CHADEMA waichambua Ripoti ya CAG. Waibua ufisadi mwingine wa Sh. Trilioni 1.6

CHADEMA

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
488
2,468
Mkutano na waandishi wa habari ulijikita katika maeneo manne yafuatayo;

1. Kufanya uchambuzi wa Ripoti ya CAG hasa katika;

1.1 Ukaguzi wa Hesabu za Serikali Kuu
Usimamizi wa fedha kwa mujibu wa taratibu za
kisheria (ambapo kuna matumizi yanayotiliwa
shaka na kuhojiwa ya trilioni 1.6, ambazo
hazikuingia hazina lkn zinadaiwa kutumika kwenye miradi ya maendeleo)
Deni la Serikali (kwa sasa wanakwepa kuweka deni la taifa Vyama vya siasa

1.2 Ukaguzi wa Hesabu za Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambao ni mojawapo ya maeneo ya uso wa Rais Magufuli na kuna failures nyingi sana.

1.3 Ukaguzi wa Hesabu za Miradi ya Maendeleo

1.4 Ukaguzi wa Hesabu za Mashirika ya Umma
ATCL
NHC
TPDC
Bodi ya Utalii
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii

2. Kufafanua maeneo yaliyokuwa yanagusa hesabu za Chama eg. suala la umiliki wa gari Nissan Patrol, matumizi yenye upungufu wa nyaraka.

3. Kumtaka Rais Magufuli atoke hadharani kuzungumzia uozo wa kutisha ulioibuliwa na CAG na anachukua hatua gani? Pia kutaka uwajibikaji wa mawaziri katika maeneo husika.

4. Kutoa maagizo na maelekezo kwa Wabunge wa CHADEMA, Kambi ya Upinzani Bungeni (mawaziri kivuli) kuanza kuifanyia kazi mara moja ripoti ya CAG ambapo Mawaziri Vivuli wanatakiwa kuendeleza uchambuzi kwa msimamo uliowekwa na kauli ya Chama kisha wazungumze na waandishi wa habari.

5. Kuzitaka Kamati za Oversight kwa maana ya PAC na LAAC ambazo zinaongozwa na Kambi ya Upinzani ambayo inaongozwa na CHADEMA, kusimamia suala hilo kwa mamlaka waliyonayo juu ya vyombo mbalimbali, ikiwemo kuviita vyama vya siasa ili vitoe maelezo ya ukaguzi wa hesabu zao. Chadema tuko tayari kuitikia wito wa Kamati hizo na kutoa maelezo ya hesabu zetu hasa ikizingatiwa kuwa Chadema ndiyo iliyoweka msukumo ndani ya bunge na hatimae kuwepo au kuwekwa kwa utaratibu wa kisheria wa CAG kukagua hesabu za matumizi ya vyama vya siasa.

Masuala yaliyochambuliwa katika ukaguzi wa CAG wa mwaka 2017/2018 ambapo ametoa ripoti 17 ni mengi, kwa hatua ya sasa, Chama kimezungumzia hayo kwanza.





 
Back
Top Bottom