CHADEMA wagonga mwamba: Rais Jakaya Kikwete awapiga chenga, ashindwa kuwakubali kutosaini

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797


  • Rais Jakaya Kikwete awapiga chenga
  • Ashindwa kuwakubalia kutosaini Muswada
  • Mnyika asema msimamo wao upo pale pale
Na Mwandishi Wetu



"Mkutano huo uliofanyika Ikulu, umefanyika katika mazingira ya maelewano na pande mbili hizo zimekubaliana kama ifuatavyo.

"Kwanza pamoja na sheria hiyo kupitishwa na Bunge, ipo haja ya kuendelea kuiboresha ili ikidhi mahitaji ya kujenga kuaminiana na mwafaka wa kitaifa.
"Pili, yawepo mawasiliano na mashauriano ya mara kwa mara kati ya Serikali na wadau mbalimbali juu ya kuboresha sheria hiyo kwa lengo la kudumisha muafaka wa kitaifa kwenye mchakato wa Katiba mpya," ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilisainiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi.

Alipozungumza na MTANZANIA juu ya Rais kutosema kama hatasaini muswada huo kama walivyokuwa wakipendekeza, Mnyika alisema: "Sisi msimamo wetu upo pale pale, kwamba tunamshauri Rais asisaini Muswada huo.


"Sasa kama atasaini hilo liko kwake, waulizeni watu wa Ikulu kwa sababu hata katika mapendekezo tuliyowaachia Ikulu jana (juzi), suala la kutosaini muswada lilikuwa ni moja ya ushauri wetu kwa Mheshimiwa Rais," alisema Mnyika.


Katika waraka wa Chadema uliowasilishwa Ikulu juzi na viongozi wa chama, walikuwa wakimshauri Rais Jakaya Kikwete kutumia mamlaka aliyonayo, kifungu 97(2) cha Katiba ya Tanzania kukataa kuukubali Muswada huo uliopitishwa na Bunge Novemba, 18, mwaka huu na sasa kinachosubiriwa ni ridhaa ya Rais kabla ya kuanza kutumika.


Katika waraka huo, Chadema walisema endapo Muswada huo utapata ridhaa ya Rais na kuanza kutumika kama Sheria, utakuwa na madhara makubwa katika mchakato mzima wa utungaji wa Katiba Mpya pamoja na amani na utulivu wa nchi.


"Mheshimiwa Rais, Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ulichapishwa kwa mara ya kwanza kwenye Gazeti la Serikali la tarehe 11 Machi 2011. Muswada huo ulipelekwa katika Mkutano wa Tatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa Hati ya Dharura tarehe 9 Aprili 2011.


"Hata hivyo, baada ya upinzani mkubwa dhidi ya Muswada huo kujitokeza karibu nchi nzima, Bunge lililazimika kuondoa Hati ya Dharura na hivyo kufanya Muswada kushughulikiwa kwa mujibu wa utaratibu wa kawaida wa kutunga sheria uliowekwa na Kanuni za Kudumu za Bunge.


"Katika Taarifa Rasmi ya Majadiliano Katika Bunge ya tarehe 15 Aprili 2011, Bunge liliiagiza Serikali ili muda zaidi utolewe kwa Kamati na wananchi kuufikiria Muswada huu na katika kufanikisha hili, iandae Muswada huu kwa lugha ya Kiswahili ili wananchi wenyewe waweze kusoma yaliyo kwenye Muswada huo badala ya kupewa tafsiri tu na watu wengine.


Waraka huo unaendelea kusema kuwa, katika kutoa maagizo haya, Bunge lilisisitiza kwamba, Muswada huu uko ndani ya Bunge, hauko serikalini, hata hivyo, hakuna hata moja ya maagizo haya ya Bunge ambalo lilitekelezwa na Serikali. Kamati ya Sheria na Katiba haikukaa kuujadili Muswada tena kati ya Aprili 15 hadi Oktoba 24, 2011 wakati Muswada ulipoletwa kwenye Kamati ukiwa umefanyiwa marekebisho makubwa.


Waraka unasema, tafsiri ya Kiswahili ya Muswada wa Aprili ililetwa Bungeni Novemba 5, siku tatu kabla ya Bunge kuanza mkutano wake wa tano, kwa maana hiyo, Muswada wa Sheria uliotolewa maoni na wadau kabla ya Oktoba 24 ni ule wa Aprili ambao maoni ya wadau yalitolewa Aprili 11 2011. Wananchi hawakupatiwa fursa ya kutosha ya kutoa maoni yao juu Muswada ulioletwa Bungeni ukiwa umefanyiwa marekebisho kwa sababu Muswada huo ulitolewa kwenye Kamati Oktoba 24 na uligawiwa kwa wabunge wote Novemba 5, 2011.

"Muswada wa Sheria hii muhimu ulihitaji na bado unahitaji mjadala wa kitaifa wa wananchi kama ambavyo makundi mbalimbali ya kijamii na asasi za kitaaluma kama Chama cha Mawakili Tanganyika, Chama cha Majaji Wastaafu, Chama cha Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, asasi zaidi ya 180 zinazounda Jukwaa la Katiba, Umoja wa Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Umoja wa Madhehebu ya Kidini Tanzania (IRCPT) na watu mashuhuri kama Jaji Mkuu mstaafu Barnabas Samatta na msomi mashuhuri nchini, Profesa Issa Shivji wanavyodai katika mijadala inayoendelea nchi nzima.


"Aidha, Bunge lilihitaji na linahitaji muda zaidi wa kuyatafakari mambo makubwa ya kimsingi ambayo limeyapitisha kuwa sheria na katika mazingira haya, tunaamini kwamba ni busara kwako Mheshimiwa Rais kukataa kuukubali Muswada huu ili kuruhusu mjadala wa wananchi unaohitajika ufanyike," ilisema sehemu ya taarifa hiyo.


SUALA LA MUUNGANO NA NAFASI YA ZANZIBAR

"Muungano wetu upo katika hatari kubwa ya kuvunjika kwa sababu ya mabadiliko makubwa ya kikatiba ambayo yamefanyika katika Katiba ya Zanzibar, mwaka 1984 kutokana na Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Hii ni kwa sababu Sheria ya Mabadiliko ya Kumi ya Katiba ya mwaka 2010, inaashiria tafsiri mpya ya Makubaliano ya Muungano na ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inahoji misingi ya Jamhuri ya Muungano kama nchi moja, mamlaka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano, na mambo muhimu ya Muungano.

"Kwamba wakati Katiba ya Jamhuri ya Muungano inatamka wazi kwamba Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano, Katiba ya sasa ya Zanzibar inatamka kwamba Zanzibar ni miongoni mwa nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Wakati Katiba ya Jamhuri ya Muungano inampa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa kushauriana kwanza na Rais wa Zanzibar kuhusu mamlaka ya kuigawa Tanzania Zanzibar katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo, Katiba ya sasa ya Zanzibar inampa Rais wa Zanzibar mamlaka hayo kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.

"Wakati Katiba ya Jamhuri ya Muungano inatamka wazi kwamba, Rais wa Jamhuri ya Muungano atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu, Katiba ya sasa ya Zanzibar inatamka wazi kwamba, kutakuwa na Rais wa Zanzibar ambaye atakuwa Mkuu wa Nchi ya Zanzibar na pia Katiba ya sasa ya Zanzibar inatamka wazi kwamba Rais wa Zanzibar atakuwa Kamanda Mkuu wa Idara Maalum.

"Wakati Katiba ya Jamhuri ya Muungano inatamka wazi kwamba mambo ya ulinzi na usalama yakiwemo mambo ya kijeshi ni mambo ya Muungano, Katiba ya sasa ya Zanzibar inaunda vikosi vya kijeshi vinavyojulikana kama Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambazo ni Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU), Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM), Chuo cha Mafunzo na Idara nyingine yoyote itakayoanzishwa na Rais wa Zanzibar ikiwa ataona inafaa.


"Wakati Katiba ya Jamhuri ya Muungano inaipa Mahakama ya Rufani ya Tanzania mamlaka ya kusikiliza rufaa dhidi ya maamuzi ya Mahakama Kuu ikiwamo Mahakama Kuu ya Zanzibar, Katiba ya sasa ya Zanzibar imefuta haki ya Wazanzibari kukata rufaa katika Mahakama ya Rufani ya Tanzania dhidi ya uamuzi wowote wa Mahakama Kuu ya Zanzibar unaohusu ukiukwaji wa haki za kimsingi za binadamu.


"Vile vile wakati Katiba ya Jamhuri ya Muungano inatambua nafasi ya Waziri Kiongozi katika muundo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Katiba ya sasa ya Zanzibar imefuta nafasi hiyo na kuunda nafasi mbili zinazojulikana kama Makamo wa Kwanza na Makamo wa Pili wa Rais," inasema sehemu ya taarifa hiyo.



 
Hivi habari hii ina jipya kweli?
Zaidi sana naona kama umeiandika katika namna ya kuponda mkutano wa Ikulu, kitu ambacho si sahihi, maana JK ameahidi kupokea ushauri wa kuboresha muswada huo!
 
Sasa ukweli utapatikana? kuwa mkutano ni mafanikio au la?
 
Hivi habari hii ina jipya kweli?
Zaidi sana naona kama umeiandika katika namna ya kuponda mkutano wa Ikulu, kitu ambacho si sahihi, maana JK ameahidi kupokea ushauri wa kuboresha muswada huo!
PakaJimmy achana na magazeti yenye wahariri vilaza,
 
Mbona hujatuielezea hiyo chenga yenyewe zaidi ya kurudia (copy and paste) tunayoyafahamu?
 
SASA KUSHINDWA KUKUBALI NDIO KISWAHILI GANI...!!!???aU ULIKUWA UNATAA KUSEMA AMEKATAA..??Tuonyeshe mahali alipokataa kwenye taarifa uliyobandika hapa..!!Watu wengine bana sijui vichwa vinapitisha upepo saingine au vinaweka mic kama gari ya petrol..!!!Nilikuwa nasoma niangalie saa na trh aliyotamka kwamba hakubaliani/au saa na dakika aliyosaini hiyo karatasi kumbe unaleta porojo za uji wa mabundubungu tu hapa kutupotezee wakati...!!Craaaap..!!:smash:
 
Kwanza ka copy na ku paste yaliyoandikwa kwenye waraka wa CDM kwa raisi hakuna inputs yake hata moja
 
Hawa ndo wanairudisha tasnia ya habari nyuma, bora hiyo page wangebandika picha ya sangara wa ziwa victoria
 
Hivi habari hii ina jipya kweli?
Zaidi sana naona kama umeiandika katika namna ya kuponda mkutano wa Ikulu, kitu ambacho si sahihi, maana JK ameahidi kupokea ushauri wa kuboresha muswada huo!
That's Journalism... Sio waandishi wote wanaona kila kitu sawasawa... hata wewe ungeandika uonavyo tofauti na wengine
 
:llama:mimi niachokiona ni kwamba kuna lugha inayoweza kutafisirwa kisheria ,au kiinginia au kisiasa lakini suala lililopo mezani kwa mhe kikwete ni la kisheria zaidi na kama ni hivyo makubaliano hayo hawezi kusaini sababu sio masahihisho ya mtihani au barua ya mwanafunzi .unaposema inahitaji marekebisho tayari umekiri kwamba kilichopitishwa sio sahihi, na anyesihiri kurekebisha sio rais bali ni kikao kile kile lazima kikae tena kifanye marekebisho na dio wenye uwezo .hivyo ni mafanikio makubwa kwa chadema
 
Back
Top Bottom