Chadema wafungua kesi ya kikatiba kupinga uandikishaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema wafungua kesi ya kikatiba kupinga uandikishaji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Balantanda, Oct 13, 2009.

 1. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimefungua kesi ya kikatiba dhidi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupinga kuendelea kwa kazi ya undikishaji watu katika daftari la kudumu la wapiga kura.

  Hatua hiyo ya Chadema inakuja wakati tayari watu kadhaa wamekwisha jeruhiwa na huku baadhi ya nyumba kuchomwa moto kutokana na kuwepo kwa vurugu zilizotokea kwa nyakati tofauti kwenye baadhi ya vituo vya kujiandikisha visiwani Pemba
  Vurugu hizo zilitokana na baadhi ya wananchi kulalamikia kitendo cha kunyimwa vitambulisho vya ukazi(ID),ikiwa ni moja wapo ya sharti kuu la kupata fursa ya kuadikishwa katika daftari hilo.

  Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willbrod Slaa aliiambia Mwananchi juzi kuwa kesi hiyo ilifunguliwa Ijumaa iliyopita katika Mahakama Kuu ya Zanzibar.

  "Tumekwenda mahakamani ili haki itendeke. Nchi hii inaendeshwa kinyume cha sheria, hivyo ni lazima watu waende mahakamani ili kuhakikisha haki na sheria zinafuatwa," alisema Dk Slaa na kuongeza;
  "Hatuwezi kujingamba kimataifa eti nchini kuna haki wakati kitu hicho hakuna na hakipo."

  Mbali na kutaka kusimamishwa kwa kazi hiyo pia wanataka Tume ya Uchaguzi Zanzibar(Zec) pamoja na wadau kutoka vyama vya siasa wakae pamoja kuzungumzia suala hilo.

  Jumanne iliyopita chama hicho kiliandika notisi ya dharura kwenda Ikulu ya Zanzibar kuonyesha dhamira ya kuishataki serikali. Notisi hiyo hutolewa kwa siku mbili.

  Kwa mujibu wa Chadema ndani ya siku hizo mbili serikali haikujibu notisi hiyo.

  "Baada ya kupita siku hizo mbili hatukujibiwa, lakini tukashindwa kufungua kesi hiyo siku ya Alhamisi kutokana na mwanasheria wetu Ally Omari Juma kuugua gafla," alisema Dk Slaa.

  Kwa mujibu wa hati ya mashtaka Chadema imefungua kesi hiyo ya kikatiba kwa madai kuwa serikali imevunja ibara ya 5 ya katiba ya Zanzibar ibara ndogo (1)na (2) katika vipengere vya a,b,c na d.

  Pia imevunja katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 katika kipengere kinachohusu uchaguzi ambacho wanadai kuwa hakuna hata sehemu moja inayoonyesha na kueleza kuwa unapokwenda kujiandikisha katika daftari la kupigia kura ni lazima uende na kitambulisho cha ukazi (ID)

  Hata havyo Dk Slaa alisema uamuzi wa chama chake kwenda mahakamani ni kwa kuwa suala hilo ni la kikatiba.

  "Watu wengi kila kukicha wanataka twende mahakamani kushitaki mambo yanayohusu EPA, lakini wanashindwa kuelewa kuwa hizi ni kesi za jinai hivyo mwenye mamlaka ya kufungua kesi hizi ni serikali tofauti na hii ya kwetu ambayo ni ya kikatiba," alisema Dk Slaa.

  Katika hatua nyingine Dk Slaa amesema uchaguzi wa serikali za mitaa na vitongoji unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 hautakuwa wa haki ila utakuwa ni wa wizi.

  Dk Slaa alisema hali hiyo inatokana na hali halisi ya kimazingira iliyojitokeza katika uandikishaji ulioanza Oktoba 4 na kumalizika Oktoba 10 nchini kote.

  "Hakuna uchaguzi wa haki hapa ila ni wizi mtupu, iko wazi tu Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) imeegemea upande wa CCM tu na si vinginevyo," alisema Dk Slaa.

  Source: Gazeti la Mwananchi
   
 2. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Chadema mwisho wenu ni Chumbe...!
   
 3. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  CUF walipaswa kuifungua kesi siku ya kwanza ya uandikishwaji,why wapo kimywa kwenda mahakamani kama Chama kikuu cha upinzani ZNZ hadi leo?

  Sheria iliyotungwa na bunge lolote lile duniani linaipa nguvu mno katiba dhidi ya sheria ndogondogo za utendaji;kama katiba inasema kupiga kura ZNZ inatakiwa mtu awe na miaka 18 na mwenye akili timamu,then sheria ndogo ya uchaguzi inasema kupiga kura ZNZ inatakiwa uwe na Zan ID na uishi sehemu moja miaka 5,basi ni sheria iliopo ndani ya katiba mama ndiyo itetekelezwa,kwa maana hiyo basi kumtaka MZNZ awe na Zan ID ndiyo aandikishwe kupiga kura ni kinyume cha katiba!

  CUF wasijidanganye kama watashinda ZNZ wakiaacha CCM iamue nani aandikishwe na nani asipige kura mwakani;waende nao mahakamani sasa hivi na nina uhakika jaji atatengua hii sheria ya Zan ID maana hata hakimu wa mahakama za Mwanzo wanajua nini kifuatwe kama kuna mgongano wa kikatiba!

  CCM wanajua hawawezi shinda ZNZ lkn kwa hila hii tutegemee hadi kuchukua majimbo baadhi ya Pemba,CUF changamkeni!
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Oct 14, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kuna mengine jamani hata hayaleti mantiki..
  Hivi kweli Chadema wanataka watu wakubaliwe kujiandikisha ktk daftari la wapiga kura pasipo kitambulisho cha ukazi?..
  Hivi kweli kama itakubaliwa hivi hawawezi kuona kama itakuwa safi sana kwa CCM ambao wana umewe wa kusomba watu toka kila kona na kijiandikisha kila kata na jimbo maadam hakuna kitambuliko cha ukazi..
  Nijuavyo mimi hakuna nchi yoyote inayomkubali mtu kujiandikisha ktk daftari la kupiga kura kama wewe sii mkazi unles kuna utaratibu unaohakikisha mtu hawezi kupiga kura sehemu mbili.
  Kisha basi kuna mambo mengi Tanzania ambayo huwezi hata kupata Pasi wala kibali kama hujachukua barua ya utambulisho toka kwa katibu kata au mjumbe wako kuwa wewe ni raia na mkazi wa sehemu fulani...
  Ningependa sana kufahamu ni utaratibu gani unatumika kumzuia Mrundi/Mkenya asiyekuwa raia kutojiandiksha ktk daftari la kupiga kura ikiwa kitambulisho cha ukazi sii hoja!
   
 5. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  Mkandara somehow you right, but you miss some very crucial point ktk kuwa na Zan ID ili kujiandikisha kwa wakazi wa ZNZ.

  Kinachofanyika ZNZ sasa ni ukikukwaji mkubwa wa katiba;katiba mama ya ZNZ na ya Jamhuri inataka kwa uwazi kabisa sifa za kujiandikisha kupiga kura ZNZ na kama kuna mgongano wa kikatiba basi mambo yote yanaachwa na kufuatwa mambo yaliyo ndani ya katiba na wala sio mambo yaliyotungwa ili kurahisisha utendaji!Msingi wa kesi ya CUF ungeanzia hapo.

  Sasa kama wanataka ku-implement hii sheria wabadili kwanza katiba,na waseme kwenye hiyo referendum wazi kuwa kupata Zan ID watendaji wataangalia sura za wana ZNZ ambapo ukiwa mfuasi wa CCM unapata kiurahisi hiyo Zan ID na ukiwa mwana CUF wanakuzungusha!

  Mambo haya ya ukiukwaji wa katiba mama na ubaguzi wa kupewa hiyo Zan ID ndiyo ninayoyasemea hapa na wala sio umuhimu wa ID kwa watz wote;ukweli ni kuwa ID ni muhimu sana kwa utambulisho na mustakabali wa Taifa letu!
   
 6. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Nadhani hiyo Zain I'd ndiyo tatizo, kwa nini wengine wapewe na wengine wakose!? Ni bora tungekuwa na I'd moja ya utaifa wa Tanzania na hiyo ingerahisisha kila kitu yaani ndio ingekuwa kadi ya kupigia kura n.k.
   
 7. K

  Kinyikani Member

  #7
  Oct 14, 2009
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 65
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Sasa huyu anayetowa hivi zan ID si ndio huyo huyo CCM ??? sasa si ndio maana hawapewi wale wote wanao onekana kuwa ni wapinzani. bro nafikiri ama unababaisha watu ama huwajuwi CCM na hata ukenda Mahakamani ni kupoteza wakati maana hata hiyo mahakama utakutana tena na Mi CCM tu huko.
   
 8. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #8
  Oct 14, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kwani 2005 tulipojiandikisha kupiga kura tulitumia ID na mbona ulikuwa hujashangaa miaka yote hiyo? and by the way why this is not happening in mainland ?au huku si sehemu ya Tanzania?
   
 9. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #9
  Oct 14, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kuna wakati fulani kesi kama hizi zinaweza kuleta hali fulani ya kujua watu wana wajibu wa kujua mambo muhimu sana katika Taifa hili na kuona mambo yanakuwa muhimu sana katika Taifa letu
   
 10. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #10
  Oct 14, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Chadema wakati mna endesha kesi hiyo huko na huku bara tunapenda kuona kesi ya dhidi ya Tume ya Uchaguzi na matendo yake ni muhimu kabla ya uchaguzi .
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  Oct 15, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kigogo,
  Mkuu nachotazama mimi ni ufanisi wa Upigaji kura. Kweli Dr. Slaa ana haki ya kufungua kesi kikatiba yaani kama imeruhusiwa Ushoga basi sii kosa kwa Padre kusimamisha kesi mahakamani lakini nachozungumzia mimi ni huyu Dr. Slaa mbali na katiba kutazama nafasi alosimama - Practice what you Preach.

  Mwaka 2005 Chadema, CUF na TLP wote hawa walipigwa na kombora la watu kujiandikisha kila kona na kuiweka CCM ktk ushindi mkubwa wa kishindo. I believe Mbowe asingeshindwa kiasi hicho pasipo mchezo huu.

  Na makumbuka vizuri jinsi CUF walivyopiga makelel na hata baadhi vijana wao kuuawa.. source ya vurugu zote visiwani ilikuwa watu wasiokuwa wakazi kwenda kupiga kura ktk sehemu ambazo wao sii wakazi..ina maana vijana wa CUF waliwahi kulishtukia hilo.

  Sasa tumejifunza kitu gani na leo tunaomba ama tunaenda mahakamani kwa sababu gani? Kusimamisha sheria ambayo ilitukana wote.. Pili, ni vyombo hivi hivi vya CCM, CUF na Chadema waliokubali kuchapishwa kwa kadi za Ukazi ikiwa na lengo la kuondoa tatizo hili.. sasa kadi zimetolewa na wananchi wote wakazi wa ZNZ wamepewa iweje mtu anayeishi dar abanataka kujiandikisha ZNZ kwa sababu katiba haijabadilishwa? wakati mnapitisha uchapishaji wa kadi za Ukazi walikuwa wakifikiria kitu gani kitafanyika!

  Ikiwa kujiandikisha ktk daftari la Upigaji kura unafanyika kwa kuwakataa wananchi wwenye kadi au kwa bahati mbaya hawajapewa hizo kazi za Ukazi nitawaelewa lakini siwezi afiki mtu anayeishi dar kuja jiandikisha ZnZ pasipo kumkataza mtu huyo huyo kupiga kura Dar na ZnZ yaani sehemu mbili.. Tunarudi ktk tatizo lile lile.

  Kisha mh. Dr. Slaa amezungumzia pia mambo ya Ufisadi kuwa ni maswala yasiyohusiana na katiba.. yaani kweli mnattaka kunambia WIZI na mikataba mibovu sio swala la Kikatiba?..Sasa utaweza vipi kumpeleka mwizi wa EPA mahakamani ikiwa kiongozi wetu kama Dr. Slaa anadai sio swala la Kikatiba! Katiba kazi yake sii kutunga sheria jamani iweje wizi wa EPA, wizi ambao yeye alikkuwa kinara hauhusiani na katiba!
  Jamani nachoka na wanasiasa wa Kibongo!
   
 12. M

  MLEKWA Senior Member

  #12
  Oct 15, 2009
  Joined: Aug 18, 2007
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nafikiri hapa ndio Wazanzibari sikue zote hujionawao sio Watanzania kwani serikali ya muungano imenyamaza kimya na unyanyasaj iwa Wazanzibari toka 1964 , Wapemba walipokimbilia Tanga na Kigamboni na Kule Tandika leo ndio hao hao wanojenga magorofa Kariakoo na wengi hata ukawakata kichwa hawataki kurudi visiwani kwa khofu ya ubaguzi , huko kulikua hakuna kufaulu mtihani kuenda shule bali baba yako akiwa ali kuwa mfuasi wa Mapinduzi basi wewe unachaguliwa kuendelea na masomo hata ukiwa umefaulu zero ndio ukaona miaka ya sabini utitiri Wa wazanzibari umekimbilia bara na leo musishangae maelfu ya wazanzibari kukimbilia bara kwani Zanzibar ni Visiwa vyenye giza nene. bado nafasi za juu kielimu zinatolewa kwa kuwa mfuasi wa chama gani , ajira uwe mfuasi wa CCM yale yale yaliotokea enzi zile wafuasi wa Mrema kuwekewa zengwe makazini ndio yanayowakuta wanangangari visiwani.
   
 13. K

  Kinyikani Member

  #13
  Oct 15, 2009
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 65
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  bro, kakwambia nani kama wakaazi wote wamepewa ID au wewe ndio uliozitowa sasa watu makelele yote hayo wanayopiga kwamba hawapewi ID zina tolewa kwa ubaguzi tu kama wewe ni CCM utapewa mpizani hakuna. alooo!!! basi kama hujuwi hii ndio mbini ya kuiba kura ukisha kuwazuiya kuandikisha basi huhitaji tena vifaru 2010 ama nyinyi Ma CCM ni sawa sawa na MA Israel kazi ni kupindisha maneno tu.
   
 14. Mateso

  Mateso JF-Expert Member

  #14
  Oct 15, 2009
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 244
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mnakumbuka shuka wakati kumekucha. Mlikuwa wapi tangu zoezi hili lianze? Watu wamepigwa kama punda, nyumba zimechomwa moto ndo manakurupuka saa hizi. Hatudanganyiki. Kama katiba ya JMT ya 1977 haionyeshi mahali panapotaka mtu awe na kipande wakati wa kujiandikisha haijazuia tume kuweka taratibu za kujiandikisha. Kwani kuna mahali imeizuia tume kuweka taratibu za kujiandikisha? Ibara ya 74(14) inasema hivi ''Katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa katiba hii, Tume ya uchaguzi haitalazimika kufuata amri au maagizo ya mtu yeyote au idara yoyote ya serikali au maoni ya chama chochote cha siasa.Sasa wewe unatoa wapi haya yako. I think and do hope that the grounds of your petition are baseless and at the same time you dont have locus stand. Any lets wait the decision of the Constitutional Bench.
   
 15. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #15
  Oct 15, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Na nyie hebu kubalini mfanye uchaguzi huru na wa haki,muwone itakuwaje, majimbo yenu matano hayatazidi...labda mfanye Kisonge na Kachorora kuwa majimbo ndo yawe saba, ibeni tu, lakini hakuna mwenye haja na CCM Zanzibar...mnaanzia bara tu, mwisho wenu chumbe.
   
 16. MwanaCBE

  MwanaCBE JF-Expert Member

  #16
  Oct 15, 2009
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,773
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Thank you CHADEMA.
   
 17. M

  Mkandara Verified User

  #17
  Oct 16, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  mkuu swala sio ID ila ni uandikishaji ktk daftari la kudumu ni lazima uwe na Id ya Ukazi.. Hakuna mashtaka yanayohusu Id kutotolewa kwa Wakazi wa Zanzibar..Huna Id kwa nini uandikishwe kupiga kura! Ebu wee nambie sababu gani waandikishwe watu ali mradi mtu anadai yeye ni mkazi wa Zanzibar, hata akitokea bara poa tu maadam yeye ni Mzenj sijui wa passport au uzawa...
   
 18. SYLLOGIST!

  SYLLOGIST! JF-Expert Member

  #18
  Oct 16, 2009
  Joined: Dec 28, 2007
  Messages: 306
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  Wakuu,
  Haya yanayodaiwa na Chadema ni yanayodaiwa na wananchi-Chadema ni wakala wa Wananchi.

  Sidhani kama wanapinga uandikishaji, bali waomba kusitisha uandikishaji huo kwa sasa, sababu ikiwa ni huo ukazi(ID)

  Haya matatizo ya kupinga,kusitisha etc...ya uandikishaji yapo tu- sehemu nyingi tu hapa duniani hata kwenye demokrasia zilizokua-na ni mara nyingi haya yanatokea wakati unakaribia uchaguzi au wakati wa uchaguzi.

  Madai haya lazima yapewe kipaumbele ikiwa Tanzania inataka kuheshimiwa kwa demokrasia changa na inayokuwa na demokrasia ya kweli!

  Walikuwa wapi lakini siku zote?
   
 19. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #19
  Mar 5, 2016
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  hgfgvvffcvvvvb
   
 20. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #20
  Mar 5, 2016
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,947
  Likes Received: 1,507
  Trophy Points: 280
  Toka lini Chadema wana uchungu na Zanzibar?pilipili wale wengine kuwashwa wawashwe Chadema
   
Loading...