CHADEMA - Wagombea wenu Bunge la Afrika Mashariki ni nani?

QUALITY

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
853
115
jana gazati la Nipashe liliandika kuwa leo jumatatu mtafanya mchakato wa kupata wagombea wenu. Mpaka sasa hatujasikia kilichojiri. CDM makao makuu mnaweza kutupa kilichojiri au zoezi halikufanyika?

Quality
 
Chadema wamteua Komu kuwania Ubunge Afrika Mashariki- EALA Send to a friend
Monday, 09 April 2012 20:53
0digg

Boniface Meena
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimemteua Anthony Komu kuwania Ubunge katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA).

Uteuzi huo ulifanyika jana jijini Dar es Salaam
Taarifa iliyotolewa na ofisa habari wa chama hicho, Tumaini Makene ilieleza kuwa katika uteuzi huo ulioamuliwa kwa kura za wajumbe, Komu aliweza kuwashinda wenzake wengine tisa, kwa kupata zaidi ya asilimia 50 katika mzunguko wa pili, baada ya wagombea wote kushindwa kukidhi kigezo cha katiba ya chama kuwa mshindi lazima apate asilimia 50 ya kura za wajumbe wa mkutano husika wa uteuzi.

Alisema wagombea ambao majina yao yalipigiwa kura katika mzunguko wa kwanza ni pamoja na Godfrey Mnubi, Edgar Chibura, John Malanilo, Patrick Nkandi, Anna Maghwira, Deogratias Assey, Pasquina Lucas, Deusdedit Kahangwa, Antony Komu na Mwantum Mgonja.

Makene alisema katika mzunguko wa pili, mchuano ulikuwa kati ya Maghwira, Malanilo na Komu. Baada ya kura, Komu aliibuka mshindi kwa kupata asilimia zaidi ya 50 ya kura zote zilizopigwa.

"Uteuzi huo wa mwisho wa kupata mgombea wa EALA kwa tiketi ya Chadema umefanyika baada ya kukamilika kwa hatua zote za awali ikiwamo uchukuaji na urejeshaji fomu za wagombea waliojitokeza kuwania nafasi hiyo,"alisema Makene.
Wakati Chadema kikimpata mgombea wake huyo, leo Bunge linatarajia kufanya uchaguzi wa wabunge watakaoiwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki.
 
Duh,Komu ni yupi hebu tukumbushane wadau
Itakuwa ni zile zile sura tunazoziona kila wakati! Sijui hakuna watu wengine! Hivi huu mchakato wenyewe umeenda chini kwa chini, nilitaka nirushe karata yangu ndani ya chama dume! Lakini sasa, Lol! Anyway, its M4C.
 
Itakuwa ni zile zile sura tunazoziona kila wakati! Sijui hakuna watu wengine! Hivi huu mchakato wenyewe umeenda chini kwa chini, nilitaka nirushe karata yangu ndani ya chama dume! Lakini sasa, Lol! Anyway, its M4C.

wa ukenyege habari za muda,bila shaka arumeru ilikupoteza jamvini,KUHUSU HOJA YAKO just compare ccm and cdm,majina ya magamba ni walewale wanaotaka kurithi kama son of malicela ,mwinyi,bilal etc
 
Komu ni mkurugenzi wa fedha na utawala hapo makao makuu. Ndo Mpango wa kubebana, "mwenzetu"?! Tudumishe demokrasia. na wengine wanaweza Bana
 
kila la kheri. iingieni mshiriki kukijenga chama msiwe pembeni kipindi cha upambanaji.inapofika uchaguzi mko kundini mnataka nafasi.
I HOPE UKISHIRIKI UKOMBOZI UTAPATA NAFASI HIYO.GET INTO POLITICS.
 
Back
Top Bottom