenye kamati, CDM impeleke mtu mwingine yeyote makini. Najua wanao wengi tu!
   
 7. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #7
  Mar 6, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Chadema wakipeleka jina la Slaa anaweza kupitishwa sioni tatizo.
   
 8. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #8
  Mar 6, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,457
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Asiwemo aendelee na kazi ya kuimarisha chama. Tundu Lissu apeleke utundu wake wa kisheria akiwa na Prof Safari
   
 9. Mtoto Wa Mbale

  Mtoto Wa Mbale JF-Expert Member

  #9
  Mar 6, 2012
  Joined: May 15, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kama kuna kosa kubwa la kiufundi CDM wanaweza kufanya ni kumpendekeza Dr. Slaa kwenye hiyo tume. Baada ya madudu ya tume, kwani siamini kama zoezi hili halitachakachuliwa na ikulu, utakuwa mwisho wa nguvu zake kisiasa. Ni bora wampendekeze mtu tofauti na Slaa, mwenye uwezo wa kusimamia hoja makini bila woga.
   
 10. A

  Anne deo JF-Expert Member

  #10
  Mar 6, 2012
  Joined: Jul 10, 2011
  Messages: 470
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Tukumbuke kuwa dr slaa ni mtendaji mkuu wa chama,ni sawa anaweza ila tuepuke kumlimbikizia mambo mengi...cdm wapo watu wengi makini kama tindu lissu,mabere marando,halima mdee nk,kuhusu usalama ni Mungu pekee anamlinda.mbona kwenye ripot ya mwanzo kabisa ya mwakyembe dr alitajwa kuwa anawindwa pia??
   
 11. tindo

  tindo JF-Expert Member

  #11
  Mar 6, 2012
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 9,967
  Likes Received: 10,130
  Trophy Points: 280
  Hata mimi sishauri Dr. Slaa awepo kwani itaonekana amelazimisha kuwepo, wao Chadema waweke watu wengine makini tu. Ili Dr.Slaa kama atateuliwa kugombea urais na chama chake huko mbeleni asionekana ni mmoja wa walioratibu mchakato huo wa katiba na hasa kama maoni yatachakachuliwa ambapo mazingira hayo ni makubwa.
   
 12. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #12
  Mar 6, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kila nikijaribu kuisoma hii thread naona kama ina matege matege hivi. Usalama wa dr Siaa unahusiana vipi na uwepo wake kwenye hiyo tume? Kwani hivi sasa anatembelea angani au.
   
 13. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #13
  Mar 6, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mimi ninachojua ni kuwa slaa ni padre. hili lasheria ndo kwanza nalisikia kwako
   
 14. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #14
  Mar 6, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Achilia mbali wingi wao, technically haitakiwi kabisa DR kuingia kwenye mchakato huu functionally, tunaamini anauwezo mkubwa sana wa kusimamia mambo ya namna hii ila itifaki hairuhusu, DR SLAA haitakiwi areport kwa Jakaya by any means, ni bora akadhalilishwe na polisi uko vituoni kwao kuliko kuwa kwenye situation yoyote ambayo kimantiki Jakaya kashika Mpini na DR Kashika makali. Jakaya will finish him out right.

  By the way, hata sasa ana nguvu ya kumould hiyo katiba anavyotaka
   
 15. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #15
  Mar 6, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Hata mapadri unauonaje uwezo wao wa kisheria ukiwapima na maulamaa
   
 16. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #16
  Mar 6, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Sangarara nini tena? Maulamaa wametoka wapi tena? Jamaa kasema tu kwamba Dr. ni padre la kisheria hajalisikia. Ungemwambia tu kwamba Dr. ana PhD ya sheria katika dini badala ya kuunganisha na mambo ya maulamaa.
   
Loading...