Chadema wajihadhari na mawakala wa kupandikizwa na ccm | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema wajihadhari na mawakala wa kupandikizwa na ccm

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Epason, Sep 14, 2010.

 1. Epason

  Epason JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2010
  Joined: Nov 9, 2009
  Messages: 427
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Mimi nina wasiwasi na mikakati mibaya ya chama tawala dhidi ya vyama vya upinzani kwa malengo ya kupata ushindi kwa njia yoyote ile.

  Tumewaona wagombea wa nafasi za ubunge waliopikwa na hichi chama na wakaingia Chadema, wakapitishwa na chama kisha muda mwafaka ulipowadia wakajitoa kwa visingizio mbalimbali kuwapisha wagombea wa CCM. Hali hiyo nayo imeendelea kwa nafasi za udiwani, hayo kwa hichi chama yanawezekana. Sasa hivi tumesikia tunataka kuwaburuza korokoroni kwa utovu wa nidhamu, nionavyo mimi, hili ni sahihi lakini tusiwe wakulalamikia siku zote pale ambapo tumeangukia, tujiulize tulijikwaa wapi. Angalizo tuwe makini na uteuzi wa wagombea wenye nia ya dhati na si bora mgombea.

  Nikirudi kwenye hili la mawakala watakao simamia hizi chaguzi kwa upande wa Chadema inawezekana vilevile wakapikwa wakapikika na kupenyezwa ndani ya chama chetu kisha wakawania hizo nafasi, wakishazipata muda ukiwadia wanauwezo mkubwa wa kutuchinjia baharini na kuambulia patupu. Hili si la kupuuza hata kidogo, useme bora wakala, tuwe makini sana.

  Haya ni maoni yangu, na angalizo tu, nikijua kwenye uwanja wa mapambano kuna mbinu nyingi.
   
Loading...