Chadema wagawanyinga

Zhu

Senior Member
Sep 26, 2010
184
24
wabunge 11 wa chadema wamepinga msimamo wa mwenyekiti freeman Mbowe wa Kususia hotuba ya rais katika ufunguzi wa bunge la kumi
 
Wamepinga! Mbona Siku ya kususia hawakubakia kwenye viti vyao?
Au walipinga kwa maneno tu lakini kuondoka ukumbini waliondoka?
 
Ukiwa tofauti na mwenyekiti katiba ikowazi tunakufukuza uanachama tuone kama ukienda ccm watakupokea na wakusinamishe uwe mbunge tena!
 
Hawakufika kabisa bungeni, hii inaonyesha ni jinsi gani mbowe na mtei wanavyotaka kuwaburuza vijana waliochaguliwa na wananchi kuwawakilisha na sasa wanataka kuwatumia kutimiza haja zao na si maslahi ya wananchi waliowachagua.
 
source yenyewe ni gazeti la uhuru jamani ndio limeandika hiyo habari. Unategemea nini hapo kwani kwenye hiyo habari
 
CHADEMA IS INTACT. Watanzania million 34 ambao hawakumpigia kura huyo kiwete sorry kikwete na Prof. pumba wanakiunga mkono. Anayebisha asubiri hapo makamanda watakapo choka wakatuamlisha tutumie Peoples power!! asieyjua nguvu zetu aulize watu wa jimbo la Nyamagana.
 
Hawakufika kabisa bungeni, hii inaonyesha ni jinsi gani mbowe na mtei wanavyotaka kuwaburuza vijana waliochaguliwa na wananchi kuwawakilisha na sasa wanataka kuwatumia kutimiza haja zao na si maslahi ya wananchi waliowachagua.


Ni haki yao kupinga. Demokrasia ndani ya CHADEMA iko wazi. Kama kweli walikuwa na ubavu wa kumpinga Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa CHADEMA, wangekwenda Bungeni siku hiyo na KUBAKI ndani wakati JK alipohutubia! Huo ni unafiki!

Unasema unampinga Mwenyekiti, unakipinga CHADEMA, halafu hufanyi vitendo? Khaaa!

Uchuro!

Watanzania waoga sana! Ningependa kujua majina yao niwanange hapa LIVE! Wekeni majina yao tafadhali! Mnawaficha nini? Hawa si watu makini, HAWATUFAI ndani ya CHADEMA! Inawezekana ndio hawa wale Wabunge Mamluki waliopandikizwa na CCM, kuja kuivuruga CHADEMA!

Tuko makini, hamtuwezi!
 
Vyombo vya habari hasa Magazeti mengi yako mikononi mwa Ccm yanaandika kile CCM wanataka. Na nia ya CCM ni kuhakikisha wanaisambaratisha CHADEMA. CCM wanataka kuwagombanisha CHADEMA wenyewe kwa wenyewe. Na inataka kuwa chochea wapiga kura ili waone CHADEMA ni chama kisichofaa. Hivyo Wana CHADEMA wawe waangalifu kwa kila hatua watakayochukuwa kudai haki. Mimi na wenzangu tunaikitakia mema Chama cha CHADEMA.
 
Kupishana kimawazo na approach za mambo kupo ila ni muhimu kuheshimu msimamo wa chama kama chama.Walivyofanya ilikuwa sawa sasa hao ambao hawakutaka wakaanza kusema kwa vyombo vya habari itakuwa si sahihi na itakula kwao.Naamini watauheshimu msimamo wa chama.
 
Ni akina nani? Wataje basi. Mbona hawakubaki mle bungeni siku hiyo? Hakuna mbunge aliyelazimishwa kuondoka mle mjengoni.........hizi ni porojo tu za akina Chiligati na Tambwe.

Tambwe hakuwepa viti maalumu vya wanawake CCM? Mmmh......
 
mi ata nashangaa wanaompinga mwenyekiti wanamaanisha nin......maana hapa lengo ni kujipanga kwa lolote ili ikiwezekana basi kwa mwaka 2015 tuwe na tume huru na katiba iwe imerekebishwa.....na ndio vita tuliyoianza ili kufikisha kilio chetu.......sasa kama wana dhan haki inakuja tu bila kuipigania watoke chadema maana sisi tunataka mapinduzi ya kweli na sio kuchekeana wakati mtu anakuchakachulia matokeo yako!!!!
tukianza kucheka nao utakuta mwaka 2015 wanafanya tena ujinga wao wakiwa na tume na katiba zao za kichina.......
zanzibar wamepigana kwa kutowatambua marais mara mbili na mwisho wamefika walipotakiwa kufika baada ya ccm kupewa shinikizo kutoka nje!
ata pia namshangaa rashid kwa kusema mgomo wa kumtambua rais upande wa zanzibar haukuwasaidia.......ndio wale wanafiki wanaoficha ukwel........ccm sio wa kukubali serikali ya mseto kwa urais kama unavyodhan..........
bila strategy tena za kisomi kama wanazozitumia chadema tena kwa kuanza mapema kama wanavyofanya..... hatutaweza kufika!
pamoja kwa nguvu ya shule na umma tutafika.......wasomi chadema endeleeni kuumiza kichwa na mzibane korodan za ccm kila inapobidi ili kilio kifike
 
Wataje kwa majina ili tujue! Vinginevyo habari yako ni mashikoless na inafaa kupelekwa kona za udaku sio hapa!
 
Kumbe wanaoitakia mabaya chadema wako wengi
Yaani huu udhalimu wa CCM hamuuoniiiiiiiiiiiiiiiiiii.
Naona fedha zinawafanya muwatete CCM bila haya au sio watanzania ninyi?
 
Sikuwaona wabunge 11 wa chadema walobaki kusikiliza hotuba bungeni. Huo ni uongo ambao si wakuuleta jamvini.
 
Hawakufika kabisa bungeni, hii inaonyesha ni jinsi gani mbowe na mtei wanavyotaka kuwaburuza vijana waliochaguliwa na wananchi kuwawakilisha na sasa wanataka kuwatumia kutimiza haja zao na si maslahi ya wananchi waliowachagua.

.
Nani kakuambia kuwa hawawakilishi masilahi yetu wananchi? Kama kuna jambo la maslahi kwetu namba moja ni mabadiliko ya katiba. Hii katiba ndio kizuizi kikuu cha demokrasia ya kweli nchini. Hivyo sisi wananchi tuliowachagua wabunge wetu tunaona fahari kwa wabunge wa chadema kwani wameanza kwa kushughulikia kipaumbele namba moja. Wakifanikiwa kwa hili la katiba basi yale mengine yatarekebika kirahisi zaidi.
 
Back
Top Bottom