CHADEMA wajibu tuhuma za Mh. Fredrick T. Sumaye baada ya kuikimbia kwa Ballot Box kumkataa

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,951
12,535
Huyu ni waziri mkuu mstaafu ndugu F. T. Sumaye aliyeondoka CHADEMA juzi kwa sababu anazosema kuwa amegusa uenyekiti wa CHADEMA taifa usiogusika

Hii inakuja baada ya kukataliwa na Ballot Box la uenyekiti wa kanda ya Mashariki hata baada ya kuwa mgombea pekee kwa kuambulia kura nyingi za HAPANA kumkataa dhidi ya za NDIYO kumkubali...

SUMAYE aliyeondoka CCM mwaka 2015 kwa sababu za uchaguzi na kujiunga CHADEMA baada ya kushindwa na wagombea wenzake na sababu alizozitoa wakati huo, ndizo hizohizo kazitoa juzi wakati anatangaza kuachana na CHADEMA...

Kilichoongezeka na kuonesha rangi yake halisi na sababu za kumleta CHADEMA ni tuhuma zilezile za miaka na miaka zinazosemwa na wapinzani wa CHDEMA siku zote, uchaga na uenyekiti taifa wa Freeman Mbowe...!!

Kumbe Sumaye alitaka kanuni za uchaguzi zipindishwe ili kumpa upendeleo yeye apite ki-CCM bila kupingwa..!!

Haya ndiyo maelezo mazuri ya chama
 
Ashukuru CDM inaruhusiwa kuchukua fomu ya uwenyekiti wa chama taifa, CCM hicho kitu hakipo ukitaka kulazimisha kesho yake utakutwa porini ukiwa hoi baada ya kuteswa na watu wasiojulikana
Unauhakika? Kwani katiba ya CCM inasemaje kuhusu Uchaguzi wa Mwenyekiti? Ukumbuke Rais ndiyo Mwanyekiti wa chama chao. Ukifanikiwa kuwa Rais wa nchi. Kwa katiba yao. Anakuwa Mwenyekiti bola kupingwa. Je? Chadema Ndivyo wanavyofanya?
 
Kitaturu, Sumaye kapiga panapostahili acheni kutapatapa

Wapi panapstahili?

Kwamba, Mbowe anaua washindani wake kwenye nafasi ya uenyekiti taifa?

Sheria za nchi zinasemaje kuhusu anayeua mtu mwingine?

Ndiyo kusema vyombo vya dola la Tanzania vimeruhusu Mbowe aendelee kuua watu???

Hebu funguka labda utaeleweka...
 
Ndio mnasema mnataka demokrasia?

Demokrasia sio kupata cheo cha dezo bali ni kushinda kihalali kwenye box la kura. Huyo mzee alizoea vyeo vya dezo anadhani hata cdm hilo liko. Ingekuwa kulikuwa na machafuko au box la kura lilitolewa kituoni na kwenda kupunguzwa kura zake hapo sawa. Ukifanya mtihani mwenyewe sio lazima ufaulu. Arudi ccm kwenye demokrasia ya kupita bila kupingwa ukiwa mwenyewe.
 
Unauhakika? Kwani katiba ya CCM inasemaje kuhusu Uchaguzi wa Mwenyekiti? Ukumbuke Rais ndiyo Mwanyekiti wa chama chao. Ukifanikiwa kuwa Rais wa nchi. Kwa katiba yao. Anakuwa Mwenyekiti bola kupingwa. Je? Chadema Ndivyo wanavyofanya?
Ujinga mtupu umeandika, kwa hiyo kama ccm isiposhinda urais automatic itakuwa haina mwenyekiti wa chama.
Na kama ccm kuna demokrasia kweli ni kwanini amruhusu mtu kuchukua form ya kugombea urais au mwenyekiti wa chama 2020 kama katiba yenu inavyowataka, mnaishia kusema ni utamaduni wa chama
 
Wacha kukutwa porini,unaweza ukutwe peponi uko na babu na bibi Adam na hawa/eva
Ashukuru CDM inaruhusiwa kuchukua fomu ya uwenyekiti wa chama taifa, CCM hicho kitu hakipo ukitaka kulazimisha kesho yake utakutwa porini ukiwa hoi baada ya kuteswa na watu wasiojulikana
 
Back
Top Bottom