CHADEMA wajipange upya kama kweli wabunge wanawake 20 wenye nguvu ndani ya chama wamenunuliwa na CCM kwa mpigo

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
27,443
2,000
CHADEMA BAWACHA ndio ilibaki nguzo pekee ya CHADEMA ya kuaminiwa.

CHADEMA walilisifu sana BAWACHA kuwa eti wabunge na madiwani wote eti kwa kile kinachoitwa kununuliwa wabunge na madiwani walikuwa ni wanaume tu wanawake wa BAWACHA hawakukubali.

Msimamo huo ulisababisha wabunge wanawake wawekwe wengi kwenye majimbo kuliko wanaume na ikapata baraka ya kamati kuu ikituhumu kuwa mianaume mingi inauzika inafika bei!

Sasa hilo limetokea yuko mbunge Aida KHATAN na wabunge viti maalumu 19 wote kwa mpigo wameingia.

CHADEMA wengine wanasema wamenunuliwa wengine wanasema hao wabunge wote 20 ni maafisa kipenyo wa serikali waliokuwa ndani ya CHADEMA!

Ina maana kwa sasa CHADEMA haitawaamini wanawake wala wanaume kwa kuwatuhumu kuwa wananunulika au ni maafisa kipenyo wa serikali!

Kwa muktadha huo CHADEMA sasa hivi wanatakiwa kwenda retreat kujipanga upya kisiasa badala ya kupigia mikelele CCM!
 
chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
3,149
2,000
Ukweli mchungu sasa kuna chadema la saba B,chadema ya ubeligiji,chadema mitandao,chadema kilakala,chadema ya kaskazini.
Hata shetani alitoka mbinguni hata mbinguni kulikuwa na mabadiliko na kukubali makosa
Wasipo tambua hilo
 
TsafuRD

JF-Expert Member
Sep 29, 2013
1,920
2,000
Suala ni njaa ya hawa wamama. Ukizingatia wengi miongoni mwao wanaujua utamu wa kuwa Mbunge na katika uchaguzi uliopita wengi walienda majimboni na wametumia mafao yao yote kupambana majimboni. Halafu ghafla anakuwa raia mwema. Kwa kweli inahitaji nguvu ya ziada kuwa raia mwema ghafla wakati huo umetumia mafao yote kwenye kampeni.

Tatizo lao tamaa tu na kuhisi wao pekee ndo wanawake wa CHADEMA na ndo wana nguvu kuliko CHAMA. nje ya CHAMA hamna mwenye nguvu. Nadhani hata Membe mmemwona. Alipotolewa tu CCM akapwaya ghafla.

Lakini tukumbuke tu ndani ya CHADEMA hao 20 siyo wanawake pekee wenye nguvu. wapo wengi sana.
 
Odhiambo cairo

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
13,832
2,000
Ni vizuri CCM ikahangaika na mambo yake, kuliko hii ya kuhangaika kuvihodhi vyama vya upinzani.

Tumeshuhudia mara kadha kila wapinzani wanapokuwa na ajenda, CCM huingilia kuvuruga. 1. Wakati wa uchaguzi wa wabunge kuwakilisha EALA, Commonwealth & Sadc. Mapendekezo yote ya upinzani CCM haikuyataka. Wakaja na ya kwao na ndiyo yalipita. Sasa na hili la viti maalumu 19 vichache kabisa hawaridhiki CCM mpaka waingilie. Hii haikubaliki
 
Hakimu Mfawidhi

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
1,859
2,000
Ccm shughulikieni matatizo ya wananchi, chadema sio matatizo ya wananchi.

Chadema sio ukosefu wa maji, chadema sio umasikini, chadema sio ukosefu wa madawa, chadema sio barabara mbovu na miundombinu mibovu, chadema sio ukosefu wa madarasa, madawati.

Miaka 60 mmeshindwa kushughulikia matatizo ya watu mmehamia chadema.
 
Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
3,562
2,000
Hio haina tofauti na jaribio la kumuua Tundu Lissu, walijua kumuua ndio watamnyamazisha kumbe hawakujua ndio wanaharibu zaidi na wanampa "SAUTI NA SIFA ZAIDI" katika anga za kimataifa, mungu anamipango yake. CCM kuwanunua hao Covid-19 ndio muendelezo wa kuipaisha CHADEMA anga za kimataifa zaidi.

CCM kila fitna wanayotaka kuifanyia upinzani, ndio wanaupaisha zaidi angani.
tapatalk_1606728997530.jpeg
tapatalk_1606729006244.jpeg
 
chabusalu

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
7,838
2,000
CHADEMA BAWACHA ndio ilibaki nguzo pekee ya CHADEMA ya kuaminiwa.

CHADEMA walilisifu sana BAWACHA kuwa eti wabunge na madiwani wote eti kwa kile kinachoitwa kununuliwa wabunge na madiwani walikuwa ni wanaume tu wanawake wa BAWACHA hawakukubali.

Msimamo huo ulisababisha wabunge wanawake wawekwe wengi kwenye majimbo kuliko wanaume na ikapata baraka ya kamati kuu ikituhumu kuwa mianaume mingi inauzika inafika bei!

Sasa hilo limetokea yuko mbunge Aida KHATAN na wabunge viti maalumu 19 wote kwa mpigo wameingia.

CHADEMA wengine wanasema wamenunuliwa wengine wanasema hao wabunge wote 20 ni maafisa kipenyo wa serikali waliokuwa ndani ya CHADEMA!

Ina maana kwa sasa CHADEMA haitawaamini wanawake wala wanaume kwa kuwatuhumu kuwa wananunulika au ni maafisa kipenyo wa serikali!

Kwa muktadha huo CHADEMA sasa hivi wanatakiwa kwenda retreat kujipanga upya kisiasa badala ya kupigia mikelele CCM!
Kadri nilivyoelewa huu mchakato, ninaweza kuhitimisha kuwa kuna wengine, miongoni mwa hao 19 hawakujua kabisa kama ule ulikuwa ni mchezo uliokuwa ukiratibiwa na akina Mdee, Bulaya & na wengine wachache, lakini bila kuihusisha kabisa Chadema kama taasisi. Kuna wengine walijua kuwa ulikuwa mchakato rasmi, na ni hao ambao sasa wanajaribu kuchomoka lakini nguvu inayowazuia ni kubwa kuliko kawaida! Hata kama Chadema wanapaswa kujipanga upya, lakini haindoi ukweli kwamba kelele kuelekezwa CCM hazipaswi kukoma kwa sababu hiki chama kimeiletea nchi hii siasa za ajabu kabisa katika awamu hii ya Tano, ambazo zinaenda kuligharimu mno taifa hili miaka michache tu ijayo! Taifa likiparanganyika katika maadili huo ndio unakuwa mwisho wake! Unapoona taasisi za uuma zimekosa hofu wala aibu, kwamba mtu ambaye suala lake linapaswa kumalizika mahakamani kwa uwazi kabisa, anafuatwa gerezani usiku gizani na kwenda kuapishwa gereji, kwa mfano, ujue nchi imeishaelekezwa kibra!
 
mdudu

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
3,948
2,000
Ccm shughulikieni matatizo ya wananchi, chadema sio matatizo ya wananchi.

Chadema sio ukosefu wa maji, chadema sio umasikini, chadema sio ukosefu wa madawa, chadema sio barabara mbovu na miundombinu mibovu, chadema sio ukosefu wa madarasa, madawati.

Miaka 60 mmeshindwa kushughulikia matatizo ya watu mmehamia chadema.
Sijui Mataga watakuelewa?
 
JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
2,698
2,000
CHADEMA BAWACHA ndio ilibaki nguzo pekee ya CHADEMA ya kuaminiwa.

CHADEMA walilisifu sana BAWACHA kuwa eti wabunge na madiwani wote eti kwa kile kinachoitwa kununuliwa wabunge na madiwani walikuwa ni wanaume tu wanawake wa BAWACHA hawakukubali.

Msimamo huo ulisababisha wabunge wanawake wawekwe wengi kwenye majimbo kuliko wanaume na ikapata baraka ya kamati kuu ikituhumu kuwa mianaume mingi inauzika inafika bei!

Sasa hilo limetokea yuko mbunge Aida KHATAN na wabunge viti maalumu 19 wote kwa mpigo wameingia.

CHADEMA wengine wanasema wamenunuliwa wengine wanasema hao wabunge wote 20 ni maafisa kipenyo wa serikali waliokuwa ndani ya CHADEMA!

Ina maana kwa sasa CHADEMA haitawaamini wanawake wala wanaume kwa kuwatuhumu kuwa wananunulika au ni maafisa kipenyo wa serikali!

Kwa muktadha huo CHADEMA sasa hivi wanatakiwa kwenda retreat kujipanga upya kisiasa badala ya kupigia mikelele CCM!
Tanzania ina watu 55M+kuondoka kwa Hawa 19,sio shida,wapo vijana wengi tu wenye vipawa,walikuwepo,Zito,Kafulila,Msemakweli,watakuja wengine,ninachojiuliza hii huruma ya Ndugai,kwanini haikuonyeshwa wakati ccm imewatimua Sophia simba,nakundi lake
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
27,443
2,000
Tanzania ina watu 55M+kuondoka kwa Hawa 19,sio shida,wapo vijana wengi tu wenye vipawa,walikuwepo,Zito,Kafulila,Msemakweli,watakuja wengine,ninachojiuliza hii huruma ya Ndugai,kwanini haikuonyeshwa wakati ccm imewatimua Sophia simba,nakundi lake
hawajengwi siku moja hao unowaponda hadi kufika walipofika walikuwa groomed si chini ya miaka 10 ni big loss
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom