Chadema wajisumbua kwa nini wasidae Tanganyika na katiba yake? Hamadi R ana nchi yao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema wajisumbua kwa nini wasidae Tanganyika na katiba yake? Hamadi R ana nchi yao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Feb 10, 2011.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kafulila, Hamad waipiga vijembe Chadema Send to a friend Wednesday, 09 February 2011 22:08

  [​IMG]Hamad Rashid

  Mwandishi Wetu, Dodoma

  MBUNGE wa Kigoma Kusini, David Kafulila(NCCR) na Hamad Rashid wa Wawi(CUF) jana waliipiga vijembe Chadema wakieleza kuwa matokeo ya uchaguzi wa wenyeviti wa Kamati za Bunge yameonyesha chama hicho kutokuwa wakweli.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya uchaguzi wa wenyeviti hao jana, wabunge hao walisema kuwa matokeo ya uchaguzi huo yameonyesha nia njema waliyokuwa nayo kwa kutaka marekebisho ya tafsiri ya maneno Kambi Rasmi ya Upinzani katika kanuni za Bunge. "Labda niseme kwa ufupi, matokeo ya uchaguzi wa wenyeviti wa Kamati za Bunge nimeyapokea vizuri hasa kamati zile tatu zinazoitwa 'Watch Dog' ambazo hushikwa na wapinzani," alisema Kafulila.

  Vita ya maneno baina ya CUF na NCCR Mageuzi kwa upande mmoja dhidi ya Chadema kwa upande mwingine ilionekana dhahiri kuhamia bungeni kufuatia Chadema kuonyesha msimamo wa kutotaka ushirika na vyama vingine kwenye kambi yake ya upinzani, baada ya wabunge wa vyama hivyo kupeana mipasho katika kikao cha kwanza cha mkutano wa bunge la kumi unaoendelea mjini Dodoma.

  Hoja hiyo juzi ilifanya mkutano wa bunge la kumi kuanza kwa moto pale Naibu Spika, Job Ndugai alipowasilisha azimio linalotoa tafsiri ya nini maana ya ‘Kambi rasmi ya upinzani Bungeni’ na baadaye azimio hilo kupitishwa na bunge hali ambayo ilitafsiriwa kuwa ni mkakati wa “kuivunja nguvu za kisheria Chadema”.

  Jana Kafulila alisema juzi wakati wa mjadala wa azimio la Bunge kuhusu marekebisho ya tafsiri ya kanuni ya Bunge kuhusu maneno Kambi Rasmi ya Upinzani, wabunge wa Chadema walionyesha kuwa yeye Kafulila na Hamad Rashid walitaka nafasi za uenyekiti wa kamati hizo.

  Alisema tofauti na mawazo hayo ya Chadema, matokeo yamekuwa tofauti na kuchukuliwa na Chadema yenyewe, UDP na TLP akiongeza kuwa hiyo ni salamu kwa Chadema. Alifafanua kuwa kwa matokeo hayo Chadema inapaswa kufahamu kuwa wao walitaka mabadiliko hayo kwa faida ya wabunge wote na si vyama vya NCCR na CUF kama Chadema walivyodhani.

  "Hiyo ni salamu kwa Chadema, wajue kwamba sisi tulitaka mabadiliko kwa ajili na faida ya vyama vyote, umeona hata nafasi hizo zimekwenda kwa vyama vya UPD, TLP na Chadema yenyewe," alisema Kafulila. Hamad Rashid kwa upande wake alisema kuwa matokeo ya uchaguzi huo yamemfurahisha na kwamba yametokana na kazi waliyoifanya juzi kurekebisha kanuni za Bunge na kuwezesha Mrema wa TLP na Cheyo wa UDP kuchaguliwa uenyeviti wa kamati.

  "Nimefurahi kazi yetu ya jana (juzi) imesaidia Mrema na Cheyo wamepata uenyekiti wa kamati zinazotakiwa kuongozwa na wabunge wa upinzani," alisema Hamad. Aliongeza:" Kelele zetu zilikuwa kuweka msingi ya demokrasia ambayo imetendeka, lakini dhana walizokuwa nazo wenzetu Chadema hazikuwa sahihi.
  Kilichofanyika ni demokrasia." Alisema kuwa kimsingi kila mbunge alishiriki uchaguzi huo na kwamba waliochaguliwa wamechaguliwa kadri ya matakwa yao, kwa kuwa ndiyo demokrasia na kwamba kilichobaki ni kuwapa ushirikiano na kujiamini.

  Alieleza kuwa hakuna haja kuwa na hofu na uongozi wa wenyeviti hao kwa kuwa wanaongozwa na taratibu na kanuni za bunge zilizopo ambapo zinamlinda kila mmoja.
  Injinia Stella Manyanya, alisema kuwa viongozi wa kamati hizo wamepatikana kwa ridhaa ya wabunge na kwamba wamechagua kwa busara. "Huu ulikuwa uchaguzi wa wabunge wenyewe, ndio wenye ridhaa, wamechagua kwa busara," alisema ambaye pia amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda na Biashara.
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Wazanzibar
  1.tunaburuzwa kwenye muungano
  2.Tunachaguliwa rais wa zanzibar (kimkakati kwani CCM inawapitishia wagombea urais)
  3. Dai jipya: TUMECHEZEWA RAFU MATOKEO YA FORM FOUR 2010 (wanataka baraza lao la mitihani)na malalamiko kibao.TUJITOE KWENYE MUUNGANO

  BARA:tudumishe muungano jamani na misemo kibao ya Mwalimu.

  My take:Tuwaachie zanzibar yao waone watafika wapi na siasa zao zisizo na hoja wala mashiko bali visasi vya kihistoria mara HANGA,ushiriki wa SEIF kumdhalilisha JUMBE,sijui mara Sultan alifanyaje yaan ajabu bin ajabu.

  Vijana wa BARA tunataka siasaleo (sio siasahistoria ya CUF+-CCM)inayochipua hoja bila woga kwa maslahi ya taifa.Tumeingia kwenye ulingo mwingine wa kuikomboa nchi kutoka kwa Mafisadi.
   
 3. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #3
  Feb 10, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Hamad Rashid anachoshindwa kujua ni kwamba anaizika CUF huku bara, mm nam-support aendelee izika. Na kwa taarifa yake hizo siasa sasa hv zinahamia mtaaani ambako neither CUF, NCCR nor CCM wanzweza mshinda CDM.
   
 4. doup

  doup JF-Expert Member

  #4
  Feb 10, 2011
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  anategemea nguvu ya wapemba waliojaa temeke
   
Loading...