CHADEMA waja na na mtindo wa Siasa za Kurusha Ngumi Hewani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA waja na na mtindo wa Siasa za Kurusha Ngumi Hewani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mlengo wa Kati, Mar 2, 2011.

 1. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwa yeyote anajua kuangalia siasa na kupima mienendo ya CHADEMA katika siasa ya sasa anaweza gundua mambo mawili
  1. Chadema inajenga umaarufu wa kupata watu wengi kwa mtaji wa 2015
  2.Chadema wanajaribu kupindua serikali kwa mwendo wa kutikisa kiberiti kama kimejaa
  Kwa hoja ya pili Chadema wanatishia kuiondoa serikali kama ilivyofanyika kwa Nchi za kiarabu,hoja kubwa ni baada ya kumaliza maandamano wanayo zunguka Nchi nzima sasa itakua ni kuiondoa serikali! Mimi nasema huu ni uhuni tena ni Uhaini wa wazi kabisa,hivi Chadema wamesahau kama Nchi hii Hatuna Katiba? Hivi kweli Mbowe na Slaa hawajui kama NNchi yetu inaendeshwa kwa Utawala wa Sheria? Jana Mbowe amekaliliwa anasema wataandamana hadi Kieleweke! Swali kieleweke kwa lipi? Mwisho Chadema ikumbuke kuwa kuna majimbo wameaminiwa na Watanzania kuwakilishwa Bungeni pamoja na kuletewa maendeleo! Swali je hawa Wabunge wanaendelea na maandamano watatimiza lini majukumu yao? Najua Chadema inawatu makini kama Prof Baregu,Zitto na Mnyika! Hivi wanashindwa kumwambia Slaa kama anachofanya ni kuhatarisha ustawi wa Taifa letu! Aidha naona hapa Slaa hana kazi ya kufanya baada ya kushindwa Uchaguzi imekua nongwa!
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Wewe ndiye muhuni.
  Unalipwa shiing ngapi?
   
 3. kalagabaho

  kalagabaho JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,272
  Likes Received: 2,054
  Trophy Points: 280
  ulimbukeni wa ubunge unawasumbu! awaache waandamane na wasahau majimbo yao. 2015 tunayarejesha yote! harafu waseme tumechakachua wakati wapo bize na upuuzi wa kumridhisha SLAA ambaye hana kazi ya kufanya sasa hivi
   
 4. Mark Francis

  Mark Francis Verified User

  #4
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 605
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hujui siasa.... kaa kimya!? CDM ina wabunge wangapi? Wabunge wangapi wapo kwenye hiyo programme?? Fuatilia kwa umakini kabla hujaanzisha thread yako...!?
   
 5. kalagabaho

  kalagabaho JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,272
  Likes Received: 2,054
  Trophy Points: 280
  wewe Paka ndiye muhuni! unapelekeshwa tuu kama boya
   
 6. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Kuna ubaya gani kujenga umaarufu?mbona CCM walifanya hivyo?
  Utawala wa sheria nchii hii unafanya kazi kwa maslahi ya wananchi au Rais aliyepewa mamlaka kubwa na Katiba??.....tuna Katiba mbovu ndo maana watu wamejisahau na CHADEMA kwa kujua mapungufu ya Katiba na mfumo mzima wa kisheria hawawezi kuutumia..its allowed as long as hayakiuki misingi ya haki za binadamu na yameruhusiwa......

  Naomba utueleze uhuni wa CHADEMA uko wapi kama wanachokidai kwenye maandamano ni mambo ambayo yanawagusa watanzania wote kwa ujumla....bei za vyakula kupanda na hali ya maisha kuzidi kuwa ngumu na ufisadi mkubwa ni uhuni? kwanini husemi Kikwete ni muhuni kutuahidi sisi wakati wa kampeni then juzi kusema kama Nyerere hakuweza kutimiza yote,Mwinyi na Mkapa hata yeye pia hataweza....muhuni ni yule aliyetuahidi uongo tumpe kura na sasa anajidai kuwa wazi kuwa alitudanganya na hawezi kutimiza yote aliyoahidi?

  Slaa ni mtu makini na hafanyi mambo peke yake,anaungwa mkono na watu makini wenzie hao uliowataja!!!
   
 7. CPU

  CPU JF Gold Member

  #7
  Mar 2, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ina maana katika mambo yote haukuona kwamba kufeli watoto wa form four ni janga la kitaifa, au kupanda gharama za maisha ndio sio UHAINI NA UHUNI WA MACHO MACHO?
  Au ndo lengo la shule za kata kufelisha watu,...maana kakaa kimya tu badala yake anaongelea chadema!
  Hivi unadhani hao 89% walofeli wanaenda wapi na wanafanya nini saivi kama sio kwenda kwenye mikutano ya chadema kutafuta tumaini la maisha ya uhakika?

  Hiyo katiba ndio iliruhusu PM aseme uongo bungeni? Na Spika atupilie mbali ushahidi wa kweli? Au huo ndio utawala wa sheria??
  Acha jazba
   
 8. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #8
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Mjinga asiyejua kwamba yeye ni mjinga huyo ni sumu katika jamii. Wewe ni moja wao.
   
 9. kalagabaho

  kalagabaho JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,272
  Likes Received: 2,054
  Trophy Points: 280
  rekebisha kauli yako! madai ya chadema hayawagusi watanzania wote! we dada vipi? umetumwa?
   
 10. V

  Vumbi Senior Member

  #10
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 191
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Thanx, umenifurahisa sana na post yako. Ningekuwa sijao ningekutafuta ungenifaa sana, lakini basi tena.

   
 11. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #11
  Mar 2, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Heshima kwako Mlengo wa kati,

  Mkuu CHADEMA ni chama cha siasa malengo makuu ya chama chochote siasa ni kushika dola,kuna ubaya gani chama cha siasa kikiwa na lengo la kupata watu wengi kwa mtaji wa siasa 2015 ?.Hoja yako ya pili unadai CHADEMA wanatishia kuiondoa serekali iliyoko madarakani kama ilivyotokea kwa nchi za kiarabu,kwamba nchi hii ina katiba na blah blah kibao.Mkuu napenda kukuambia hata Misri walikuwa na katiba inayolinda madaraka ya rais wa nchi hiyo lakini ilipofikia mahali wananchi wakachoswa waliiondoa serekali ya Hosn Mubarak bila kujali katiba iliyokuwa ikimlinda hawakuata hata kusubiri Mubarak amalizie muhula wa uliokuwa umebakiza miezi nane tu.Nikirejea Tanzania zipo dalili za wazi serekali ya J Kikwete imeshindwa kumaliza matatizo ya umeme ambayo aliyakuta kipindi cha muhula wake wa kwanza.Kikwete ameshindwa kumaliza ufisadi ndani ya chama chake na serekali anayoiongoza.Ameshindwa kwa kiasi cha kutisha na kusikitisha kutambua na kuchukua hatua madhuti kuongoza taifa.Hajui wajibu na dhamana ya urais wa JMT hana tofauti na baba aliyeshindwa kuwapatia chakula watoto wenye njaa [analia na watoto wanalia hakuna tofauti ya baba na mtoto].

  Katiba ya JMT tunajua ipo lakini si lazima tuvumilie hadi miaka mitano imalizike huku taifa likiendela kuyumba kiuchumi,kisiasa na kijamii rais akishindwa kutimize wajibu wake wananchi waliompatia kazi wana uwezo na sababu za kumwondosha madarakani.Tanzania ikifanya hivyo haiata kuwa nchi ya kwanza au ya mwisho dunia kuchukua hatua kama hizo.

  [
  Heshima kwako PakaJimmy,

  Mkuu JF ni jukwa la magreat thinker hoja hujibiwa kwa hoja si viroja.

  Heshima kwako Kalagabao

  Jibu hoja wacha matusi.

  Heshima kwako Michelle,

  Ewaa nimependa na kuzikubali hoja zako.
   
 12. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #12
  Mar 2, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
   
 13. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #13
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  umetumwa au una share na mafisadi lile jinamizi la kuchakachau ndio linawatafuna nyie mafisadi na vibaraka wenu wote
   
 14. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #14
  Mar 2, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  salva rweyemamu habari ya mchana,..daily news halikutoshi mpaka uje na huku kuandika tahariri zako za kipropaganda
   
 15. b

  beahunja Member

  #15
  Mar 2, 2011
  Joined: Feb 6, 2010
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lazima upo chini ya kivuli kinachotokana na neema ya watawala ni sahihi kabisa kutetea matawi kivuli kiendelee
   
 16. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #16
  Mar 2, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,461
  Likes Received: 5,846
  Trophy Points: 280
  Hajatumwa...amejituma...madai ya CHADEMA hayawagusi wachache kama wewe mlio katika payroll ya mafisadi
   
 17. msafiri.razaro

  msafiri.razaro JF-Expert Member

  #17
  Mar 2, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 616
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Ungekuwa wa maana kama ungelimshauri Spika kuwa haya ni madhara ya kuwaziba midomo wabunge wetu, angeruhusu hoja ya Hali mbaya ya umeme, mfumuko wa bei, katiba mpya na Mabomu, maandamano yasingefanyika kwani ujumbe ungefikishwa pale panapohusika. Lakini kwa katiba hiyo hiyo chama tawala na wabunge wake wakishilikiana na spika mulizuia hoja za wabunge wa upinzani ambazo ndio kilio cha wananchi walio wengi kwa serikali yao, sasa kama wameshindwa kutoa hoja bungeni ili serikali ifanyie kazi changamoto zao, basi wameamua kutufikishia changamoto hizo sisi waajili wa serikali, ili tupime na tuamue.

  Naomba kuwakilisha.
   
 18. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #18
  Mar 2, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,461
  Likes Received: 5,846
  Trophy Points: 280
 19. msafiri.razaro

  msafiri.razaro JF-Expert Member

  #19
  Mar 2, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 616
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Ungekuwa wa maana kama ungelimshauri Spika kuwa haya ni madhara ya kuwaziba midomo wabunge wetu, angeruhusu hoja ya Hali mbaya ya umeme, mfumuko wa bei, katiba mpya na Mabomu, maandamano yasingefanyika kwani ujumbe ungefikishwa pale panapohusika. Lakini kwa katiba hiyo hiyo chama tawala na wabunge wake wakishilikiana na spika mulizuia hoja za wabunge wa upinzani ambazo ndio kilio cha wananchi walio wengi kwa serikali yao, sasa kama wameshindwa kutoa hoja bungeni ili serikali ifanyie kazi changamoto zao, basi wameamua kutufikishia changamoto hizo sisi waajili wa serikali, ili tupime na tuamue.

  Naomba kuwakilisha.
   
 20. Ba Martha

  Ba Martha JF-Expert Member

  #20
  Mar 2, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Crappppppppppp!!!!!
   
Loading...