George Maige Nhigula Jr.
JF-Expert Member
- Mar 14, 2008
- 470
- 149
Ndugu wana JF,
Napenda kutoa maoni yangu huru juu ya umuhimu wa CHADEMA kuhamishia makao makuu ya chama Kanda ya Ziwa na ofisi kuu ndogo kubaki Dar es salaam na mbeya kwa nyanda za juu kusini.
Hii itakuwa ni mkakati wa makusudi kukifanya chama kuwa karibu na zones za wapiga kura wengi na walio kanda ya ziwa na nyanda za juu kusini na kuweza ku penetrate vijijini ambako ndio iwe road map ya ushindi wa viti vingi vya serikari za mitaa na uchaguzi mkuu 2014 na 2015 respectively.
Hii itaonesha nia thabiti na utashi wa kisiasa wa chadema kuwa karibu na wapiga kura wengi hususani kanda ya ziwa yaani mwanza, shinyanga, mara, kagera, kigoma na Tabora. na ofisi kuu ndogo Mbeya itasaidia kuhudumia mikoa ya mbeya, iringa, ruvuma, Rukwa na baadhi ya mikoa ya kusini kama mtwara na lindi, hali kadhalika ofisi kuu ndogo ya Dar es salaam, itahudumia mikoa ya dar, pwani, Tanga, morogoro, na kanda ya kati na kazikazini.
Strategy hiyo itaweza kuwaonesha wananchi wa maeneo hayo kuwa Chadema inawathamini na inakwenda kwa wapiga kura sio kulindikana Dar es salaam kama vyama vingine vingi vilivyorundikana Dar es salaam,
Hali kadhalika Chadema watumie RUZUKU watakazozipata kipindi hiki kujenga majengo ya Makao makuu mwanza yenye hadhi ya kuwa kitega uchumi cha chama na sisi wanachama tutajitolea michango ya hali na mali kwa ujenzi wa ofisi za makao makuu ambayo itakuwa landmark ya mapambano ya kuiondoa ccm madarakani 2015, na kuendelea kujenga majengo yatakayokuwa landmark ya chama kwenye ofisi ndogo kuu za kanda Dar es salaam na mbeya.
Hatutaki kuiona chadema inakuwa na sura ya kimaskini wakati uwezo wa kuwekeza kwenye majengo ya kisasa na headquarters za kisasa tunao, hiyo headquarter ya CHADEMA pale kinondoni haifai kabisa kwa hadhi ya chama kikuu cha upinzani Tanzania, hivyo is time now kubadilisha sura na muonekano wa chama towards 2015.
Napenda Mh. Mwenyekiti Freeman Mbowe atumie nafasi hii kwa kuonesha mfano wa kutenga nusu ya 100milioni anazopata kama kiongozi wa upinzani bungeni zichangie ujenzi wa makao makuu ya chama ya kisasa mkoani mwanza, na percentage flani ya ruzuku itengwe kuchangia mfuko huo wa ujenzi wa makao makuu ya kisasa na wanachama tuhamasishwe kuchangia ujenzi huo na mimi nitakuwa mstari wa mbele kuchangia na kutafuta wazamini.
Tunaomba watalamu ambao ni wapenzi wa chadema hapa JF waje na master plan ya majengo hayo ambayo yatakuwa na ofisi, kumbi za mikutano na hoteli za kimataifa, na shopping malls, lengo ni kuwa na headquarter ambayo itakuwa kitega uchumi cha chama, chadema need to aim higher hivi sasa wakati wa small plan imepita lazima tuje na big plans na watueneshe wananchi kuwa wako serious na kujenga chama chenye sura ya kitaifa na kujikita kwa wananchi ambao ndo wapiga kura.
Haya ni mawazo yangu huru, Naomba kama kuna mdau ana mawazo tofauti au ya kuboresha zaidi idea basi tujadiliane, pesa za ruzuku lazima ziwe invested kwenye kujenga ofisi za kudumu za chama, kuna wazalendo watajitolea hata viwanja kwani vuguvugu la ukombozi limepamba moto na wakati wa kufanya mambo makuubwa ni huu.