Chadema wajifunze hili kutoka kwa Ismail Jussa (We need to walk the walk)

Ndugu Wana JF,

Napenda kukiri wazi kabisa na bayana siku zote huwa na kuwa na mitazamo tofauti na Ismail Jussa kwenye masuala mbali mbali yanayohusu siasa na mustakabali wa Taifa letu lakini leo nimepitia kwenye Facebook account yake nimejifunza kitu ambacho Chadema ingekuwa busara wakafanya hivyo pia ili kuondoa dhana potofu ya ki propaganda inayojengwa na Mafisadi! Anyway kitu chenyewe ni hiki hapa chini.

Uwazi kama huu Chadema tunauhitaji sana, Nadhani huwa kuna nafasi za kazi zinatokea makao makuu na mikoani ndani ya chama, Je huwa zinatangazwa hadharani kama hapa JF au facebook au kwenye newspaper au zinajazwa kinyemela? Hapa Mh. Ismail Jussa ijapokuwa ni hasimu wangu, but myonge myongeni lakini haki yake mpeni, Kwani Jussa ana ndugu, jamaa na marafiki wangapi ambao angewapa hizo nafasi? lakini kaamua kuzianika hadharani, Vitu kama hivi ndo tunaita to do things differently and not business as usual kama CCM, WE NEED TO WALK THE WALK AND NOT TALK THE TALK.

Ismail's Profile · Ismail's Wall
  • Ismail Jussa
    I am looking for two suitable and qualified persons to work at the CUF Headquarters in Zanzibar in the Office of Deputy Secretary General. If you are interested, kindly inbox me your number and I will get in touch with you and enlist you for an interview.


    y-2LR9eyI1L.gif
    Sunday at 21:43 via Mobile Web ·LikeUnlike · Comment
    • 13 people like this.
      • Elly Mbilinyi posho? Sunday at 21:48 via Facebook Mobile · LikeUnlike

      • Amani 'amasha' Mhinda Qualification ni zipi comrade kwa faida ya vijana Sunday at 21:52 via Facebook Mobile · LikeUnlike ·
        tddUIK01p63.png
        1 personLoading...

      • Jemal Tour Guide Yeap thats very good quastion @ AMASHA. Sunday at 22:07 via Facebook Mobile · LikeUnlike

      • Magan Omar Nimeinbox hapo komredi. Sunday at 22:18 via Facebook Mobile · LikeUnlike

      • Nasriya Al-dugheish Am I suitable enough???? Sunday at 22:40 · LikeUnlike

      • Ismail Jussa Qualifications: kwa aina ya kazi zenyewe itakuwa vizuri mtu akiwa na angalau first degree. Lakini kama tujuavyo, degree si hoja, unaweza ukawa huna degree lakini ukawa una maarifa mazuri na uwezo wa kutosha pamoja na uzoefu wa kuifanya kazi hii. La muhimu uwe ni mwanachama wa CUF, uwe na maarifa ya kisiasa, uwezo mzuri wa kuandika barua na ripoti kwa Kiswahili na Kiingereza na utashi wa kuhudumia watu. Kazi ya kisiasa haina mshahara ila tunatoa posho la kusaidia kujikimu. Natumai nimesaidia kwa wale waliokuwa na maswali. Sunday at 22:45 via Facebook Mobile · LikeUnlike ·
        tddUIK01p63.png
        2 peopleLoading...

      • Ismail Jussa Nasriya, wewe tena? Akushinde nani? Hahahaha..... Sunday at 22:47 via Facebook Mobile · LikeUnlike

      • Nasriya Al-dugheish Thanks bro Sunday at 22:49 · LikeUnlike

      • Omar Kattah hon Jussa this is what is called political transparent for the sake of zanzibar people. good step forward. i have in box you though. Sunday at 22:54 · LikeUnlike ·
        tddUIK01p63.png
        2 peopleLoading...

      • Slim Kingstone I am not Cuf,,,but kama maambo yatakuwa yanafanywa this way ,,,itapendeza mno,,,equal opprtunity for all. laitit ajira zote zingetolewa hivi,,,,tungekuwa mbali sana Sunday at 23:02 · LikeUnlike ·
        tddUIK01p63.png
        3 peopleLoading...

      • Omar Haroub Adi good this is how democracy is gone well big up jussa Sunday at 23:10 · LikeUnlike

      • Omar Jr S. Mohammed We ndo muheshimiwa wa kwanza kutangaza nafasi ya kazi kwa sisi marafiki zako wa facebook, najua umeona na kutambua umuhimu wetu! Sina kwa kukwambia zaidi ya Ahsante kwa nafasi uliyoitoa na Mungu akupe nafasi zaidi ya kutoa nafasi za kazi kichama na zisizo cha kichama! Baarakka llahu feeka! Sunday at 23:36 via Facebook Mobile · LikeUnlike ·
        tddUIK01p63.png
        1 personLoading...

      • Ali Said nice mr ismail do that way to find some have qualified ,how know his jobb . sio kumpa mpara samaki,, awe aducation minister ,,watoto skuli hawana vitabu vya kusoma, Sunday at 23:39 · LikeUnlike

      • Omar Jr S. Mohammed Kweli usemayo Slim Kingstone. Nadhani Mh. Jussa anatumia vilivyo kauli mbiu ya Chama Cha wananchi ya HAKI SAWA KWA WOTE. Laiti kazi za kitanzania zingeangaliu uwezo kama huu aliokuwa nao Mh. Jussa! Tanzania isingekuwa nchi ya Mgao wa umeme wala shida ya maji! Wala wanafunzi wa vyuo vikuu kukopeshwa wala shule za misingi kuchangia madawati! Yote kwa yote acha niseme Mungu Ibariki Tanzania Aaaameen! Sunday at 23:41 via Facebook Mobile · LikeUnlike

      • Salma Ali Hassan uwanachama wa CUF ni part ya Qualification? Yesterday at 00:50 · LikeUnlike

      • Seif Abalhassan mtume(s.a.w)anasema"zimezoezwa/zimezoeshwa nyoyo juu ya kumpenda mtu mwenye kuzitenda wema na kumchukia mwenye kuzitenda uovu".. binafsi nampenda sana jussa,ALLAH mbariki jussa kwa kuwa kiongozi wa maneno na vitendo,kwa ukweli na uwazi wake na mwisho kwa kuwapenda watu wake!.. unachofanya kaka ni beyond our politics!.. ni kinyume na mazoea,kwa njia naamini utapata watu sahihi kwa ajili ya kazi husika!.. wabillah tawfiq Yesterday at 01:22 via Facebook Mobile · LikeUnlike ·
        tddUIK01p63.png
        2 peopleLoading...

      • Salma Said Huyo Jussa huyo tumempenda wenyewe.... Yesterday at 01:44 · LikeUnlike

      • Othman S Othman Kwanza nikuulize muheshimiwa wataka wazungu au washwahili?
        Pili sifa za mtu umtakae hujazisema ungetaja tukajua kama tuko na hamu ya kuomba Yesterday at 01:49 · LikeUnlike

      • Ismail Jussa Salma, naam uanachama wa CUF ni mojawapo ya qualifications. Hizi ni kazi za Chama kwenye Makao Makuu ya Chama. Loyalty kwa Chama ni moja ya vigezo. Yesterday at 01:58 via Facebook Mobile · LikeUnlike ·
        tddUIK01p63.png
        3 peopleLoading...

      • Othman S Othman ok, haya maneno ya juuu nlikuwa cjayaona, asante sasa sawa. Yesterday at 02:00 · LikeUnlike

      • John Maziku Je kama nikiwa natoka Bara je, naruhusiwa? 23 hours ago · LikeUnlike

      • Said Seif Please give us qualification of that job. 13 hours ago · LikeUnlike

      • Hakim Kombo what the qualifications and describe the job, please? 13 hours ago · LikeUnlike

      • Ismail Jussa Said na Hakim, someni hapo juu. 11 hours ago via Facebook Mobile · LikeUnlike

      • Mohammed Ali Mussa very good step toward building transparency and democracy in our political party of Civic United Front (C.U.F) 11 hours ago · LikeUnlike

      • Khamis H. Haji ‎@Mh. Jussa , job descriptions plz!!! 8 hours ago · LikeUnlike

      • Amar Ali musimuone Mh Jussa leo anang'ara mukafikirie ni bahati mbaya tu, alianzia kama hivi hivi kukitumikia chama mpaka leo amekuwa mtu mmoja muhimu ndani ya chama. Wenye uwezo na hamu ya kutaka kukitumikia chama na kutaka kujifunza mambo, basi musiitupe nafasi adhimu kama hii! Na kila wakipatikana vijana kuanzia miaka 20 mpaka 30 ndio itakuwa safi kabisa! 5 hours ago · LikeUnlike

      • Hassan Khamis muheshimiwa Khamis Mohammed, umesoma vyema hayo maelezo? maana umeambiwa "KINDLY INBOX ME". sio uweke kweupeni,

        kila la kheri 5 hours ago · LikeUnlike

      • Khamis Mohammed Ahsante kwa kunikumbusha @hassan 4 hours ago · LikeUnlike

    • Write a comment...


QUALIFICATION MOJAWAPO UWE MWANA CUF: Kama ni kazi professional, uanachama na udini usiwe vigezo, kama ni kazi ya kichama ilibidi watangaze internally. Au mnatafuta wanachama kwa njia ya ajira
 
Uwazi kama huu Chadema tunauhitaji sana, Nadhani huwa kuna nafasi za kazi zinatokea makao makuu na mikoani ndani ya chama, Je huwa zinatangazwa hadharani kama hapa JF au facebook au kwenye newspaper au zinajazwa kinyemela?

Wakati nakubaliana nawe kwenye swala la transparency ndani ya taasisi yoyote kuna mambo mengi ya kuzingatia kabla hatujavutwa kwa hisia ya kile amekifanya Jussa. Kwanza si CUF wanaotangaza kazi.
I am looking for two suitable and qualified persons to work at the CUF Headquarters in Zanzibar in the Office of Deputy Secretary General. If you are interested, kindly inbox me your number and I will get in touch with you and enlist you for an interview.

Ina umimi zaidi na sio chama, vipi kama angesema "Kuna nafasi ya DSG-CUF Head Quarters mwenye sifa atume maombi kwenda......."
Je, walifanya hivi kumpata Bw. Mtatilo ambaye anashika nafasi ya Maalim Seif??

Kuna issue ya kuwa loyal kwa chama; kwa mfumo wa kutangaza tu kila atakaye aje unapima vipi loyalty ya mtu hata kama kweli ana vigezo vingine tajwa. Nafasi ya Secretary General wa chama sio kama other professional jobs kama Uhasibu.

Ila kama umewahi kusoma juu ya Recruitment inavyofanyika utagundua kwamba wewe ulielewa moja tu "Sourcing by Advertising" ukiamini ndio njia pekee iliyo wazi. Kama ndivyo basi CDM na nyie tangazeni ila Makamba au Mangula wakiomba make sure they'll be considered maana wana uzoefu na qualification kuliko katibu mkuu mwingine yeyote.

Kila taasisi ina recruitment policy yake na pengine ungetufahamisha sie tusio wanachama, recruitment policy ya CDM ikoje??

Kama kuna HR manager unafahamiana nae mwombe akujuze ju ya Internal and External recruitment
 
CHADEMA WAKUBALI WASIKUBALI WANA MENGI SANA YA KUJIFUNZA KUTOKA CUF. KWANI HAWA NI WAKONGE NA WAMEPITIA NJANJA MBALIMBALI KATIKA MUSTAKABALI WA NCHI YETU HUSUSAN UPANDE WA ZANZIBAR. ZANZIBAR ILIPOFIKIA NI JUHUDI ZA CUF.

uSHAURI KWA CHADEMA KUWA WAACHE KWANZA UKANDA, UKABILA NA UDINI BALI WAWE WAKELI WA KAULI ZAO NA KUACHA UBAGUZI NA USHARI.

KAZI KENU CHADEMA
 
CHADEMA WAKUBALI WASIKUBALI WANA MENGI SANA YA KUJIFUNZA KUTOKA CUF. KWANI HAWA NI WAKONGE NA WAMEPITIA NJANJA MBALIMBALI KATIKA MUSTAKABALI WA NCHI YETU HUSUSAN UPANDE WA ZANZIBAR. ZANZIBAR ILIPOFIKIA NI JUHUDI ZA CUF.

uSHAURI KWA CHADEMA KUWA WAACHE KWANZA UKANDA, UKABILA NA UDINI BALI WAWE WAKELI WA KAULI ZAO NA KUACHA UBAGUZI NA USHARI.

KAZI KENU CHADEMA

mmhhhh.....
 
CHADEMA WAKUBALI WASIKUBALI WANA MENGI SANA YA KUJIFUNZA KUTOKA CUF. KWANI HAWA NI WAKONGE NA WAMEPITIA NJANJA MBALIMBALI KATIKA MUSTAKABALI WA NCHI YETU HUSUSAN UPANDE WA ZANZIBAR. ZANZIBAR ILIPOFIKIA NI JUHUDI ZA CUF.

uSHAURI KWA CHADEMA KUWA WAACHE KWANZA UKANDA, UKABILA NA UDINI BALI WAWE WAKELI WA KAULI ZAO NA KUACHA UBAGUZI NA USHARI.

KAZI KENU CHADEMA
 
Ushauri wa bure kwa yule ambaye haipendi Chadema na roho inamkereketa kutokana na mafanikio makubwa iliyopata uchaguzi uliyopita hadi kuwa ndio chama kikuu cha upinzani Tanzania, ushauri ni huu hapa:
Jizuie kuitaja Chadema au kuiandika Chadema, kama mkono wako unafukunyuwa huwezi kupitisha siku bila kutaja au kukiandika chama cha siasa basi anza kujizoeza kuiandika TLP, PONA,JAHAZI lakini sio la Mzee Yusuf. kuendelea kuiandika Chadema kila siku nyinyi ndio msaada mkubwa sana kwa Chadema maana ndio mnaipa umaarufu kuliko ule iliyopaswa kuwa nayo. mti wenye matunda ndio unaopigwa mawe.
 
Ningekuwa mtoa mada bado ningeendelea kuwa na mtazamo tofauti kwa kuangalia yafuatayo;

1. Waliotangaziwa ni marafiki zake wa facebook. Kama usingeileta hapa kama fundisho kwa CDM tusingejua. Soma comments za waliomshukuru.

2. Wengi anawajua. Tayari ameshawaandikia wengine 'hakuna zaidi ya wewe' sasa interview ya nini? Kutakuwa na usawa katika hiyo process?

3. Angalia majina ya wote waliomjibu kasoro John Maziku kutoka 'bara'. Na kwa ulichopost hakujibiwa. Kwa hilo unaweza ukajua pool of choice itakuwa na mix gani!

Hayo ni machache ambayo kama CDM tutajifunza na hatutayafanya. Tunashukuru kwa fundisho lako kupitia kwa makosa ya Jussa sio CUF!
 
Ningekuwa mtoa mada bado ningeendelea kuwa na mtazamo tofauti kwa kuangalia yafuatayo;

1. Waliotangaziwa ni marafiki zake wa facebook. Kama usingeileta hapa kama fundisho kwa CDM tusingejua. Soma comments za waliomshukuru.

2. Wengi anawajua. Tayari ameshawaandikia wengine 'hakuna zaidi ya wewe' sasa interview ya nini? Kutakuwa na usawa katika hiyo process?

3. Angalia majina ya wote waliomjibu kasoro John Maziku kutoka 'bara'. Na kwa ulichopost hakujibiwa. Kwa hilo unaweza ukajua pool of choice itakuwa na mix gani!

Hayo ni machache ambayo kama CDM tutajifunza na hatutayafanya. Tunashukuru kwa fundisho lako kupitia kwa makosa ya Jussa sio CUF!

nakushukuru kwa ilo,maana watu wanaongea kama hawajielewi. Tangu lini facebook page ya mtu ikawa chombo cha kutangaza kazi? Pia Ismail kasema hawatalipwa mshahara ila posho,je iyo ni kazi?au wanataka cdm waache kutoa mishahara nao watangaze kazi za posho?tena kwenye facebook page ya mwanaCUF?jaman ivi IQ za watu zimenaswa na nini? JE,watu hawajui kuwa ili umuinibox mtu kwenye facebook si mpaka uwe Rafiki/swahiba?pia uwe member wa Fcbook?ayo yote ni discrimination kwa non-fbook members! Cdm haikurupuki. Siku nyingine watasupport Rasimu ya katiba ya Cuf kwa rafiki yao Kombani wakingali wanaelewa kuwa katiba inapaswa iandikwe na watanzania wenyewe!si ya mtatiro,komban wala jk. Hawa watu wanaendeleza udikteta. Wachangiaji wa jf Wanadai chadema waache ukanda na ukabila na udini,fanya analysis kwenye fbook ya Ismail,useme marafiki wake/cuf ni wa ukanda gani,dini gani,tamaduni gani,mavazi gani,muonekano upi na ukaribu upi kwa Ismail? Kama kuiga ndo huku Cdm basi iige ili ife. Uwezo wa kufikiri tunao,na kufikiri ni bure na ni zawadi ya bure toka kwa mola Muumba wa mbingu na dunia,pamoja na vyote vilivyomo.
 
nyie nendeni zenu huku ndo tunaita kutafuta cheap popularity! kama kweli CUF wana nia ya kuajiri the best qualified person ni kutafuta consultancy ifanye hiyo kazi! Huyo Jussa hayuko qualified kufanya hiyo interview! Nina uhakika 95% atakayechaguliwa hapo lazma atakuwa mwenye imani moja pili 60% atatoka Zanzibar! hiyo ni kasoro tayari maana mhusika mwenyewe ukiangalia comments zake zina mrengo fulani usio neutral! na pia katika kuajiri watu katika chama kuna vitu kama uaminifu unatakiwa uangaliwe! yaani huwezi kuajiri mtu baki tu kuwa incharged of IT! lazma awe pia mwanachama wa chama husika! maana unaweza ajiri afisa wa UWT ikawa info zinavuja kila siku!
 
Back
Top Bottom