CHADEMA wagomea uchaguzi wa Naibu meya manispaa ya Iringa, msimamizi avunja mkutano

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,903
141,850
Baraza la madiwani manispaa ya Iringa lina wajumbe 28 CHADEMA 14 na CCM 14.
Awali Naibu meya alikuwa mwanachama wa CHADEMA lakini aliunga mkono juhudi na kuhamia CCM ambako walimwomba agombee tena udiwani na kisha unaibu meya.

Uchaguzi umevunjika baada ya CHADEMA kudai kila mpiga kura aandike jina lake kwenye karatasi ya kupigia kura kitu ambacho ni kinyume cha utaratibu na walipokataliwa waliamua kutoka nje ya ukumbi.

Source ITV habari!
 
Kwani katika uchaguzi wa meya; kuna ubaya gani mwana ccm kumpigia kura mgombea wa Chadema? Pia hakuna ubaya mwana chadema kumpa kura mgombea wa ccm. Hiyo ndio democrasia tunayoitaka. Kama mpiga kura anaona mgombea wa chama chake hawezi jukumu la umeya, ana uhuru wa kumpa kura mgombea wa chama kingine.
Hali hiyo imetokea maeneo mengi hapa tz na maeneo mengi tu duniani.

Suala kwamba kuna wapiga kura 'wamenunuliwa' na chama kingine hilo linahusu udhaifu ndani ya chama husika. Kimsingi watu wawe huru kumpigia kiongozi wanaemtaka lakini wasikubali kununuliwa.
 
Baraza la madiwani manispaa ya Iringa lina wajumbe 28 Chadema 14 na CCM 14.
Awali Naibu meya alikuwa mwanachama wa Chadema lakini aliunga mkono juhudi na kuhamia CCM ambako walimwomba agombee tena udiwani na kisha unaibu meya.

Uchaguzi umevunjika baada ya Chadema kudai kila mpiga kura aandike jina lake kwenye karatasi ya kupigia kura kitu ambacho ni kinyume cha utaratibu na walipokataliwa waliamua kutoka nje ya ukumbi.

Source ITV habari!
Hivi hawa madiwani wa Chadema hawana akili hadi Msigwa akague kura zao?kuandika jina kwa mujibu wa sheria na utaratibu upi?
 
kama ni kweli hicho ni kituko
Chadema ni chama Cha demokrasia kiache utoto.Waache demokrasia ifanye Kazi.Diwani huchaguliwa na watu wote wenye vyama na wasio na vyama Sasa akishachaguliwa kule ndani Kama Ni kuchagua meya au naibu demokrasia iachwe ichukue mkondo.Si vizuri kila wakati kutuhumiana sijui Nani kanunuliwa chadema acheni utoto.Kura Ni Siri ya mtu na ibaki hivyo
 
Chadema hawaaminiani kabisa!
 
Kwani katika uchaguzi wa meya; kuna ubaya gani mwana ccm kumpigia kura mgombea wa Chadema? Pia hakuna ubaya mwana chadema kumpa kura mgombea wa ccm. Hiyo ndio democrasia tunayoitaka. Kama mpiga kura anaona mgombea wa chama chake hawezi jukumu la umeya, ana uhuru wa kumpa kura mgombea wa chama kingine.
Hali hiyo imetokea maeneo mengi hapa tz na maeneo mengi tu duniani.

Suala kwamba kuna wapiga kura 'wamenunuliwa' na chama kingine hilo linahusu udhaifu ndani ya chama husika. Kimsingi watu wawe huru kumpigia kiongozi wanaemtaka lakini wasikubali kununuliwa.
Watu walipigwa mkwara kwenda kumuona Lema gerezani unadhani ni mchezo.
 
Ni kweli mkuu........ tena mchungaji Msigwa kasema wako tayari kuharibu kura kuliko kupiga kura za siri!
Msigwa anaweka precedence mbaya CCM na sisi tukisema tuko tayari hata kuharibu kura ili Msigwa asiwe mbunge tena wa Iringa Mjini uchaguzi ujao atasema tumemuonea? Wakati yeye ndie kalianzisha?
 
Nikulipe mshahara,posho,hela ya mafuta na umtangaze mtu wa upinzani hiiiiiiiiiiiiiiii
 
Sasa ukiandika jina kwenye Karatasi ya kupigia kura si unakua umeharibu kura?
Walitaka jina lake liandikwe nyuma ya karatasi ili ijulikane ile kura kapiga nani, wasiwasi wao kuna madiwani wa chadema walikuwa tayari kumpigia diwani wa CCM. Maana hata diwani mmoja tuu wa CDM akimpigia wa CCM tayari ccm wanashinda kwa kuwa wana idaidi swsawa ya madiwani.
Hii ni sawa na kusema watu wakapange mstari nyuma ya mgombea. Hawa jamaa Demokrasia imewashinda kura ni siri wakubaliane na matakwa ya demokrasia.
 
Baraza la madiwani manispaa ya Iringa lina wajumbe 28 CHADEMA 14 na CCM 14.
Awali Naibu meya alikuwa mwanachama wa CHADEMA lakini aliunga mkono juhudi na kuhamia CCM ambako walimwomba agombee tena udiwani na kisha unaibu meya.

Uchaguzi umevunjika baada ya CHADEMA kudai kila mpiga kura aandike jina lake kwenye karatasi ya kupigia kura kitu ambacho ni kinyume cha utaratibu na walipokataliwa waliamua kutoka nje ya ukumbi.

Source ITV habari!
Lakini naona hapo Chadema wanashindwa tu hesabu. Kama wanajua idadi yao wote( Ccm na Chadema) ni 28 si watahesabu kura zisiwe zimezidi idadi ya wajumbe? Mbona hilo sio tatizo. Labda wanataka ubishi tu basi.
 
Back
Top Bottom